Robert James Masunga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 414
- 395
aibu sana.
Haya maongezi mubashara yalioneshwa television gani?Ndani ya Sheikh Amri Abeid Arusha. Kuaga miili ya waliofariki kwenye ajali ya basi dogo. Watu 35 wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1 wa Shule ya Lucky Vicent.
Nilikuwa Jukwaa kuu. Karibu na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Muda wa salamu za rambirambi ukafika. Wakuu wa kiserikali na kisiasa wakawa wanakaribishwa. Mkaribishaji ni RC Mrisho Gambo wa Arusha. Mwenyeji
Wasaidizi wa Mama Samia wakapata ujumbe mfupi kutoka kwa Mbowe. Wakamletea Mama Samia. Mama Samia akamuagiza mmojawapo amuite RC Gambo ili amuagize jambo. Jambo muhimu la kisiasa na kiserikali. Amri
Mama Samia,Gambo alipokuja, akamuagiza Gambo awaongeze Mbunge Lema na Meya Lazaro kwa watoa salamu za rambirambi. Wakati huo,mzungumzaji alikuwa Ndugu Simbachawene. RC Gambo akatikisa kichwa kumkatalia Mama Samia. Akina Lema hawakuongezwa
Amri ikakataliwa. Mamlaka ikakosewa. Kinachotakiwa sasa ni kumuondoa Gambo kwakuwa Makamu wa Rais,kama taasisi ya pili ya juu nchini,lazima alindiwe heshima yake. Who is RC!?
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
Wasicho jua watu wengi ni kwamba Gambo kapokea maelekezo kutoka juu Mbinguni kuwa Lema Mbunge wa Arusha mjini asipate fursa ya kuwapa pole wafiwa! Tupo msibani wengine wanawaza kukomoana. Unapo muona RC Gambo na RC BASHITE ujue mkomoaji yupo katikati yao.Bashite alikuwepo Arusha.. yawezekana ni yeye aliyempenyezea Kijana yule..
Mna uhakika kama kweli mh makamu wa Rais alimwambia aongeze majina hayo mkuu wa mkoa?????Ndani ya Sheikh Amri Abeid Arusha. Kuaga miili ya waliofariki kwenye ajali ya basi dogo. Watu 35 wakiwemo wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1 wa Shule ya Lucky Vicent.
Nilikuwa Jukwaa kuu. Karibu na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Muda wa salamu za rambirambi ukafika. Wakuu wa kiserikali na kisiasa wakawa wanakaribishwa. Mkaribishaji ni RC Mrisho Gambo wa Arusha. Mwenyeji
Wasaidizi wa Mama Samia wakapata ujumbe mfupi kutoka kwa Mbowe. Wakamletea Mama Samia. Mama Samia akamuagiza mmojawapo amuite RC Gambo ili amuagize jambo. Jambo muhimu la kisiasa na kiserikali. Amri
Mama Samia,Gambo alipokuja, akamuagiza Gambo awaongeze Mbunge Lema na Meya Lazaro kwa watoa salamu za rambirambi. Wakati huo,mzungumzaji alikuwa Ndugu Simbachawene. RC Gambo akatikisa kichwa kumkatalia Mama Samia. Akina Lema hawakuongezwa
Amri ikakataliwa. Mamlaka ikakosewa. Kinachotakiwa sasa ni kumuondoa Gambo kwakuwa Makamu wa Rais,kama taasisi ya pili ya juu nchini,lazima alindiwe heshima yake. Who is RC!?
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha)
Hayo yamezungumzwa...na haya lazima yazungumzwe kwa kuwa yana athari zake pia.Swali la muhimu kabisa, tutadhibiti vipi hizi ajali,silioni.
Ila nani aliitwa kutoa ngonjera na nani hakuitwa naona sana mazungumzo yake.
Inaonyesha jinsi gani jamii yetu inavyojali ngonjera na risala kuliko kutatua matatizo.
Lakini unaonaje lema kutokupewa haki yake ya kiprotokali ya kutoa neno akiwa ni mbunge mwenyeji?Mna uhakika kama kweli mh makamu wa Rais alimwambia aongeze majina hayo mkuu wa mkoa?????
Acheni ushabiki wa kipuuzi, mkuu wa mkoa hawezi kunkatalia mtu anayeto ndani ya mamlaka yake ya uteuzi
Makamu wa Rais yupo ndani ya taasisi ya Urais
Tuache kushabikia mambo yasio na tija,
Uwiiiiiiii, wamekoma huko walikoNinyi nyote huwa nawafananisha na kopo la kuchambia kazi yenu ni moja tu kusafisha uchafu matak*ni na kuyaacha mat*ko yakiwa safi. na mnaiweza kazi hiyo hongereni kwa umahiri mkubwa.
Na hiyo ndiyo ingekuwa funzo kwa Gambo.Lakini mama naye muoga.
Lakini unaonaje lema kutokupewa haki yake ya kiprotokali ya kutoa neno akiwa ni mbunge mwenyeji?
Ukiacha ushabiki pembeni.
Unajua kusoma?
Mimi sioni umuhimu wa mwanasiasa yeyote kuongea katika msiba, labda kama msiba wa mwanasiasa mwenzao na wanaongea kwa kuwa wanamuongelea mtu wa kada yao.
Vinginevyo, msiba wa raia, haitakiwi rais, mbunge, mkuu wa mkoa au mwanasiasa yeyote kuongea.
Wanasiasa wakitaka kuongea wafanye press conference zao. Watoe hotuba zao, kwao, si msibani.
Kwa sababu wakisema maneno msibani, wataugeuza msiba kuwa sehemu ya siasa na hilo litaondoa maana ya msiba ya kufariji waliofiwa. Watu ndiyo wataanza kuongea siasa za vyama.
Sasa hapo sijabagua chama, nimewalundika wanasiasa wote.
Tangu awali.
Nakushangaa unanipa majina ya wanasiasa fulani wa chama fulani kama nimetetea wanasiasa wa chama fulani.
Ndiyo maana nikauliza, unajua kusoma?