Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ulishawahi kupita mahali ukakuta mfuniko wa karo la choo au kisima umewekwa pembeni na sio kati kati?
Je, kati ya mtu aliyeweka mfuniko kati kati na mtu aliyeweka mfuniko pembeni nani yupo sahihi?

Uzito wa zege katika slab hufanya nondo zipinde kutokana na mzigo uliopo juu yake na hizo nondo hupinda zaidi katika eneo la katikati (maximum deflection katika slab inatokea at the midspan of the slab)

Katika eneo la kati (kwa nondo za chini), sio tu kukata nondo kwa ajili ya kuacha uwazi wa mfuniko bali hata kuunga nondo kwa nondo (yaani kufanya overlapping) haitakiwi kwa sababu ndio sehemu ambayo ipo katika risk kubwa ya kufeli

Kwahivyo mtu ambaye anaweka mfuniko wa karo/kisima pembeni (ambapo ndipo kuna deflection ndogo) ndio yupo sahihi (Nitawaletea picha baadae)

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane +255(0)624068809
 
Kabla ya kuanza kupiga plaster katika kuta, hakikisha fundi wako anaweka timanzi katika kuta ili kuhakikisha plaster yako inanyooka vizuri hata kama ukuta ulikuwa umepinda mahali. Ni vizuri timanzi akaziweka siku moja kabla ili zipate muda wa kutosha kukauka

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
timanzi ni nini?
 
Timanzi ni alama ambazo zinawekwa kwenye kuta (nyuso za kuta) au kwenye sakafu ili kuhakikisha sakafu yako inakuwa katika usawa mmoja katika pont zote za chumba/nyumba au kufanya plaster yako katika kuta inyooke kutoka juu kwenda chini.

Mara nyingi huwa tunatumia vipande vya tiles, kama ulishawahi kuona mahali vipande vya tiles vimenasishwa kwenye kuta basi hizo ndio timanzi zenyewe na kuna namna yake ya kuviset, sio kwamba vinapachikwa tu hivi hivi bila vipimo
 
Ukipita baadhi ya nyumba utaona kuna baadhi ya madirisha/milango kunakuwa na nyufa kati ya mkanda wa juu na ile kozi ya tofali ya chini ya mkanda.

Hii huwa inatokea pale mzigo uliopo juu ya mkanda katika madirisha ama milango ni mkubwa kiasi cha kupelekea mkanda upinde kwenda chini, mkanda ukipinda unafanya zile sehemu za mkanda za pembeni karibu na kuta (support) kupanda juu na kufanya mkanda uachane na tofali. Ufa huo huendelea kadri mkanda unavyozidi kuelemewa na mzigo na wakati mwingine kufanya uungane na ufa wa dirisha jingine

Ili kuzuia hii hali, ni vizuri sehemu zote zenye uwazi chini ya mkanda (mfano madirisha, milango n.k) ukaongeza kipande kimoja cha nondo chini kati kati ya nondo mbili, ambapo hicho kipande kikikaribia asilimia 25 ya urefu wa huo uwazi kutokea kwenye ukuta kuja katikati ya dirisha unakikunja kielekee juu kufungwa na nondo za juu kila upande (kulia na kushoto) na pia kipitilize walau kwa futi moja na nusu kutokea kwenye ukuta
 
Kabla ya kuskim gympsum boards zako, hakikisha unaweka fiber tape katika maungio ya gympsum board moja na nyingine

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Ukipita baadhi ya nyumba utaona kuna baadhi ya madirisha/milango kunakuwa na nyufa kati ya mkanda wa juu na ile kozi ya tofali ya chini ya mkanda.

Hii huwa inatokea pale mzigo uliopo juu ya mkanda katika madirisha ama milango ni mkubwa kiasi cha kupelekea mkanda upinde kwenda chini, mkanda ukipinda unafanya zile sehemu za mkanda za pembeni karibu na kuta (support) kupanda juu na kufanya mkanda uachane na tofali. Ufa huo huendelea kadri mkanda unavyozidi kuelemewa na mzigo na wakati mwingine kufanya uungane na ufa wa dirisha jingine

Ili kuzuia hii hali, ni vizuri sehemu zote zenye uwazi chini ya mkanda (mfano madirisha, milango n.k) ukaongeza kipande kimoja cha nondo chini kati kati ya nondo mbili, ambapo hicho kipande kikikaribia asilimia 25 ya urefu wa huo uwazi kutokea kwenye ukuta kuja katikati ya dirisha unakikunja kielekee juu kufungwa na nondo za juu kila upande (kulia na kushoto) na pia kipitilize walau kwa futi moja na nusu kutokea kwenye ukuta
haya maelezo yangekua na kamchoro ingekua safi
 
Nikupongeze mkuu kwa elimu unayoitoa..swali langu kwako ni moja tuu..
Ni kwa namna gani unaweza kujenga msingi wa mawe kwenye ardhi ya udongo wa mfinyanzi..??
Katika udongo wa mfinyanzi, pendelea kuanza na reinforced strip footing (hii kwa kiswahili sijui niite vipi, kiufupi ni zege nene yenye nondo ndani yake ambayo inakuwa inamwagwa kuzunguka msingi wote kabla ya kuanza kupanga tofali/mawe).
NB: Hii ni tofauti kabisa na ile zege nyembamba (blinding concrete), strip footing ni nene zaìdi, blinding concrete yenyewe huwaga ni nchi 2

Hiyo strip footing kwenye udongo wa mfinyanzi inasaidia kuzuia nyufa zinazojitokeza kwenye udongo kutokana na kusinyaa na kutanuka kwa udongo zisiweze kusababisha kuta za msingi kutitia (unequal settlement) na kuleta nyufa/kukatika
 
Katika nyumba za bati la kuficha (contemporary), ni vizuri ukatumia bati za migongo midogo (corrugated) kuliko kutumia bati za migongo mipana (IT 5)

Hii ni kwa sababu, migongo ya bati za IT 5 maarufu kama msouth ipo flat na kasi ya maji ni ndogo sana kutokana na slope ya paa jinsi ilivyo hivyo uwezekano wa maji kuingia katiķa matundu ya misumarì ni mkubwa tofàuti na upande wa bati za migongo midogo ambayo yenyewe migongo yake imechongoka

Ramani, makadirio au ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Ili uweze kutumia tiles zenye size tofauti tofauti katika nyumba (mfano sebleni 60x60, vyumbani 40x40, vyooni 30x30 n.k), inatakiwa uweke step ndogo (hata kama ni ya nchi 1) mahali ambapo pattern mbili tofauti zinakutana ili kuua hizo pattern kwa corner strip

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ramani ya vyumba viwili (vyote self), sebule, jiko, dining na choo cha jumuiya
+255(0)624068809
20240420_152114.jpg
 
Kipindi cha mvua kama hiki, mashimo ya wadudu kama Tandu, Nge, Nyoka n.k hujaa maji hivyo wadudu hawa hukimbia makazi yao na kutafuta hifadhi sehemu zingine zikiwemo makazi ya watu

1. Unashauriwa kabla ya kuvaa viatu ukague vizuri viatu vyako kabla hujavivaa, Tandu na Nge hupendelea kujificha humo kutafuta joto

2. Pekua nyumba yako vizuri japo mara mbili au zaidi kwa mwezi, unaweza ukakuta hata unaishi na Nyoka chini ya sofa, chini ya kabati au kitanda bila wewe kujua

3. Panda mmea wa mchai chai kuzunguka nyumba yako kwani inasemekana ile harufu yake huwakera sana wadudu hatari na kufanya wahame kabisa mazingira hayo

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
 
Kuna fundi kanambia nyumba ya kawaida nondo za mm10 zinatosha kabsa

hii imekaaje?
 
Kuna fundi kanambia nyumba ya kawaida nondo za mm10 zinatosha kabsa

hii imekaaje?
10mm hapana mkuu, sikushauri. Yote hayo watu wanayafanya ili kukwepa ama kupunguza gharama ambazo baadae inaweza ikakuingiza hasara zaidi.

Katika nyumba za kawaida, minimum size ya nondo kwa structure yoyote iwe ni nguzo, mkanda ama slab ni milimita 12.
 
Back
Top Bottom