Ramadhan Special Thread

Mungu akulipe heri Hance Mtanashati
Akujaalie heri dunian na akhera
pamoja na waislamu wote kiujumla Insha Allah ramadhan njema
na katika dua zetu ndugu zangu tusiwasahau ndugu zetu wa turkey iraq libya yemeni na mataifa mengine ya middle east yaliyochafuliwa na wazayuni,ndani ya ramadhani hii Allah (s.w)awajalie umoja subra amani na utulivu
 
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:


Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: 183]

Allaah Anajulisha katika Aliyoyafadhilisha kwa waja Wake kwamba Amewajibisha Swawm kama Alivyowajibisha ummah zilizopita kwa sababu ni shariy’ah (hukmu) na amri zinazomnufaisha binaadamu katika kila zama.

Nayo ni changamoto ya kumhuisha mtu nafsi yake kwani inapasa kushindana na wengine katika mambo ya kheri ili mkamilishe amali zenu na mkimbilie (kuchuma) sifa njema na hakika hayo si katika mambo mazito mliyohusishwa nayo.
Swada mkuu Ngoja tumuangalie huyo muumini ninani?au yupi?
(Qur-an 8:2-4 Surat Al anfaal )

2. Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.

3. Hao ambao wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku.

4. Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao Mlezi.
Hizo ndio sifa za muumini tujilize je sisi ni miongoni mwao?
 
Uzuri Wa Kutekeleza ´Ibaadah Ya Kufunga Mwezi Wa Ramadhaan


Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:

“Yeyote atakayefunga mwezi wa Ramadhaan kwa Imani na kutarajia malipo kutoka kwa Allaah basi Allaah Atamsamehe madhambi yake yote yaliyopita.” [Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, An-Nasaaiy na Ibn Maajah].

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema tena, alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:

“Allaah amesema: “Kila ‘Amali ya mwanaadam ni yake yeye mja Wangu ila Swawm. Ni yangu Mimi na mimi ndiye Nitakayemlipa mja Wangu.”


Swawm ni kinga.

Itakapofikia siku mmoja wenu amefunga ajiepushe na kufanya kitendo cha jimai na mabishano na watu. Na yeyote atakayetaka kupigana naye basi amwambie “Mimi nimefunga.” Naapa kwa jina la Allaah, Harufu inayotoka katika mdomo wa mwenye kufunga ni nzuri kwa Allaah kuliko harufu ya Misk. Kwa Mwenye kufunga ana furaha mbili: Furaha anapofungua Swawm yake na furaha pale atakapoonana na Mola Ameridhika kwa kufunga kwake.”
[Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim na An-Nasaaiy]


Sahl ibn S’ad (Radhiya Allaahu ´anhu) alimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:

‘’Peponi kuna mlango unaitwa Ar-Rayyaan. Wale wenye kufunga wataingia peponi kupitia lango huu siku ya Qiyaamah na hakuna mwengine atakayepita katika mlango huu ila (wafungaji).

Itaambiwa: ‘’Wako wapi waliokuwa wakifunga?” Watasimama na watapita katika mlango huu na watakapomalizika kuingia wote (wafungaji) utafungwa na hakuna mwengine atakayepita hapo tena.“
[Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy na Muslim, At-At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na An-Nasaaiy].
 
Kufunga Mwezi Wa Ramadhaan Ni Wajibu Pale Mwezi Unapoonekana


Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akisema:

“Fungeni kwa kuona au kuandama mwezi wa Ramadhaan na fungueni (malizeni) kufunga mwezi wa Ramadhaan kwa kuona mwezi na msipouona mwezi basi timizeni siku thelathini.”

[Imeripotiwa na Al-Al-Bukhaariy, Muslim, na An-Nasaaiy].
 
Mwezi Wa Ramadhaan Unathibitishwaje Kuonekana Kwake?


Mwezi wa Ramadhaan unathibitishwa kuonekana kwake na mtu mmoja mwenye kujulikana kwa ukweli na kumcha kwake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) au kwa kutimiza siku thelathini za mwezi wa Sha’abaan.

Ibn ´Umar amesema watu walikuwa wakitafuta kuandama kwa mwezi. nikamjulisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) kuwa mimi nimeuona mwezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) akafunga na akaamrisha watu wafunge.
” [Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab I’rwa al-Ghaliyl na. 908 na Imeripotiwa na Abu Daawuwd].


Ikiwa mwezi haukuandama, kwa sababu ya kufunikwa na mawingu au kwa sababu nyingine basi hapo mwezi wa Sha’abaan utatimizwa kwa siku thelathini kama alivyoripoti Abu Hurayrah katika Hadiyth iliyo hapo juu.

Lakini mwezi wa Shawwaal unatangazwa kuonekana kwa mashahidi wawili.’ ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Al-Khattwaab amesema:

“Nilipokuwa nikikhutubia siku ambayo ni ya shaka (kama mwezi wa Ramadhaan kama umekwisha ama la), nikasema: “Nilikaa na Maswahaba zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) nikawauliza wao. Wakaniambia mimi kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alisema:

‘’Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi na tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake. Ikiwa kuna mawingu basi timizeni siku thelathini. Na Ikiwa Waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuonekana kwa mwezi basi fungeni na mfungue kwa kushuhudia kwao mwezi.’’
[Hadiyth Swahiyh. Angalia Kitaab cha Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh al-Jamiy’ Asw-Swaghiyr na. 3811. Pia Imeripotiwa na Imaam Ahmad na An-Nasaaiy bila kipande kinachosema ‘’Waislamu wawili.’’].


Mtawala wa Makkah, Al-Haarith bin Hatwiyb amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alituambia sisi tekelezeni ´Ibaadah ya Hajj kwa haki zake munapouona mwezi. Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini mashahidi wawili wa kuaminika wakishuhudia kwa kuona mwezi tunatekeleza ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’

[Hadiyth Swahiyh angalia Shaykh Al-Albaaniy, Swahiyh Sunan Abiy-Daawuwd, na. 205. Imeripotiwa na Abu Daawuwd].


Tukiangalia ripoti mbili hizi,
’’Ikiwa waislamu wawili watachukua kiapo kwa kuona mwezi, basi fungeni na fungueni’’ katika Hadiyth ya Abdur-Rahmaan bin Zayd na:
‘’Na ikiwa hamkuuona mwezi lakini watu wawili wenye kujulikana kwa ukweli wakasema wameuona mwezi tunatimiza haki za ´Ibaadah ya Hajj kutokana na ushahidi wao.’’ katika Hadiyth ya Al-Haarith wanaonyesha kwa kutilia mkazo, kuwa haifai kuanza kufunga au kumaliza kufunga kutokamana na ushahidi wa mtu mmoja pekee. Juu ya hilo, tangu kuanza kwa kufunga imeondolewa uzito kutokana na ushahidi (uliotolewa hapo juu), inawacha suala la kumaliza kufunga, ambalo halina ushahidi kwamba linatoshelezwa kwa ushahidi wa mtu mmoja pekee.

Huu ni ufupi wa mjadala unaopatikana katika Kitabu ‘Tuhfah Al-Ahwadhiy’ [Mjalada wa 3, uk. 373-3749].


Tanbihi: Ikiwa mtu atauona mwezi yeye peke yake, hafungi mpaka watu wafunge na hamalizi kufunga mpaka watu wamalize kufunga kama ilivyoripotiwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu), kwamba amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam):


‘’Swawm (kufunga) ni siku ambayo watu wanafunga. Na kumaliza kufunga ni siku ambayo watu wanamaliza kufunga. Na kuchinja ni katika siku ambayo watu wanachinja.’’

[Hadiyth Swahiyh. Angalia Swahiyh Al-Jami’ Asw-Swaghiyr, na. 3869].

Imehifadhiwa na Imaam At-At-Tirmidhiy ambaye amesema:

‘’Baadhi ya Maulamaa wanaifasiri Hadiyth hii kwa maana:

“Kuanza kufunga na kumaliza kufunga kunatekelezwa na watu wote kwa pamoja na wakati mmoja.”
 
Back
Top Bottom