Hii tena ni Yanga, mechi ilikuwa kati ya Yanga na Cadet Club ya Mauritius katika kombe lililokuwa linaitwa 'Africa Cup of Winner Cup', mwaka sikumbuki. Yanga tulishinda 3-1, magoli yaliyofungwa na Mohammed Hussein (goli 1,3) na James Tungaraza (goli la 2). Unaweza kuamini nimekumbana na tiketi ya mechi hii katika takataka zangu?
Waliosimama kutoka kushoto ni:
Team Manager Nurdin Ally, Mahmoud Nyalusi, Keneth Mkapa, Reuben Mgaza, Sylvatus Ibrahim, Ismail Issa, Mathias Mulumba, Vincent Peter, Sadiq Kalokola, Kocha Mkuu Mkongo Tambwe Leya (kwa wasiomfahamu inabidi mtafute historia yake na soka la Tanzania), na kocha msaidizi Mrundi Nzoyisaba Tauzany.
Waliochuchumaa kutoka kushoto ni:
Maalim Saleh, James Tungaraza, Ally Yusuph Tigana', Anwar Awath, Mzee Abdallah, Mohammed Hussein na Bakari Malima.