Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Wananchi walioambatana na Kihongosi ni kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo wajasiriamali, mama lishe na baba lishe, Vijana wanajishughulisha na usafiri wa bajaji na pikipiki maarufu kama Bodaboda pamoja na wananchi wengine, wakitangaza rasmi kumuunga Mkono Dkt. Samia kutokana na mafanikio makubwa yaliyoshuhudiwa Mkoani Arusha kwa kipindi cha Miaka minne ya Uongozi wake.
Zoezi la kupata wadhamini wa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan linafuatia mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania Urais kwenye Tume huru ya Taifa ya uchaguzi INEC Agosti 09, 2025, Tayari kwa kutetea nafasi yake katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 akiambatana na Mgombea mwenza Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.