Ramadhan Kailima: Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni huru

Uhitaji uchunguzi wowote kuona matendo / kazi ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wakati wa chaguzi zetu. Na hakuna kazi / tendo lolote linaloweza kufanyika bila kuwa na order ya mkuu wao. Ndiyo maana kama ni jambo zuri anasifiwa aliyetoa mkuu wao order na kama ni baya vile vile ananyoshewa kidole mkuu wao aliyetoa order.

Tatizo tunalaumu sana vyombo vya ulinzi! let say kwa Siku moja viamue kukaa kimya nadhani hata hiyo nyumba yako watu watagawana mbao! ni kosa kubwa kuhusisha vyombo vya ulinzi na Usalama na maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la Kura.
 
Kila mtanzania ni mnufaika Uchaguzi wa mwaka 2015 ni somo tosha kuna nchi kibao Tume zao zinayumbayumba sisi Tanzania watu wanakuja kujifunza tunawezaje kufanya chaguzi za amani.
Hongera kaka ila hayo unayo yasema ndo mtaji wenu vijijini kwa wasio jitambua.... hivi kweli we Kinje, tume nzima kuanzia Mwenyekit mpaka wakurugenzi wanateuliwa na mmoja wa washiriki kwenye uchaguzi harafu utegemee tume itende haki.... kweli?
 
Uhitaji uchunguzi wowote kuona matendo / kazi ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wakati wa chaguzi zetu. Na hakuna kazi / tendo lolote linaloweza kufanyika bila kuwa na order ya mkuu wao. Ndiyo maana kama ni jambo zuri anasifiwa aliyetoa mkuu wao order na kama ni baya vile vile ananyoshewa kidole mkuu wao aliyetoa order.

Kaka yangu Ruga huna namna unavyoweza kuviweka pembeni vyombo vya Ulinzi hasa linapokuja suala la usalama wa vituo vya kupigia kura, wananchi n.k hakuna nchi inayojiendea yenyewe bila ulinzi.
 
Hongera kaka ila hayo unayo yasema ndo mtaji wenu vijijini kwa wasio jitambua.... hivi kweli we Kinje, tume nzima kuanzia Mwenyekit mpaka wakurugenzi wanateuliwa na mmoja wa washiriki kwenye uchaguzi harafu utegemee tume itende haki.... kweli?

Sio kweli najua tutatofautiana hapa, ingekua ni hivyo basi Upinzani wasingekua na Mbunge hata mmoja, au Mgombea wa Upinzani wa Urais mwaka 2015 asingepata Kura zile. Cha msingi ni uelewa wa pamoja na tuwe na tabia ya kukubali matokeo, na pia Anaposhinda mgombea mwingine tofauti na uliyemtarajia haimanishi hakuna Haki.
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima amesema chombo anachokiongoza na kukisimamia kinatekeleza majukumu yake kwa Uhuru na wala hakiingiliwi na mtu, chama au kikundi chochote katika kutekeleza majukumu yake ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria, amewataka wanasiasa kote nchini wajiamini. Msikilize hapa akizungumza katika mahojiano Mubashara Dodoma FM

Kwakuwa mmewekwa kwa ajiri ya kunyonga haki za vyama vingine hamuoni aibu lkn amini nawaambia hakuna hukum mtakayoikimbia kwa maamuzi yenu machafu yenye kuchefua c tume huru hata siku moja
 
???????????????????????????????????????????
 
Wakenya walipata Tume huru ila ni balaa eti hawaiamini , Tatizo wanasiasa wa Tanzania hawajiamini wanaishi kwa hisia na kuwaza kuibiwa kura. Tanzania wagombea wanaposhindwa uchaguzi, hata kama mtu kapata kura 1 na mwenzake kapata 5000 anasema wamemuibia kura wanasiasa wanatuponza sana hawaelewi siasa pia maana ya Uchaguzi.
Toka lini tume huru ikachaguliwa kwa design hii ya Tanzania. Kila mtu Altona jinsi maafisa walivyoondolewa kwenye nafasi zao kabla ya uchaguzi. Malengo yake yalikuwa nini?

Actually, kudai eti Tanzania Tume yake ni huru na ya uwazi kuliko SADC yote ni kuwafanya Watanzania ni mazuzu.
 
Kaka yangu Ruga huna namna unavyoweza kuviweka pembeni vyombo vya Ulinzi hasa linapokuja suala la usalama wa vituo vya kupigia kura, wananchi n.k hakuna nchi inayojiendea yenyewe bila ulinzi.
Swala siyo uwepo wao, na kimsingi vinahitajika sana tena sana, linalotia shaka ni pale ukiukwaji wa sharia taratibu na kanuni unapokiukwa wazi wazi na pengine kwa kusaidiwa na vyombo hivyo hivyo kwa masilahi ya upande mmoja uenda kwa maelekezo maalumu. Hiyo ndiyo inakuwa taabu na shida dada yangu
 
Sio kweli najua tutatofautiana hapa, ingekua ni hivyo basi Upinzani wasingekua na Mbunge hata mmoja, au Mgombea wa Upinzani wa Urais mwaka 2015 asingepata Kura zile. Cha msingi ni uelewa wa pamoja na tuwe na tabia ya kukubali matokeo, na pia Anaposhinda mgombea mwingine tofauti na uliyemtarajia haimanishi hakuna Haki.
Sasa shida iko wapi kuwa na tume huru ya uchaguzi kama mnaamini hivo?. Simba na yanga wenyewe refa atajulikana siku ya mechi sembuse uchaguzi.. . Hizo fikra zenu kawalisheni huko vijijini kanswenswe....#TUME-HURU-YA-UCHAGUZI
 
Swala siyo uwepo wao, na kimsingi vinahitajika sana tena sana, linalotia shaka ni pale ukiukwaji wa sharia taratibu na kanuni unapokiukwa wazi wazi na pengine kwa kusaidiwa na vyombo hivyo hivyo kwa masilahi ya upande mmoja uenda kwa maelekezo maalumu. Hiyo ndiyo inakuwa taabu na shida dada yangu
Sasa shida iko wapi kuwa na tume huru ya uchaguzi kama mnaamini hivo?. Simba na yanga wenyewe refa atajulikana siku ya mechi sembuse uchaguzi.. . Hizo fikra zenu kawalisheni huko vijijini kanswenswe....#TUME-HURU-YA-UCHAGUZI

Sikio la kufa halisikii dawa!
 
Wanakuja kujifunza lakini wanaishia kushangaa huu uwizi unaofanyika. Wenyewe wanasema siku Watanzania wakiacha ukondoo basi mambo yatakuwa mengine. Ki ujumla huwa wanasikitika kupoteza muda wao kuja kujifunza kwa raia makondoo wakati nchini mwao uwezo wa wananchi wao kujitambua ni mkubwa.

Usilete dharau, hakuna ukondoo kwenye maamuzi ya Watanzania! Unachokiongea sio sawa na sio sahihi na inaelekea unatakiwa kuelimishwa, Watanzania wana akili sawasawa.
 
Pole vumilia kwani ukweli una tabia ya kuuma hivyo sishangai ww ukiugulia maumivu ya ukweli.
 
Back
Top Bottom