Spika wa Bunge Tulia Akson asema Ripoti ya CAG haijafika Bungeni Bado

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,224
6,468
Asema Ripoti ya CAG haikufika Bungeni na watu wawe watulivu. Amedai baada ya Ripoti kusomwa taarifa huwa inaletwa Bungeni na kujadiliwa na maazimio ya Ripoti kutolewa na Bunge.

Ameendelea kusema mambo ya serikali hayaendi kinyemela ila ni kwa sheria na kanuni. Hivyo Ripoti ya CAG ipo jikoni na inakuja Rasmi ndani ya Bunge hilihili na Mkutano huuhuu wa 11 na wabunge watajadili. Baada ya hapo Bunge Kama Mhimili litatoa maamuzi.

Kadai hakuna mtu wa kuilinda serikali, mambo yatakuwa wazi na kila Mbunge atasema apendacho na atakacho Ripoti hiyo ikishakuwa wazi kwa Umma. Kilichosomwa na CAG ni Muhtsari wa Ripoti na Kuna mambo Mengi bado hatuyajui. Ripoti ya CAG huwa ni kubwa Sana na ikija Bungeni ina maana kila kitu kipo wazi, itasomwa na kujadiliwa na maazimio kuwekwa na Bunge.

NB: Ule muda wa kuisoma kwa Rais kupitia CAG huwa ni Muhtsari au summary. Kuna Mengi ndani tusiyoyajua. Muda utafika!!
 
Back
Top Bottom