Bonson
Senior Member
- Apr 20, 2013
- 183
- 147
Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Magufuli,
Watanzania tulio wengi tunamshukuru Mungu kwa ajili yako. Hadi sasa umeweza kutatua matatizo mengi sugu kwa wananchi wako.
Moja kati ya tatizo linalonikera mimi pamoja na watanzania wengine ni jinsi ambavyo Ubalozi wa USA na UK wanavyotufanya katika maombi ya VISA. Yani unalipishwa kiasi kikubwa cha pesa katika maombi ya VISA, halafu ukikosea kujaza forms, au baadhi ya vielelezo vikipungua, basi unanyimwa VISA na pesa hairudi. Ukitaka ku-apply tena wanakwambia lipia upya. Kwanini hawa watu wasijifunze kwa Ubalozi wa Korea Kusini? Ubalozi wa Korea Kusini hawachukui pesa yako hadi wahakikishe una vigezo vyote vya kupewa VISA. Yani ukisha lipia tu ujue umepata VISA.
Kinachoniuma zaidi ni usumbufu wa kupewa VISA wakati wao wanapokuja kwetu wanachukulia VISA zetu airport.
Mheshimiwa Rais, naomba Serikali yako iliangazie swala hili.
Dhuluma katika upatikanaji wa VISA za USA & UK ni jipu la kutumbuliwa sasa.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania