Rasimu ya Katiba inayopendekezwa 2014

TUME HURU YA UCHAGUZI
(a) Tume Huru ya Uchaguzi
Kuundwa kwa
Tume Huru ya
Uchaguzi
211.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya
Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya
kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa
kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.

Hivi kuandika tume huru ya uchaguzi inatosha kuwa huru? Nani anaichagua hiyo tume huru? Inawajibika kwa nani?

Hapa hamna kitu, mvinyo ule ule, bilauri tofauti!
 
Napata wasiwasi juu ya upigaji wa kura wa katiba fake kwani waliopo huko almost wote ni maccm. Kutakuwa na uhakiki gani mbali na maccm wakati wa kuhesabu kura ili ionekane kuwa hakukuwa na upikaji wa matokeo? All in all hata wakiipitisha tuoneshe mshikamano kuwaondoa mwakani ili tutengeneze katiba ya wananchi.
 
Tofauti kubwa ambayo ike kwenye mchakato huu ni kuwa umeanzishwa na watawala sio wananchi. Sisi wananchi tumeshirikishwa tu. Ila aminibusiamini kwa vyovyote vile bado content za katiba si ajabu zingekuwa hizihizi tunazozizpmea hsra kama mchakato unaenda tulivyotaka kwani kuna hoja ya wengi against wachache hata katika public. Usipoheshimu maonibya wengi una lako jambo tena binafsi na wewe si mwana demokrasia.
 
Napata wasiwasi juu ya upigaji wa kura wa katiba fake kwani waliopo huko almost wote ni maccm. Kutakuwa na uhakiki gani mbali na maccm wakati wa kuhesabu kura ili ionekane kuwa hakukuwa na upikaji wa matokeo? All in all hata wakiipitisha tuoneshe mshikamano kuwaondoa mwakani ili tutengeneze katiba ya wananchi.

Kila mbunge ataulizwa kipengele kwa kipengele... upo hapo
 
Loooo!! Kumbe ni jina tu ''itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi” ni yale yale tu
TUME HURU YA UCHAGUZI
(a) Tume Huru ya Uchaguzi
Kuundwa kwa
Tume Huru ya
Uchaguzi
211.-(1) Kutakuwa na Tume Huru ya U chaguzi ya Jamhuri ya
Muungano itakayoitwa “Tume Huru ya Uchaguzi”.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine saba watakaoteuliwa na Rais baada ya
kupendekezwa na Kamati ya Uteuzi.

(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume Huru ya
Uchaguzi watashika madaraka mara baada ya kuapishwa na Rais.
(4) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Uchaguzi utafanywa kwa misingi kwamba, endapo Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa
kutoka upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
nani aliwaambia ukawa watoke bungeni? pumbavu zao

Hawakutaka historia ije kuwahukumu kwa kupitisha sera za magamba na kuuita katiba. Yaami fisadi Chenge ndie mtu msafi mlie ona anafaa kutunga katiba ya Tanzania?? Hii ni aibu kwa Ccm na wale wote walioko Dodoma
 
Wewe ungejibu swali la Kwenju badala ya kuzunguka.Sasa ya nini kuiita Tanganyika ya wakoloni wakati unajua kabisa mpaka tuwe na serikali moja ndio ife?.Sometyms mnakera sana kwa kujivua ufahamu na kuwa vibaraka wa watawala watu kama nyie ambao walau mmebahatika kupata elimu ya juu.Shame on you!!!
Kuwa mpole. Mimi kijijini kwetu hakuna anayehangaishwa na jina. Wananchi wanapata shida sana kwa sababu hawana matibabu, elimu kwa watoto, maabara, pembejeo na huduma nyingine za kijamii. Kuna watu wanakufa kwa njaa au kwa kukosa matibabu, lakini sijawahi kuona wala kusikia wakifa kwa kukosa neno 'Tanganyika'. Hangaikia mambo ya kukupa manufaa badala ya kuhangaikia majina. Majina hayana tija, ndiyo maana hata wanangu hakuna mwenye jina la 'kizungu' wala 'kiarabu'. Tanzania ni jina lililobuniwa na Watanzania huru wenye akili na utashi huru ndani ya nchi yao mpya iliyo huru.
 
mhh jamani watoto wangu baada ya hii sijui watakua wapi? Hivi hawa walioleta hii rasimu wana watoto kweli? Nina wasiwasi na uzazi wao. Ehee Mungu naomba uingilie kati tutakwisha na dhambi
 
Kuwa mpole. Mimi kijijini kwetu hakuna anayehangaishwa na jina. Wananchi wanapata shida sana kwa sababu hawana matibabu, elimu kwa watoto, maabara, pembejeo na huduma nyingine za kijamii. Kuna watu wanakufa kwa njaa au kwa kukosa matibabu, lakini sijawahi kuona wala kusikia wakifa kwa kukosa neno 'Tanganyika'. Hangaikia mambo ya kukupa manufaa badala ya kuhangaikia majina. Majina hayana tija, ndiyo maana hata wanangu hakuna mwenye jina la 'kizungu' wala 'kiarabu'. Tanzania ni jina lililobuniwa na Watanzania huru wenye akili na utashi huru ndani ya nchi yao mpya iliyo huru.

Hivi ni kwa nini mnakana identity yenu kama Watanganyika? kuna aibu ani kuitwa mtanganyika? Hakuna Tanzania bila zanzibar na Tanganyika.

Zanzibar wako proud kujiita na kutambuliwa kama wazanzibar....inakuwaje nyie watanganyika mnaonea aibu taifa lenu?

Hakuna kitu kinaitwa Tanzania bara...hakuna nchi kama hiyo...kuna Tanganyika
 
Akili zako za ki CCCM (Genge la wezi) ndo maana unadhani Zanzibar ikiondoka hakuna maisha! Pole we

sidhani kama umenielewa
mi nilukuwa namjbu aliyesema kuwa tanganyika ni,jina tuliopewa na wakoloni
cjui kama umenielewa sasa???????
 
94.-(1) Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani
endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa
masharti ya Ibara hii.
(2) Bila kuathiri masharti mengineyo ya Ibara hii, hoja yoyote ya
kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama itadaiwa kwamba Rais ametenda
mojawapo ya makosa yafuatayo:
(a) ukiukwaji mkubwa wa masharti ya Katiba hii;
(b) makosa makubwa ya jinai;
(c) kuzuia kwa namna yoyote ile yeye kuchunguzwa kwa mujibu wa
Ibara hii;
(d) rushwa;
(e) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha nafasi ya madaraka ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano;
33
(f) kupuuza au kukataa kutekeleza uamuzi au amri halali ya Mahakama;
au
(g) amefanya kitendo ambacho kinakiuka kanuni za maadili au miiko ya
uongozi.
(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama-
(a) hoja ya namna hiyo itatolewa baada ya miezi kumi na mbili tangu
hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge; na
(b) taarifa ya maandishi, iliyotiwa saini na kuungwa mkono na
Wabunge wasiopungua asilimia ishirini na tano ya Wabunge wote
itawasilishwa kwa Spika siku kumi na nne kabla ya kikao ambapo
hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni.
(4) Taarifa itakayowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (3)(b)
itafafanua makosa aliyoyatenda Rais, na itapendekeza kuwa Kamati Maalum ya
Uchunguzi iundwe ili ichunguze tuhuma zilizotolewa dhidi ya Rais.
(5) Wakati wowote baada ya kupokea taarifa iliyotiwa saini na Wabunge
na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuwasilisha hoja
yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha mbele ya Bunge na
kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja
ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(6) Endapo hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi itaungwa
mkono na Wabunge wasiopungua asilimia sabini na tano ya Wabunge wote,
Spika atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.
(7) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya Ibara hii, itakuwa
na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa Mwenyekiti
wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti; na
(c) Wabunge watano kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano,
watakaoteuliwa na Spika kwa kuzingatia uwakilishi wa kila upande
wa Muungano.
(8) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchunguzi
kuundwa, itachunguza na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na
kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu utakaowekwa na kanuni
za kudumu za Bunge.
(9) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi
siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.
(10) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi,
taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na kanuni
za kudumu za Bunge.
(11) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa,
Bunge litaijadili taarifa hiyo na kutoa fursa kwa Rais kujieleza, na kisha, kwa
kura za Wabunge wasiopungua asilimia sabini na tano ya Wabunge wote, Bunge
litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais ama yamethibitika au
hayakuthibitika.
(12) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais
yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika madaraka ya Rais, Spika
34
atamfahamisha Rais juu ya Azimio la Bunge na Rais atakuwa ameondolewa
madarakani na Makamu wa Rais ataapishwa mara moja kushika madaraka ya
Rais.
(13) Endapo Rais ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na
mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya:
(a) kushika nafasi yoyote ya madaraka nchini; na
(b) kupata malipo yoyote ya uzeeni, posho wala kupata haki au nafuu
nyingine anazopewa Rais au mtu aliyekuwa Rais kwa mujibu wa
Katiba au sheria.
 
Ndugu wana jf... Kilichosomwa bungeni tayari kwa kujadiliwa na bunge kabla ya kupigiwa kura hiki hapa....

hata hamu ya kuifungua kuona kilichomo sina, endeleeni nayo wenye moyo, mimi nasubilia kura ya maoni tu.
 
Kuwa mpole. Mimi kijijini kwetu hakuna anayehangaishwa na jina. Wananchi wanapata shida sana kwa sababu hawana matibabu, elimu kwa watoto, maabara, pembejeo na huduma nyingine za kijamii. Kuna watu wanakufa kwa njaa au kwa kukosa matibabu, lakini sijawahi kuona wala kusikia wakifa kwa kukosa neno 'Tanganyika'. Hangaikia mambo ya kukupa manufaa badala ya kuhangaikia majina. Majina hayana tija, ndiyo maana hata wanangu hakuna mwenye jina la 'kizungu' wala 'kiarabu'. Tanzania ni jina lililobuniwa na Watanzania huru wenye akili na utashi huru ndani ya nchi yao mpya iliyo huru.

hoja za mbunge alli kesi zinajibu hoja zako.

lakini we kama msomi ungesema unataka srkli ngapi??
kwa sababu huo umaskini wa wazazi umeletwa na mfumo mbovu wa muungano

ila kwa kywa ww pia ni,,,
 
hoja za mbunge alli kesi zinajibu hoja zako.

lakini we kama msomi ungesema unataka srkli ngapi??
kwa sababu huo umaskini wa wazazi umeletwa na mfumo mbovu wa muungano

ila kwa kywa ww pia ni,,,

Pengine sijui nimeingia kwenye mjadala na mtu mwenye uelewa kiasi gani. Muungano unasababisha umasikini? Burundi ni masikini-wao ni muungano wa nchi ngapi? Malawi ni malofa kupindukia-Malawi ni muungano wa jamhuri zipi? Basi, niishie hapo.
 
Back
Top Bottom