Komeo
JF-Expert Member
- May 3, 2011
- 2,498
- 1,172
Mkuu tunashukuru kwa ufafanuzi ambao wapiga dili hawapendi watu wengine tujue. Wenyewe juzi walituambia meli zimekimbia bandari ya Dar kwa kodi wanazotozwa mawakala a.k.a. madalali wa kitanzania. Kwa maana nyingine walizifukuza meli wenyewe kwa kupiga debe bovu huko anga za Kimataifa wakifikiri wanaikomoa Serikali bila kujua kwamba wao ndio watakuwa waathirika wa kwanza. Na wakati huo huo bado wanataka mafuriko ya makontena kwenye ICD wanazopigia dili. Jamani you can't eat the cake and have it.Mkuu kuwa mkweli,
kwenye mkataba wa TPA na ICD kuna kipengele ki nasema kuwa, mizigo itapelekwa IDC ikiwa tu eneo la kuhifadhia mizigo hiyo au Containers ndani ya Bandari litakuwa limejaa.
Sasa ICD nyingi zikawa zina mtandao wao hapo bandarini ambapo mizigo ikifika tu hata kama ndani ya Bandari bado kuna nafasi ya kuhifadhi mizigo ilikuwa inapelekwa ICD hivyo kuikosesha TPA mapato yake na wakati mwingine ICD zilikuwa zinawacheleweshea wateja wao mizigo yao kwa makusudi ili waweze kupata mapato.
kwa hatua hii, naishukuru sana serikali kwa hatua hii.