RC Kunenge kufanya hivyo ni sawa na kuwafukuza Machinga Dar es Salaam

Machinga tunawatambua kuwa ni mojawapo ya kundi ambalo linapigika sana kimaisha kutokana na sera mbovu za chama tawala. Lakini pia na wao watambue kuwa wanapaswa kufuata taratibu na sheria zilizopo wanapiendesha shughuli zao za kubangaiza.

Ni lazima kabisa watambue wao ni wahanga wa matamko ya kisiasa, kwa ni lazima wacheze mziki kutokana na midundo ya ngoma. Wasijisauhilishe kuwa maisha yao ya kijasiriamali yalianza kipindi cha utawala wa mwendazake.

Waende mbali na wakumbuke wakati wa kipindi cha Mkapa, Kikwete, Mwinyi na hata Kambarage walikuwa na huo uhuru wa kufanya biashara kiholela na kwa kutokuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa? Ni lazima mtambue mwendazake aliwaingiza chaka kwa kutowapa ushauri mzuri wa kuendesha shughuli zenu kwa utaratibu unaofaa.

Kilio cha machinga kitakuwa na mantiki tu endapo kitakuwa ni kwa serikali ngazi zote kuwatafutia maeneo maalum ya wao kuendesha shughuli zao pasipo kuwa bughudha yoyote ile. Lakini nje ya hapo kitu chochote kile kikiwekwa ktk eneo kisipostahili kuwepo na kuwa kero kwa watu wengine ktk lugha ya jumla tunaita ni "takataka", kumradhi kwa neno hili ashakum si tusi.
 
Kwamba lile gari la matangazo lililokuwa linapita lilipotea njia? Anaogopa kutumbuliwa tu huyu kune boy......ilani kero sana kwenye barabara na maeneo ya vituo ya daladala, kuna wachoma mihogo, vitumbua ,chipsi yaani ni hatari tupu kwa watimiaji wa maeneo hayo.....na hata abiria wa daladala akisimama unashangaa wanakwambia unazuia wateja toka mbele.

Tuache siasa kama taifa tuwe serious kwakweli na baadhi ya mambo, mji unatia kinyaa
Alichoongea Kunenge na hilo gari la Matangazo kuna tofauti gani?
Wameongea kitu kimoja kwa maneno tofauti
 
Wananchi wote tufuate sheria za miji bana....asiyeweza arudi vijijini kufanya kufanya kilimo. Kwani walioko vijijini sio watanzania? Mambo ya kudekezwa watu kuvunja sheria,kwa mtaji wa siasa haitasaidia kwa maendeleo endelevu....tusidanganyane.
Atakayebaki mjini hadi mwezi wa saba huyo mwanaume
 
Back
Top Bottom