RC Chalamila: Uwa nashangaa kuona Wanafunzi Dar wanakaa chini wakati kuna DC na Ma-DED

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kuwa anashangaa kuona taarifa zinazohusu wanafunzi katika baadhi ya shule zilizopo mkoani Dar es Salaam wakikaa chini, licha ya kuwepo kwa viongozi kama Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya na Maafisa Elimu.

Amesema kuwa changamoto hiyo siyo matokeo ya ukosefu wa fedha, bali inasababishwa na kukosa mipango ya muda mrefu.

“Nataka niwathibitishie kuwa wanafunzi kukaa chini siyo ukosefu wa fedha, bali ni ukosefu wa mipango,” amesema RC Chalamila.

Hayo ameyaeleza Februari 12, 2026, alipokuwa katika ziara yake Wilaya ya Kinondoni, ambapo alikagua miundombinu katika Shule ya Sekondari Tarimba Abbas ambayo inajengwa.

Ikumbukwe kwamba baadhi ya wadau wamekuwa wakiripoti changamoto ya wanafunzi kukaa chini kutokana na uhaba wa viti kwenye baadhi ya Shule Dar es salaam. Katika baadhi ya shule, iliripotiwa kuwa wanafunzi wanalazimika kwenda na mifuko kwa ajili ya kukalia kama mbadala wa madawati.
 
hivi zile milion 5 tano za magoli zisingeweza nunua madawati kwel na kutatua tatizo la kukaa chin?
 
wamenunua magoli mpaka hela zimeisha watoto wa walalahoi wanakaa chini wakwao wamejazana huko feza na nje ya nchi, na hela hawana sasa wanauza akiba ya dhahabu ya nchi.
 
Back
Top Bottom