Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,542
- 2,172
Akiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Rc Kafulila ameifananisha kasi ya maendeleo inayopigwa na Rais Samia inafanana kabisa na ile ya mashujaa wetu,
" Kumbukumbu ya Mashujaa inatukumbusha historia yetu,
inatukumbusha historia ya wazee wetu na mchango wao wa damu kumkabili mkoloni Tanzania na Afrika;
Kuhakikisha Tanzania huru dhidi ya kila aina ya uvamizi ikiwemo uvamizi wa Idd Amin!
Wazee wetu walifanya Taifa letu kuwa Kitovu cha ukombozi wa Bara la Afrika , tulikua Taifa Kiongozi wa Agenda ya Afrika zama hizo.
Hivyo kumbukumbu hizi sio tu zinatukumbusha historia bali kumbukumbu hizi zinatukumbusha WAJIBU wetu na hasa kizazi cha milenia kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa Taifa Kiongozi katika Agenda ya Afrika kila zama.
Ndio sababu tunampongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa mkakati mkubwa wa kujenga diplomasia yetu na kurejesha Tanzania katika jukwaa la Kimataifa.
Rais wetu anafanya kitu kikubwa sana chenye tafsiri ya kukumbuka mashujaa wetu kwani lengo Lao ndio lengo bado; Kujenga Tanzania kubwa yenye nafasi muhimu kimataifa, kujenga Taifa kiongozi kwa bara la Afrika"- David Kafulila, wilayani Bariadi katika kumbukumbu za mashujaa!.