RC Kunenge kufanya hivyo ni sawa na kuwafukuza Machinga Dar es Salaam

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Kwanza wasizibe njia za waendao kwa miguu, barabara za Mwendokasi na Barabara za Magari mengine

Pili wasifanye biashara mbele ya wafanyabiashara wengine

Tatu msijenge vibanda vya kuuzia biashara na kujikinga na mvua na jua

Mwisho wasipikie mihogo na vitumbua kwenye msongamano wa watu.

Kama mambo yote haya utayakamilisha ipasavyo basi ni kama vile umetangaza kuwafukuza Machinga Dar kwakuwa hizi zote ndio tabia halisi za machinga kwenye mazingira ya jiji, na ndizo zinazowafanya waitwe Machinga.

Bahati mbaya Wamachinga wamelelewa hivyo kukoka moto popote na kupika chochote hata kwenye barabara iendayo airport.

Hakuna namna tusimung'unye maneno, Machinga wafanyekazi halali kwenye maeneo halali.
 
Kwamba lile gari la matangazo lililokuwa linapita lilipotea njia? Anaogopa kutumbuliwa tu huyu kune boy......ilani kero sana kwenye barabara na maeneo ya vituo ya daladala, kuna wachoma mihogo, vitumbua ,chipsi yaani ni hatari tupu kwa watimiaji wa maeneo hayo.....na hata abiria wa daladala akisimama unashangaa wanakwambia unazuia wateja toka mbele.

Tuache siasa kama taifa tuwe serious kwakweli na baadhi ya mambo, mji unatia kinyaa
 
Tatizo Sisi wafanya biashara ndogo ndogo(machinga) tuliichukulia tofauti kauli ya hayati yakutaka tufanye biashara popote majiji na miji vimekuwa kama minadani Hakuna sura ya miji wala majiji...tumesahau kama Kuna sheria ndogo ndogo za miji...pia hawa wanasiasa nao ni wanafiki tu walikuwa wapi kusimamia izo sheria za miji wakati magufuli akiwa hai? Japo ni sheria lakini italeta chiki sana kati ya serikali ya Samia na wanachi
 
Iko siku wamachinga watakuja kuleta balaa kubwa hapa nchini. Akishalipishwa 20,000 basi anakoka moto hata kwenye nguzo za umeme, wanapanga bidhaa hata kwenye stendi za magari na ukikanyanga bidhaa yake vurugu inaanzia hapo, iko siku machinga watautia moto mji mzima. Idadi ya watoto wanaohamia mijini kutoka vijiji inaongezeka kila siku.

Wanasiasa wamefilisika kimaono kabisa, badala ya kuwapa vijana mitaji wakalime, kufuga, na kuvua wanawadanganya watoe 20,000 ili wafanye Kazi yoyote popote bila kubughudhiwa.
 
Mambo kama haya ndio hupima uwezo wa viongozi. Bwana fulani yeye alichukua njia rahisi ya kupata umaarufu at the expense of sustainability.
Hata mkiendelea kumlaumu Mwendazake bado haitatuondolea tatizo la wamachinga. Wamachinga wamekuwepo tangu awamu ya pili. Tatizo letu ni kwamba hatutafuti solutions za muda mrefu, and ni sustainable kuweza kulipatia ufumbuzi tatizo la wamachinga. Unapowazuia na kuwafukuza mabarabarani, unawapeleka wapi wakafanye biashara zao za kujipatia riziki? Kumbuka wamachinga ni ajira isiyo rasmi ambayo pengine inaweza kuzidiwa na kilimo peke yake kwa wingi wa wahusika. Tukiwafukuza na kuwaacha wazurule mitaani maana yake tunatengeneza jeshi la vibaka, wabwia unga, wezi, nk.
Ni lazima tuje na mipango madhuhuti ya kuwahakikishia usalama, haki, na sustainable solutions za kuendesha maisha yao.
 
Wananchi wote tufuate sheria za miji bana....asiyeweza arudi vijijini kufanya kufanya kilimo. Kwani walioko vijijini sio watanzania? Mambo ya kudekezwa watu kuvunja sheria,kwa mtaji wa siasa haitasaidia kwa maendeleo endelevu....tusidanganyane.
 
Unadhani hiyo solution yako kuwarudisha kijijini wakafanye kilimo ni sustainable kwa kiasi gani?
 
Fukuza kabisa machinga , hawa watu ni Kero kubwa , watengewe maeneo kama hawataki , bas wabaki kwenye minada , hii nchi kama tupo jalalani
 
Ni lazima tuje na mipango madhuhuti ya kuwahakikishia usalama, haki, na sustainable solutions za kuendesha maisha yao.
Hapana, mtu atoke kijijni aje mjini kuuuza vitu barabarani? Hapana, Magufuli aliwaendekeza kutafuta cheap popularity madhara yake ndiyo haya!
 
Ifike wakati nchi iongozwe kwa sheria na siyo mapenzi ya mtu eti kisa anatala kutufurahiaha hata kama tunavunja sheria
 
Hoja dhaifu

Ndo matokeo ya kusoma vitabu vya Ulaya halafu uje kutatua matatizo ya Afrika. Halafu hapo ongeza na ukosefu wa ubunifu na uvivu wa kufikiri

Lengo la #jiwe ni zuri. Kama watendaji wanakosa jinsi ya kulishughulikia kitaalamu hayo ndo matokeo ya ubovu wao
 
Hamuondoi machinga lakini, Kwanza wasizibe njia za waendao kwa miguu, barabara za mwendo kasi na barabara za magari mengine, pili wasifanye biashara mbele ya wafanyabiashara wengine, tatu msijenge vibanda vya kuuzia biashara na kujikinga na mvua na jua; na mwisho wasipikie mihogo na vitumbua kwenye msongamano wa watu. Kama mambo yote haya utayakamilisha ipasavyo basi ni kama vile umetangaza kuwafukuza machinga Dar kwakuwa hizi zote ndio tabia halisi za machinga kwenye mazingira ya jiji, na ndizo zinazowafanya waitwe machinga.

Bahati mbaya wamachinga wamelelewa hivyo kukoka moto popote na kupika chochote hata kwenye barabara iendayo airport.

Hakuna namna tusimung'unye maneno, machinga wafanyekazi halali kwenye maeneo halali.
Sawa, lakini sio kuziba njia za waenda kwa miguu. Utaratibu mwingine inabidi ufuatwe maana sasa naona imekuwa shida.

Tatizo lenu wamachinga hamfuati utaratibu wa kuheshimu waenda kwa miguu na vilevile kuharibu mazingira kwa kuliweka jiji kuwa chafu.
 
Hapana, mtu atoke kijijni aje mjini kuuuza vitu barabarani? Hapana, Magufuli aliwaendekeza kutafuta cheap popularity madhara yake ndiyo haya!
Kwani kikwete alifanya nini kuwaondoa wamachinga? Acha chuki zako kwa mwendazake
 
Hata mkiendelea kumlaumu Mwendazake bado haitatuondolea tatizo la wamachinga. Wamachinga wamekuwepo tangu awamu ya pili. Tatizo letu ni kwamba hatutafuti solutions za muda mrefu, and ni sustainable kuweza kulipatia ufumbuzi tatizo la wamachinga. Unapowazuia na kuwafukuza mabarabarani, unawapeleka wapi wakafanye biashara zao za kujipatia riziki? Kumbuka wamachinga ni ajira isiyo rasmi ambayo pengine inaweza kuzidiwa na kilimo peke yake kwa wingi wa wahusika. Tukiwafukuza na kuwaacha wazurule mitaani maana yake tunatengeneza jeshi la vibaka, wabwia unga, wezi, nk.
Ni lazima tuje na mipango madhuhuti ya kuwahakikishia usalama, haki, na sustainable solutions za kuendesha maisha yao.
Acha kutetea bana.

Mwendazake kaiharibu nchi kwa kuwabeba machinga Popote.
 
Wasukuma sisi ni washamba sana! Nyumba ya Msukuma ukiingia ndani/sebuleni utajua tu hapa ni kwa Msukuma! Vyungu kama vyote vimejazwa sebuleni na mazagazaga yote!
Hayo ndo alikuwa anatuwekea Mwendazake.Nchi yote kuanzia Majiji, Manispaa na Miji yote imekuwa minada ya wananzengo!
 
Back
Top Bottom