Hivi, ukiiweka rasimu hii ya katiba, pembeni ya rasimu ya pili ya tume kuna tofauti zipi ambazo zimejitokeza ukiacha kuundwa kwa shirikisho la serikali 3. nadhani haya ndio ya kujadili zaidi kwa nini wananchi hasiikubali rasimu hii badala ya kutumika kisiasa. Tuyasome mapendekezo yao na tuyachambue wapi wananchi hawaridhiki badala ya kuendelea kulilia rasimu ya Warioba ambayo ingepitia mtihani huu vile vile.
Kilichoandikwa na Chenge ni maoni ya rasimu yao ya mafichoni.
Kuyajdili ni kutoa uhalali usiohitajika.
Tume ya Warioba usioikubali, mapendekezo yake yamepigwa chini.
Haya unayoyaona ni ya tume ya Samwel Sitta na Shibuda waliojiteua na kuanza kuongea na wafugaji na wakulima tu.
Tena wanatumia takwimu za wakulima 17 na wafugaji 23.
Wewe Mkandara ulihoji takwimu za Warioba kama si sahihi, hebu tueleze takwimu za watu 40 zina usahihi gani.
Mkuu, katiba ni nyaraka nyeti si daftari la shule kama unavyodhani.
Hakuna maoni ya wananchi, hakuna kujadili
Mkandara exposure inakusaidiaje mkuu.
Hata wewe unaamini mtovu na muovu kama Cheng anaweza kuandika kitu cha maana ukajadili kweli.
Kwamba hukuona usanii wa kupiga kura kwa internet via yahoo na fax bila msimamizi.
Huoni vituko vyote hivyo unataka watu wajadili upuuzi.
Mkuu, kwani hukuona jinsi vifungi 1 na 6 vilivyoepukwa. Hivi unawezaje kujadili jengo bila msingi.
CCM wenyewe awanasema vifungi hivyo ni moyo wa katiba, wewe unavikwepa kwasababu tu unataka kulinda masilahi ya S2 kwa faida za wazanzibar.
Unasikitisha sana, najiuliza huko vijijini sijui ni aje kama mtu mwenye fursa kama wewe hawezi kuona umbali zaidi ya pua yako