Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Binafsi nianze kwa kumpongeza mama Spora Liana ambaye ndiye Mkurugenzi mpya wa jiji la Arusha. Pongezi hizi kimsingi zinafuatana na taarifa aliyoitoa mama huyu jana kwa vyombo vya habari hususan kupanda kwa mapato ya jiji kwa tarkiban mwezi mmoja tu toka aingie jijini Arusha.
Kwa maelezo yake alipokutana na vyombo vya habari jana Spora alisema pamoja na changamoto anazokumbana nazo mapato ya jiji yapanda kutoka Shilingi milioni 450 hadi mia 700. Ambapo wanatamia kununua magari kwa ajili ya kutengeza barabara, magari ya taka na vile vile kuchimba shimo kubwa kwa ajili ya taka na mambo mengine kadha wa kadha. Pamoja na hayo, Changamoto kubwa aliyokutana nayo Spora ni swala mgongano wa kimaslahi kati ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ndg Magesa Mulongo na baadhi ya wafanyabiashara ambao Magesa anawakingia kifua.
Spora Liana amesimamia kuhakikisha mabango yote ambayo hajalipiwa na ambayo mapato yake hayajulikani yanapokwenda basi yang'olewe jambo ambalo lilionekana kumkera RC na kuamua kuingilia kati kwamba kuna mtu anatakiwa aachwe. Hili lilimfanya mama huyu asimame kidete jambo ambalo lilipelekea mama huyu kumwomba Hoseah Mkurugenzi wa TAKUKURU ampe vijana ili amfunze Mulongo adabu lakini kabla ya hatua hiyo RSO aliingilia kati na kumwomba mama huyu amsamehe huyu bwana.
Akizungumza na waandishi jana Spora alisema nanukuu " kuna wakubwa wanasema nitumie busara katika swala la mabango nami nawaambia busara iliyo ni sheria zinazolinda Nchi na hasa jiji hili. Sina busara zaidi ya hiyo manake kama nikienda kinyume na sheria hizo hapo ndipo nitakapoonekana kuwa sina busara sasa kama wakubwa hawa wanadhani wana busara zaidi yangu ama hizo sheria basi waendelee kuniingilia katika shughuli zangu. Bodi na kamati zote ziko kisheria hivyo hatuna njia za mkato na kamwe mimi sijazoea njia za mkato." mwisho wa kunukuu.
Katika hali ya kushangaza wakati Mkurugenzi akiendelea na kikao na waandishi wa habari waliingia askari Polisi waliovamilia nguo za kiraia na kuanza kupiga picha wakijifanya ni waandishi wa habari lakini baadae ilijulikana kuwa walitumwa na mkubwa mmoja hata hivyo sababu ya kutumwa haikujulikana mpaka muda huu.
Mama Spora Liana anafahamika vyema kimsimamo na hasa katika swala la kukusanya mapato na hajali mtu yeyote pale anapoamini kuwa anasimamia haki. Na hili sakata la RC ni mwanzo kuna mengi yanakuja.
Kudos Spora Liana endelea kuipa Arusha heshima.