Rais wetu kupewa jezi ya RONALDO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wetu kupewa jezi ya RONALDO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredwash, Mar 17, 2010.

 1. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 593
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Kwanza kabisa napenda kutoa anaglizo... ikiwa unaona nimekurupuka pasipo kufikiri kuandika hii article basi niwie radhi au pengine ni uelewa wangu mdogo wa jinsi mnavyoendesha hii serikali yenu

  Kama kawaida tumeona jinsi viongozi wetu walivyo na mawazo finyu au sijui ni kupenda kutanguliza hisia zao au basi kuonekana kwa hao wanaowatukuza. kwa kumfanya rais wetu kituko... Kama kuna vitu vilivyonikera katika wiki hii basi ni lile la "RAIS" wetu kwenda kwenye halfa then akapewa jezi ya ronaldo wa madrid.. ikidaiwa kuwa madrid wametoa kwa kutambua mchango wake michezoni... khaaaa! YAAANI jesus inaonekana dhahiri kuwa achilia mbali huyo perez hata ronaldo au huyo ronaldo bali hata mtu wa habari na mawasiliano wa madrid hana habari hizo... yaani meya wa jiji letu akampe rais wake jezi ya mchezaji wa timu( tena club tu na sio timu ya taifa) ya nje ambayo haina na haijawahi kuwa na nasaba au ushirikiano wa aina yoyote na tanzania katika nyanja yoyote ile... ampe kama zawadi kwa kutambua mchango wako michezoni... yeye kimbisa ni nani hadi hicho ki halfa kifanyike kiaina na yeye apewe jezi ampe rais wake yaani yeye ndio mwakilishi wa madrid... huku ni kudharauliana kupita kiasi... hivi ni mchango gani wa michezo aliofanya kikwete kiasi cha kuwagusa hao madrid kutoa hiyo jezi..haya ni matokeo ya rais kujifanya BABU wa kila mtu... yeyote anayeamua kuji show off anaanda kisherehe anamwita rais anakuja kumpa chochote akidai anathamini mchango wake.... tusijeshangaa wa man u na arsenal nao au hata mashoga wa ulaya wakija kumpa zawadi rais wetu.......

  Rais aache kufanya mambo ya maaana uende akatukuze kitu cha nchi ya nje ambacho hakina msingi wowote achilia mbali kama hao watu wa madrid wana taarifa ama la..... VYOVYOTE ILIVYO KAMA HALFA HIYO INA MKONO KWELI WA MADRID HATA KAMA HUYO PEREZ ANGEKUJA MWENYEWE KUTOA BADO ITS NONSENSE.... MKAPA ALIKUWA HANA TIME NA UPUUUZI WA AINA HII

  Ndio shansema sasa..........................khe!
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  ni shabiki wa madrid - ameahidi kuwaleta bongo kabla ya uchaguzi---
   
 3. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani hata kujadili hili naona soni...! ni aibu aibu kubwa..!
  [​IMG]
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  JK mtu wa WATU bwana. Matamasha yumo, kombe la FIFA yupo, Hashim Thabeet kala naye lunch, kapiga picha na Bi Kidude, Leo kasaini muswada "live" wa pesa za matumizi ya uchaguzi, mawodini kwa wagonjwa utamkuta, misibani, mazishini hakosi,......
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Hiyo ilikuwa personal issue....unapotoka kwenye media inakua public...jezy kama hiyo machinga wanauza mitaani
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa rais wetu hataki kupitwa na chochote, anyway angekuwa sio maarufu tungesema anautafuta, lakini sasa sijui nisemeje ??????????????
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kelele za chura....
  Mtasema mchana, usiku mtalala...
  Mwenzenu mwezi wa kumi anashinda kwa asilimia 70 ya wafuata upepo...

  Kulijadili hili kweli ni kupoteza muda.
   
 8. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona hapa JK anatafuta kura mwaka 2010 kwa kila njia. Hapa wanaoombwa kura ni wapenzi wa timu husika na labda wa mpira wa miguu au michezo kwa ujumla wake
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hahaha inafurahisha ..Rais yuko Kikazi zaidi
   
 10. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hayo mabilioni yaliyomshina kipindi kile leo atayatoa wapi?
   
 11. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  wehu tu
   
 12. D

  Donrich Senior Member

  #12
  Mar 17, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nilipoiona hii habari kwa mara ya kwanza katika vyombo vya habari vya Tanzania,nilistuka sana,kwamba raisi amepewa zawadi ya jezi ya mchezaji wa nchi ya ulaya,..nilijiuliza uzalendo upo wapi?,ni kwa nini wasimpe zawadi ya mchezaji wa Taifa au timu yeyote ya nyumbani?,Katika hali ya namna hii tunawatia moyo wachezaji wetu wa ndani au tunawakatisha tamaa...infact inatia aibu.
   
 13. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mkwere kapewa nchi aiongoze. kama hupendi anayofanya au anayofanyiwa basi wewe Jeuri. nakushauri kuanzia sasa wewe sema Hewala Bwana kwa lolote linalomhusu Mkwere. Mind you ana miaka mingine mitano Magogoni pale.
   
 14. MANI

  MANI Platinum Member

  #14
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Nafikiri ni wakati washauri wake wawe wanampangia nini cha kufanya public na personal ila sidhani kama itawezekana kama alikataa ushauri wa kumpumzika kwa ajili ya afya yake sasa hili la kujenga umaarufu atakubali?
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ha ha ha hawa viongozi wetu ni vikatuni kupita kiasi kusema kweli.nilicheka sana nikasema mtu kasaidia kukuza michezo nchini kwake anaenda kupewa jezi ya madrid? sasa hapa ndio tunapiga vita vitu vya mchina wakati mpaka viongozi wetu wenyewe hawathamini vya nyumbani?

  jezi zote za nyumbani hizo kashindwa kumpa? kama raisi mshabiki wa madrid si angempa hio jezi wakati wa birthday yake huko vichochoroni?

  hawajamaa niwachemkaji sana,mambo ya vijiweni ndio vinawapotosha hawa viongozi wetu.
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Rais wenu aliyepita mlisema hapendi michezo, sasa mmepata anayependa michezo bado mnalalamika - kosa lipi alilolifanya hapo? kupokea jezi na kuongea na mmiliki / kocha wa madrid ni kosa? mnataka Rais wenu afikirie mambo ya mafuriko, wodi za kinamama wazazi , barabara hafifu, maisha duni ya wananchi wake. ajali za barabarani, ufisadi nk muda wote akiwa ikulu? mnataka afe kabla ya muda wake? aaa mwacheni naye afanye walau social activites ajisahaulishe kidogo na matatizo ya nchi yetu - muda kidogo anaopata basi na yeye afurahi na bi kidude - i think its ok.

  Msimlaumu sana -
  a) Sioni kosa kupokea ile jezi - kwani ameiabisha nchi kuwa na jezi ya Ronaldo?- angalia maudhui ya rais kwenda huko yalikuwa nini si uangalie upokeaji wa jezi tu.

  b) Sioni tatizo kumpokea mwanamichezo yoyote maarufu wa kitanzania - kumkaribisha ikulu na kula naye chakula

  Cha msingi ni kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu - Rais hawezi kutufanyia sisi kila kitu - haiwezekani- tutaishia kulalama na miaka inasonga mbele- kuna watu hapa JF wanapenda kulaumu tu wakati wao wenyewe ni mizigo tosha kwa taifa letu.

  Ukiwa maskini wa pesa na fukara wa mawazo, ukaamua kujifungia ndani kwako na familia yako - utakuwa maskini na fukara milele - Toka nje angalia wenzako wanafanya nini, ongea nao, jifunze toka kwao - then jaribu kufanya mwenyewe - thats what Mr President is doing.
   
 17. Miwani

  Miwani Senior Member

  #17
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 182
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni aibu hata kujadili hii topic
   
 18. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Safari bado ni ndefu kweli.............
   
 19. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni sawa kabisa kwa mambo mepesi mepesi kama hayo yumo kwa masuala magumu ya kitaifa kama kulinda maliasili yetu hajui afanyeje
   
 20. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Tha make the two of us!!
   
Loading...