Aidha ni miongoni mwa wenye kumwangusha Rais Samia na au anafanya yaleyale ya mtanifanya nini!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,118
Samahani, kwa sasa nitakuwa naanza na neno Watu weusi pausua kichwa, tunamatatizo gani? Mbona hatuwezi karibu kila kitu?

Baada ya kutugundua na kujiaminisha kwamba, Watanzania hata uwafanyie ubaya unaozidi ubaya, hawawezi kukufanya chochote, zaidi sana wataandika na kulalamika huku wakiishia mitandaoni, ndicho wanachotufanyia viongozi wa CCM

Yumkini Waziri wa Nishati ndiyo wale viongozi wa ccm ambao hawampendi kabisa Rais aliyepo na ama anachotufanyia watanzania ni kile kiburi cha mtanifanya nini na mimi ndiye mimi na kwamba nikiamua umeme uwake masaa 5 badala ya masaa 24 mtafanya nini nyinyi watanzania msiojua maumivu yoyote kuhusu uchumi wenu?

Tangu nimekuwa nikajielewa, naelewa fika kwamba, majira ya kiangazi umeme wetu huwa tia maji tia maji, lakini wakati wa mvua, tunakuwa na umeme usio na shida

Ninachokiona kwa sasa, ni sawa na kwamba, tupo kwenye majira ya kiangazi mabwawa yetu hayana na yamekauka maji,

Hizi mvua ambazo sasa mpaka zimekuwa kero, ni bwawa lipi ambalo halijajaa maji?

Waziri wa Nishati Mh. Dotto Biteko, embu toka hadharani utwambue wananchi wenzako tatizo la umeme linasababishwa na nini?

Hatuoni sababu kukosa umeme kwa sasa!

Kumbe Makamba na wewe ni wale wale mnazidiana matamko tu

Hiyo wizara amekosekana wa kuiweza? Si apewe sasa aliyekuwa waziri kipindi cha Magufuli Kalemani!
 
Shida hapo Tanesco watumishi wa parokia wamejazana na hawana ubunifu,hawana hofu ya mungu,wanachojua ni kuiba na kuhujumu serikali
 
Kwani tatizo la umeme shida ni Waziri? Ukiteuliwa wewe umeme Utawaka?
 
Back
Top Bottom