kwanza niseme tu asante sana super man, na nimekugongea haki yako kama kawaida. pia shukrani kwa wadau wote walioonesha concern, pamoja na kuwa wengine hawakunielewa vizuri. Mm siyo fisadi na wala sifanyi kazi serikalini, ni mjasiriamali mdogo sana tu. ila niliposema RR nilimaanisha 4.6 HSE, wala siyo VOGUE (sijawa na mil80 ya kununua gari!). Kutokana na kazi zangu naenda sana shamba, pia naenda sana crossborder, hivyo nahitaji gari ambayo ina pull kubwa, confotable pia tofauti kidogo ofcz!. Pamoja na majibu mazuri ya wakuu, bado nimebaki njiapanda, sijapata sgstions kwamba unaonaje khs gari hii, au hii. Toyota sawa, lakini toyota gani? nataka kitu tofauti kidogo wazee, hata kama ni toyota. Najua hapa hapa kuna watu watasababisha nifikie uamuzi wa busara na kupata gari nzuri tu. Pia kuna mdau alinidokeza kuhusu Jeep Grand Cherokee, mwingine akasema Toyota JL lakini nikaona bei za JL hazishikiki. Heshima mbele kama kawaida wazee
Naipenda tanzania ndy maana bado nipo bongo, kilimo kwanza.