RC Arusha amvaa Mbowe, CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RC Arusha amvaa Mbowe, CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Noti mpya tz, Nov 12, 2011.

 1. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naomba niwashirikishe jf habari hii ya mkuu wa mkoa wa arusha ambayo imeandikwa na Mwananchi leo.  Friday, 11 November 2011 21:26 0digg

  [​IMG]Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mboye

  Peter Saramba, Arusha
  MKUU wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo jana alitumia kikao chake na viongozi, watendaji na wawakilishi wa makundi mbalimbali katika Manispaa ya Arusha kujibu mapigo ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe huku akiahidi kupambana nao iwapo wataendelea kuvuruga amani na usalama mkoani mwake.

  Mulongo alikejeli falsafa ya ‘nguvu ya umma’ na maandamano inayotumiwa na Chadema kiasi cha kuchafua hali ya hewa ya kikao hicho baada ya madiwani na viongozi wa Serikali za Mitaa waliopata nyadhifa zao kupitia udhamini wa chama hicho cha upinzani kususia na kutoka nje.Viongozi hao walisema wasingeweza kuendelea kumsikiliza mkuu huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani hapa.Mulongo aliitisha kikao hicho kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi ili kujadili na kupeana mikakati ya maendeleo kwa viongozi na watendaji wa Manispaa ya Arusha.

  “Kuna mtu (Mbowe), juzi alikuja hapa na kuhoji hivi Mkuu wa Mkoa (Arusha) ni nani hadi atishe watu? Sasa leo nimewaiteni hapa kuwaambia mkuu wa mkoa ndiye mimi. Sikupendezwa sana na maneno hayo, lakini sitaki kuingilia mambo hayo kwani wazee wetu walitufundisha kuwa ukioga ziwani, akaja kichaa akachukua nguo zako nawe ukichomoka kumfukuza, utaonekana kichaa ni wewe,” alisema Mulongo.
  Alihoji pia uwezo na ujasiri wa Mwenyekiti huyo wa Chadema kutoa masharti kwa Serikali kuhusu mkutano wao wa hadhara uliofanyika Jumatatu iliyopita.

  Mbowe alikuwa ameonya kuwa angeendesha maandamano
  ya siku saba mfululizo na kuvuruga ziara ya Mtoto wa Malkia wa Uingereza, Prince Charles aliyetembelea Arusha karibuni.
  “Hivi anatoa wapi uwezo na ujasiri wa kuitisha Serikali na kuipa masharti? Narudia tena leo, tena mbele ya hadhara tofauti na juzi nilipozungumza na waandishi wa habari pekee kwamba, nikiwa mhimili wa ulinzi, amani na usalama mkoa, sitakubali kushuhudia mtu anavuruga amani tena Arusha. Kibaya zaidi wengi wao wanatoka nje ya mkoa wetu. Imetosha ! Tumechoka.”

  Mkuu huyo wa mkoa alikejeli maandamano ya mara kwa mara ya Chadema: “Haya mambo ya maandamano sawa kwa sababu wanaruhusiwa kisheria. Lakini yakishazoeleka na kukolea, wanaweza kujikuta wanaandamana hata

  baada ya kuingia madarakani. Si wameshazoea kuandamana?”
  Alisema mgogoro wa Arusha hauwezi kutatuliwa kwa matumizi ya nguvu ya dola lakini akahoji nia halisi na uthabiti wa Chadema katika suala hilo wakati walikataa kusikiliza hata ushauri wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Alisema Pinda alikuwa amewaasa kutofikia hatua ya kuwatimua waliokuwa madiwani wao waliolalamikiwa kwa kuingia muafaka bila ridhaa ya uongozi wa taifa.“Hivi tukiamua kurejea uchaguzi wa Meya Arusha ambayo wanadai ndilo chimbuko la matatizo Arusha, watashindaje wakati tayari wamewafukuza madiwani wao watano?”

  Maneno hayo yalionekana kuwakera madiwani na viongozi wa Serikali za Mitaa kupitia Chadema ambao waliamua kususia na kutoka nje.Wakizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa kikao, viongozi hao wa Chadema walitangaza mgogoro na Mkuu huyo wa mkoa na kuapa kutoshirikiana naye kutokana na kuonyesha dharau kwao, chama na viongozi wao wa kitaifa.

  “Leo (jana) tumeitwa hapa kwa barua zinazoonyesha RC atazungumzia mikakati na mipango ya maendeleo Arusha. Lakini badala ya kujikita katika misingi hiyo anageuza kikao jukwaa la kuishambulia Chadema na viongozi wake. Kwa mtindo na kasi hii aliyoanza nayo, Arusha itamshinda. Tunamshauri ahame kabla mambo hayajamharibikia,” alisema Mwenyekiti wa Mtaa wa Kambi ya Fisi, Hillary Monyi.

  Wakati viongozi hao wa Chadema wakitoka nje ya ukumbi, Mulongo alilazimika kunyamaza kidogo na kuendelea: “Hata siku Rais anazindua Bunge kule Dodoma hawa wenzetu walitoka nje, lakini waliporudi hawakutueleza. Naamini nao (waliokuwa wakitoka nje) watarudi.”

  Katika kikao chake na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kujisalimisha polisi Jumatano iliyopita, Mbowe alihoji kitendo cha Mulongo kutumia vyombo vya dola kuwatishia viongozi, wanachama na wafuasia wa Chadema.

  Alilalamika akisema hana mkuu huyo wa mkoa mamlaka ya kuwatisha waliochaguliwa kwa kura nyingi za umma wakati yeye (RC) ameteuliwa na mtu mmoja (Rais).
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  "Kuna mtu (Mbowe), juzi alikuja hapa na kuhoji hivi Mkuu wa Mkoa (Arusha) ni nani hadi atishe watu?

  Nimeipenda hiyo.
   
 3. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Napitia kidogo hizo red na naomba msaada kwenu, Magessa kwani kwao ni arusha? hata kama wengi wao wanatoka nje ya arusha so waache haki ikisiginwa arusha bila kuingilia?
  Naomba kujua wasifu wa huyu mtu na ninaona kabisa hapa kuwa kwa style hii amani haiwezi kupatikana ktk nchi hii.
  Narudia tena who is Magessa?
   
 4. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo Rc hana ubavu wa kutisha makamanda, kwanza kaharibu kule Bagamoyo na akaletwa hapo Arusha, sasa naona hata hapo patamshinda nadhani wamtafutie mkoa mwingine
   
 5. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kazi imeshamshinda kabla hata ya kuanza
   
 6. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi mkuu wa Mkoa (Arusha) ni nani hadi atishe watu? Faizafox najua ulioegemea ila nasikitika sijui maslahi yako kwa wanaosigina haki ya raia, siku moja utangaze maslahi yako toka kwao
   
 7. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du! hapa sister bado sijakusoma "What you mean?"
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kwani hoja au nia ya chadema ni kuchukua umeya wa arusha au haki,kanuni na sheria zifatwe kwenye uchaguzi huo...hivi maana ya uchaguzi ni nini, inamaana diwani wa chadema hawezi kumpigia kura meya kupitia ccm...chadema ina wabunge wasio zidi 50 wakati ccm ina wabunge mara 6 kwanini tulifanya uchaguzi kama hoja ni wingi..
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,004
  Trophy Points: 280
  Huyu si ndo yule alikuwa mkuu wa wilaya bagamoyo?Katumwa huyu si bure.

  Akijenga chuki na wana Arusha atajutia mwenyewe.

  Eti wengine wametoka nje ya mkoa,yeye ametoka ndani ya mkoa gani?

  Lets wait n c
   
 10. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu kama alishindwa Wilaya halafu wakampandisha cheo kuwa mkuu wa mkoa kuna logic yoyote hapo? na kwa nini wampeleke mkoa mwingine na wasimfukuze kazi? au ndo Ushikajicracy?
   
 11. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umesema kweli mkuu na mfano mzuri ni Halmashauri ya Wilaya ya Hai..
   
 12. only83

  only83 JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umeipenda eeh!! ila Mbowe kaoa ndio tatizo...nadhani ile mission yako imefeli pole!! Jaribu kwa ****** wa kaya.....
   
 13. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  RC is 100% right.

  CHAPA KAZI KIONGOZI, HAKUNA WA KUKUTISHA. UNAYO SUPPORT YA WANA-ARUSHA.

  Wakati mefika kusafisha mambo ya kihuni Arusha. Enough is enough.
   
 14. k

  kiloni JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hili ZZUZU!! rc LIMETUMWA NGOJA TUONE!
   
 15. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu

  Hii kauri imenitisha yaani tunafikia tunaanza kubaguana kuwa huyu anatoka mkoa fulani????????????? Kikwete aingilie hii kauri kwa maslai ya nchi, huyu jamaa anatakiwa kuondolewa haraka iwezekanavyo, anapandikiza ukabila?
   
 16. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama unasifia lugha aliyotumia basi hujui historia ya nchi hii, na hujui kuwa wengine tunajivunia utanzania wetu ambao kokote nikienda ni mtanzania na nina haki zote.
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Umeipenda eeh!! ila Mbowe kaoa ndio tatizo...nadhani ile mission yako imefeli pole!! Jaribu kwa ****** wa kaya.....
   
 18. N

  N series Senior Member

  #18
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  magesa na huyo shosti wake alomtuma,wote viburudisho vya cameron,vilaza tu hao wanaotumia masaburi kufikiri . . . . . !.
   
 19. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Anaonekana kujinadi kama mtu wa Arusha..na pia anaonekana kama mkabila Vile...kwani wengine hawastashili kuwepo Arusha?? Je Dar ni watu gani wanastahili.....Masaburi Thinker
   
 20. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  huyu bibi Magessa, atapata wakati mgumu sana Archuga!
   
Loading...