Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Endapo ukipewa picha ya nyumba ambayo mtu ameipenda halafu wewe uichore ramani yake, si inawezekana? au ramani nzuri ni ile unayoichora wewe kutokana na specifications za mteja?
Ndio ndg inawezekana kabisa, ukija na sketch yako mimi nitaidesign lakini pia palipo na kasoro za kiufundi kwenye hiyo sketch nitakushauri namna ya kuparekebisha. Ukinipa specifications zako pia nitadesign kama unavyohitaji kwa kufuata aspects zote za designing

Hata wateja wanaokuja kwangu na ramani zao kwa lengo la kufanyiwa makadirio huwa nawashauri pia kasoro ndogo ndogo za ramani zao walizouziwa na watu wengine kabla hawajaanza ujenzi.
 
Ahsante sana mkuu kwa majibu mazuri.

Sasa umenipa uwanja mpana wa maamuzi
 
Ni bora ukatumia twin socket moja kuliko kutumia single socket mbili katika chumba. Hii itasaidia kupunguza gharama ya vifaa na ufundi pia kwa sababu jumla ya bei ya single socket mbili ni kubwa kuliko bei ya twin socket moja.

Upande wa switch pia ni bora ukatumia 2 gang au 3 gang one way switch kuoperate taa mbali mbali (mfano taa ya sebleni, taa za nje na koridoni zote zikawa ktk switch moja ya 3 gang switch) kuliko kutumia 1 gang switch zaidi ya moja, itakufanya uongeze idadi ya metal box pia achilia mbali idadi ya hizo switch
Nyumba ninayoishi nikitaka kuwasha taa za nje upande wa mbele, taa za nyuma, sebuleni na kwenye corridor zote zina socket yake na hazipo sehemu moja kitu ambacho kinaleta usumbufu sana
 
Nyumba ninayoishi nikitaka kuwasha taa za nje upande wa mbele, taa za nyuma, sebuleni na kwenye corridor zote zina socket yake na hazipo sehemu moja kitu ambacho kinaleta usumbufu sana
Huyo fundi aliyefanya wiring inawezekana alikuwa hana uzoefu wa kutosha ndio maana akatenganisha kila taa zikawa na switch yake, nadhani sasa hivi atakuwa ameimprove kama atakuwa ni mtu wa kujifunza
 
Tuma na Cv's tuone na kazi ulizowahi kufanya...
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
 
Sio earth rod zote zimetengenezwa kwa madini ya copper, kuna zingine zimetengenezwa kwa madini ya chuma halafu zikapakwa madini ya copper kwa nje...ukienda kichwa kichwa, utauziwa earth rod ya chuma kwa bei ya earth rod ya copper (utauziwa kuku kwa bei ya mbuzi)
 
Habari mkuu ninakiwanja changu kina ukubwa wa mita za mraba urefu 35 na upana ni 22 sasa nauliza kwa ukubwa huo ninao uwezo nikajenga nyumba ya vyumba viwili na sebule mbili na servant kota ya chumba sebule moja na nikapata eneo la kujenja kibanda cha wazi cha kupumzikia kwa nnje yani uwani na nikapata kuweka uzio fensi na nikapata na parking ya gari kwa ukubwa huo wa kiwanja
 
Ndio inawezekana ndg, hicho kiwanja chako ni kikubwa (ni sawa na viwanja viwili vya mita 22 kwa mita 17.5)
Kama utahitaji nikutengenezee ramani tuwasiliane ndg
 
Switch socket zinatakiwa ziwekwe angalau futi 2 (60cm) kutokea kwenye floor ili hata mtu anapokuwa anadeki floor kusiwe na uwezekano wa maji kuingia kwenye socket na kuleta shida

Na upande wa switch inatakiwa ziwekwe angalau futi 5 (150cm) kutokea kwenye floor

Ramani, Makadirio, Ushauri tuwasiliane
 
Hii imekaa vzr
 
Kwenye mkanda wa chini ni bora ukafunga nondo tatu tatu na nguzo kwenye kona za msingi kuliko kufunga nondo nne nne kwenye mkanda halafu usiweke nguzo yoyote kwenye msingi
vip nondo tatu na nondo nne ipi bora ama ubora utakua sawa kwenye mkanda
 
vip nondo tatu na nondo nne ipi bora ama ubora utakua sawa kwenye mkanda
Nondo nne ni bora zaidi, mimi nilikuwa nasema kuliko kuweka nondo nne nne kwenye mkanda huku kukiwa hamna nguzo hata moja, ni bora ukafunga nondo tatu tatu then nondo zingine utumie kuweka nguzo kwenye msingi. Ila kama mfuko unaruhusu, weka nondo nne nne na nguzo pia.
 
na je ukiweka 3 kwenye mkanda na 3 kweny lenta ili uweke izo nguzo za kona apo imekaaje
 
na je ukiweka 3 kwenye mkanda na 3 kweny lenta ili uweke izo nguzo za kona apo imekaaje
Mkanda wa juu ni vizuri ukatumia nondo nne nne mana kuna sehemu zinakuwa na uwazi (madirisha na milango) na juu yake kunakuwa tena na mzigo wa tofali (stop courses) japo wapo wanaoweka nondo tatu tatu kupunguza gharama
 
Hakikisha circuit breaker zako unazikagua mara kwa mara kujua kama bado zipo active ili kujihakikishia usalama wa nyumba yako pale kunapotokea hutilafu za umeme kama umeme mwingi, short circuit n.k

Ni sawa na kumtegemea mlinzi anayelinda getini kwako kumbe na yeye mwenyewe kalala
 
Back
Top Bottom