Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

nimeuliza swali moja tu ambalo nilihitaji ufafanuzi simple coz hamna mtu anayejua kila kitu, and unaongelea vitu ambavyo hata havihusiani duh...

Napost kila napokuwa na mda ,coz yapo mengi ya kuwajuza watu....

Kumbe wanifuatilia,sasa si tayari nishapata umaarufu au...
Anyway bro mimi huwa siyo mtu wa hivyo am doing out of passion,kama umekwazika aya.
Mimi huwa namjibu mtu kulingana na namna alivyouliza...kwani wangapi huko juu wameuliza maswali kwa lengo la kutaka kujua na nimewajibu tu vizuri? Mtu anayeuliza kwa lengo la kutaka kujua anauliza namna hiyo? We umekuja kwa lengo la kubishana, kwamba uonekane we ni mjuzi zaidi kuliko wengine. Endelea tu na nyuzi zako bro, mimi nipo hapa kibiashara sijaja kubishana na watu, atakayeuliza kistaarabu nitamjibu kistaarabu pia (mimi ni mtu mmoja peace sana, sipendagi kujibizana na watu kwa sababu ambazo hazina msingi)
 
Usikimbie mkuu,,j
Tafadhali ibu kwa namna gani ratio ya mortar kuwa kali kuliko ya plasta,inasababisha hiyo michirizi....?
 
Kama una ramani yako na unahitaji kufanyiwa makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane, makadirio yatakuongoza katika ununuzi ya vifaa vya ujenzi na kukuepusha kubakiwa na material mengi ambapo utalazimika kuuza kwa bei ya hasara hata kama hujayatumia
 
Wakati unasuka nondo kwa ajili ya mkanda wa juu, funga matoleo ya nondo sehemu za madirisha ili hata baadae ukitaka kuweka kofia za zege usipate shida tena kutindua tindua
 
Wakati unasuka nondo kwa ajili ya mkanda wa juu, funga matoleo ya nondo sehemu za madirisha ili hata baadae ukitaka kuweka kofia za zege usipate shida tena kutindua tindua
nyumba nzuri inatakiwa iwe na kozi ngap mkanda wa chini mpaka lenta na kozi za juu?
 
nyumba nzuri inatakiwa iwe na kozi ngap mkanda wa chini mpaka lenta na kozi za juu?
Kozi 10 kati ya mkanda na mkanda, kozi 3 juu ya mkanda wa juu. Kama utapendelea madirisha marefu, weka kozi 11 au 12 kati ya mkanda na mkanda
 
Kabla ya kupigilia mbao za dari, hakikisha fundi wako anatumia pipe level kuweka reference points ili dari lako liwe limekaa sawa (limenyooka kimlalo). Mafundi wengi wanachukulia usawa wa tofali la mwisho kama reference line kitu ambacho kama ukuta haujanyooka, dari lazima liiname. Kabla fundi hajaanza kazi, muulize pipe level yako iko wapi, na uhakikishe anaitumia sio awe nayo tu kwenye begi

Ramani, Makadirio, Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Katika upigiliaji wa mbao za dari, ikitokea kwamba chumba chako ni mstatili (mfano 3mx4m n.k), basi upande ambao ni mfupi ndio unatakiwa upigilie mbao ndefu (mbao nzima) na upande mrefu ndio unatakiwa upigilie mbao za vipande.

Yaani mbao ndefu ambazo hazikatwi zinatakiwa ziwe parallel na upande ambao ni mfupi au perpendicular na upande ambao ni mrefu, na mbao za vipande zinatakiwa ziwe parallel na upande ambao ni mrefu au perpendicular na upande ambao ni mfupi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ufungaji wa bomba za umeme, ni bora ukatumia spring bender kukunja bomba kuliko kutumia elbows..Elbows zina tabia sana ya kuchomoka chomoka maana nyingi unakuta hazina nyuzi 90, hivyo kama utatumia elbows utalazimika kutumia tangit katika maungio.

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
 
Gharama ya vifaa kuwa kubwa katika hatua ya uwekaji wa umeme katika nyumba inachangiwa kwa kiasi kikubwa na design ya michoro itakayochorwa na fundi umeme. Kuna namna nzuri ya kudesign michoro ambayo itakufanya usitumie bomba wala nyaya nyingi hivyo ukajikuta unaokoa gharama nyingi ambazo hazikuwa na ulazima wowote
 
Baada ya kuskim ukuta wako, paka binder kabla ya kuanza kupaka rangi. Inasaidia sana kuua vumbi la gympsum powder na kufanya rangi ishike vizuri ukutani

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane +255(0)624068809
 
Kabla ya kuanza kupiga plaster katika kuta, hakikisha fundi wako anaweka timanzi katika kuta ili kuhakikisha plaster yako inanyooka vizuri hata kama ukuta ulikuwa umepinda mahali. Ni vizuri timanzi akaziweka siku moja kabla ili zipate muda wa kutosha kukauka

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
 
Mpangilio mzuri wa vipimo katika ramani utafanya jengo lako lifanane na ramani exactly baada ya jengo kukamilika. Lazima mchoraji aweke vipimo ambavyo kiuhalisia vinapimika kiurahisi, mfano unakuta mchoraji kwenye ramani kaweka ukuta uwe na urefu wa sentimita 40, wakati huo tofali lina urefu wa sentimita 45 (fundi hawezi akawa anachonga tofali la 45cm ili apate tofali la 40cm, ataweka tu tofali zima kama lilivyo)

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
20240412_173959.jpg
 
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane +255(0)624068809
Mkuu inawezekana nondo za mm 12 zikatumika kwenye nguzo za ghorofa 1 nyumba ya kawaida ya familia?
Maana kuna wanaosema inawezekana kuna wanaosema katu ki structural engineering haitakiwi kamwe maana nguzo za ghorofa moja ni sharti ziwe mm 16 full stop.
 
Kwa jengo la ghorofa moja, minimum diameter ya nondo kwa nguzo inayotakiwa kutumika ni milimita 16, hiyo ya milimita 12 watu wanaforce tu kupunguza gharama.

Kwenye jengo la ghorofa, nondo za milimita 12 huwa zinatumika kwenye slab na ngazi
 
Ok kuna majengo ya ghorofa 1 nimeona hawaweki jamvi yaan boma linaanzia tu baada ya mkanda wa chini as if ni nyumba isiyo ya ghorofa na wanaweka tu rough floor then tiles ingawa yana nguzo, mikanda na base kawa kawaida ya ghorofa zinavyojengwa hii kitaalam ni sahihi? je haiwezi pelekea jengo kutitia au kuanguka?
 
Hapana, uzito wa jengo huegemea kwenye vitako vya nguzo (footings) na kupelekwa moja kwa moja ardhini sio kwenye jamvi la chini (Oversite concrete). Jamvi la chini linasaidia kuongeza uimara wa floor, na uzito wake hupelekwa ardhini moja kwa moja bila kubebwa na mkanda/nguzo (asilimia chache ya uzito ndio unaweza kubebwa na beam kama nondo zitatumika)
 
Back
Top Bottom