Nimekusoma mwanzo hadi mwisho na uliyoongea yote ni kweli tupu! Kukujibu swali lako, plain clear TUNAPOTEA!!!
Awali nilishindwa kumaliza maneno kv nilidhani sababu zilizopelekea uamumuzi huo ni kwamba hivi sasa bandarini kuna nafasi ya kutosha (though in free market sio justifiable argument but can be tolerated) lakini ukisoma barua ya SUMATRA, sababu sio hiyo! Kosa la kwanza hapa una-jeopardize investors confidence... watu hawatakuwa na uhakika kwa investments wanazofanya kv hawajui kesho serikali na taasisi zake watachukua uamuzi gani! Suala la ICDs lililetwa na serikali yenyewe ili kupunguza msongamano wa mizigo bandarini! Investors wakanunua mitaa Kurasini na kujenga ICDs... wakachukua mikopo n.k... from nowhere, unasema from hakuna mizigo kwenda ICDs!!!! Si tu kwamba hawajali fixed investments ambazo zimeshafanywa lakini inaonekana hawajali hata benefits zinazotokana na hizo ICDs... madereva, matingo, wabeba mizigo, Mama Lishe pamoja na wafanyakazi wa ICDs husika wataathirika na uamuzi huo!
Madai wanayotoa watu kwamba ICDs zinatumika kutorosha makontena ni madai ya kijinga na yasio na maana yoyote kwa kuwa hakuna meli yenye uwezo wa kupita chini kwa chini bila kuonekana na kuibukia ICD... zote lazima zipite bandarini!! Sasa kwanini watu watoroshe makontena wakati meli zinapitia hapo hapo!!
Halafu hapo unaota kujenga viwanda kwa kutumia wawekezaji binafsi! Nani atakuwa tayari kuwekeza kwenye versatile business environment!