Ushauri kuhusu Ujenzi

commm

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,674
1,905
Wakuu habari za wakati huu.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Baada ya Kupambana na Mungu kuniwezesha kupata kiwanja. Natamani sana kwa mwaka ujao Mungu anisaidie nianze ujenzi.

Ila ningependeza nianze na vyumba viwili kwanza (chumba na sebule) ili ni niweze kuhamia kwangu kwa kuwa bado sijaoa,, huku nikiendelea kujitafuta kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ambayo itanitoshea mimi na familia yangu.

Ukubwa wa Kiwanja ni (25×40 sqm). Nawakaribisha kwa Ajili ya ushauri na maoni.

NB: Pia ningependa kujua nawezaje kupata ramani ambayo itaniwezesha kukadiria gharama za huo ujenzi
 
Kiwaanja kikubwa sana hicho, jenga nyumba kubwa acha habari za chumba na sebule. Jenga mdogo mdogo nyumba ya maana kabla haujapata familia
 
Ujenzi hua unategemea na mfuko wako!!
Kama unafikiria kujenga chumba na sebule unaweza kuvijenga pembezoni mwa kiwanja ukaacha nafasi kubwa ya kujenga nyumba ya ndoto yako hapo baadae.
Hiki chumba na sebule kitakua ni chumba cha nje kwa matumizi mengine ambayo ni mengi tu, utachagua mwenyew kwa jinsi itavokufaa.
Kwa chumba na sebule sidhani kama unahitaji ramani! Isipokua kama unajenga msingi wa nyumba yote kisha uinue vyumba viwili kwa ajili ya matumizi ya awali, lkn bora zaidi kua na vyumba viwili vya kujitegemea pembeni ya nyumba
 
Wakuu habari za wakati huu.

Niende moja kwa moja kwenye mada.

Baada ya Kupambana na Mungu kuniwezesha kupata kiwanja. Natamani sana kwa mwaka ujao Mungu anisaidie nianze ujenzi.

Ila ningependeza nianze na vyumba viwili kwanza (chumba na sebule) ili ni niweze kuhamia kwangu kwa kuwa bado sijaoa,, huku nikiendelea kujitafuta kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ambayo itanitoshea mimi na familia yangu.

Ukubwa wa Kiwanja ni (25×40 sqm). Nawakaribisha kwa Ajili ya ushauri na maoni.

NB: Pia ningependa kujua nawezaje kupata ramani ambayo itaniwezesha kukadiria gharama za huo ujenzi
Vipi kuhusu choo?
 
Kuna msemo unasemwa ukianza chumba na sebure, wengi hukwama hapo hapo bila kuendelea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom