Rangi wanazopaka wanajeshi mwilini wakiwa vitani huwa zinaashiria nini?

ashidodi

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
291
339
Habari za Leo wadau wa humu ndani.

Niende Moja Kwa Moja kwenye swali, mwenye uelewa anieleweshe.

Rangi wanazopaka wanajeshi usoni wakiwa wanaelekea kwenye oparesheni za kivita huwa zinaashiria nini, au zinamaana gani?.

00a8ea316590de9aa387d6b489cfc3cd.png

Nawasilisha
 
Mbwembe, Kama Unazozifanya wewe kazini kwako.
Ukisikia "kazini kwangu Kuna kazi"
Jeshi Ni kazi Kama kazi Zingine, Bila maokoto unazani Kuna mtu angeshobokea Dundo....Maslai Baba.... Watu Wote Duniani wanaitaji ngawila.... Ndugu
 
Kuna kitu kinaitwa "Camouflage" ...Ni mbinu ya kijeshi inazotumika kuficha taswira ya binadamu ili asiweze kutambulika kirahisi. Rangi wanazopaka wanajeshi mwilini zinaendana na mavazi, nyenzo na mizigo aliyobeba. Huakisi asili na hali ya uwanja wa mapambano, uliotokana na tabia za wanyama kama chui na kiumbe kinyonga.
 
Hata jkt haukupita??
Hiyo ni camouflage.

Sio wanajeshi tu hadi zana za kivita kama vile vifaru na magari vinapambwa ili vifichike kiurahisi/visionekane kwa urahisi/vifanane mazingira husika
 
Unadhani adui akikukamata umepaka lipstick atakufanyaje mkuu?Sasa Ili kukwepa kupakatwa na adui huwa wanapaka rangi za kutisha,wengine tope zito na Kuna jeshi zaman huko naskia walikuwa wanapaka kimba,adui kuwasogelea tu waliona jau.
 
Kuna kitu kinaitwa "Camouflage" ...Ni mbinu ya kijeshi inazotumika kuficha taswira ya binadamu ili asiweze kutambulika kirahisi. Rangi wanazopaka wanajeshi mwilini zinaendana na mavazi, nyenzo na mizigo aliyobeba. Huakisi asili na hali ya uwanja wa mapambano, uliotokana na tabia za wanyama kama chui na kiumbe kinyonga.
Asante sana angalau nimeng'amua kitu, Kuna mijitu humu haijui hata thamani ya hili jukwaa inaropoka tu
 
Habari za Leo wadau wa humu ndani.

Niende Moja Kwa Moja kwenye swali, mwenye uelewa anieleweshe.

Rangi wanazopaka wanajeshi usoni wakiwa wanaelekea kwenye oparesheni za kivita huwa zinaashiria nini, au zinamaana gani?.

View attachment 2985973

Nawasilisha
Hizo ni camoufladge paint. Zimekuwa desinged ku minimize mngao na kumficha askari afanane na mazingira yanayo mzunguka haswa vichaka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom