Rais wetu Asaidiwe kuandaa Hotuba

Rais wetu Asaidiwe kuandaa Hotuba

Ukiachia mambo ya uanamtandao, urafiki, upenzi, kujuana, nk. katika kupeana kazi, mambo ambayo Rais wetu amejidhihirisha kuwa "sterling", mimi naona Rais kwa kumchagua January Makamba kuwa mwandika hotuba zake, ambazo sasa tunazilalamikia, amefanya makosa mawili tunayoyaita "fallacy of association". Kwanza, amemu"associate" January na baba yake - mzee makamba. Pili, ame"associate" eloquence ya public speech na kuwa writer. Yaani kwa kiingereza wanasema "a great speaker is also a good writer". Haya ni makosa yanayowakumba sana watu wenye uwezo mdogo kiakili wa kuchambua mambo kiundani, yaani "people with limited minds go with associations". Maana unaweza kuwa great public speaker lakini si kwa hoja bali ni kwa vichekesho na burudani. Hivyo hata utakachoandika kitaendana na mind ya ki"comedy". Pili, si lazima kipaji cha baba ndicho kipaji cha mtoto. Unapompa kazi mtu, hasa katika nafasi nyeti, unapaswa kumjua kwa ndani mteule wako, hapo inabidi uende hatua moja mbele kukiruka kihunzi cha "association". Yaani ufanye analysis za ideas za mteule kabla ya kumpa nafasi.
 
Rais wetu anajitahidi sana kuoanisha lile analolisema na hatua anazochukua. Sema tu wengi tulishamhukumu hata kabla ya kumsikiliza.
 
I don't care about whether speech reflect who you are or not!

Mimi nahitaji mkuu wa nchi anayewafanya watanzania wafanye kazi; anayeweza kuwaondoa watanzania kwenye ugonjwa wa siasa kila mahali hata pale ambapo si muhimu siasa iwepo...

Sipendi kiongozi yeyote yule anayejinadi kwamba atawaletea wananchi maendeleo... Nahitaji kiongozi anayewaambia wananchi tangu kwenye uchaguzi kwamba nitawaongoza mujiletee maendeleo...

Kwa sababu tukiongoze kufanya kazi kwa 20% tu... effect kwenye uchumi inaweza kuwa 50%

Kitendo cha kujadili hotuba za Rais badala ya kujadili kipi kimefanyika na kipi hakijafanyika.... ni muendelezo wa ugonjwa wetu wa muda mrefu wa kuweka siasa mbele.

Leo nilibahatika kuona gazeti moja la kiingereza linalotoka kila jumapili amini usiamini zaidi ya 40% ya contents ilikuwa EPA, na Oboma... sasa hapo nchi itaendelea vipi... Hakuna habari za Kilimo, Miundombinu, Ufugaji, Uvuvi etc.

Sifa ya Rais gani anaingia madarakani inatokana na rai wanahitaji nini wakati gani? Mfano... Mkapa aliingia kwa wakati muafaka...

Na kulingana na ya utawala wa Mkapa, alihitaji Kikwete... hayo mambo yenu ya EPA baada ya muda mutaona hayana maana, mutatafuta Rais wa Kukuza uchumi...ndio evolution ya Taifa... Hakuna Rais hata awe vipi ataweza kujibu hoja za miaka 15 mfululizo... Kawaida ukiingia madarakani kuna unayoleta mazuri alafu kutakuwa na ambayo umeyarudisha nyuma....

Kwa hiyo unataka kiongozi na hotuba kama hii bonyeza hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23484-sambwee-shitambala.html

Hii hapa chini


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23484-sambwee-shitambala.html
HOTUBA YA SAMBWEE SHITAMBALA- MGOMBEA MTEULE (CHADEMA) ALIYOITOA KATIKA OFISI YA CHAMA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI WA KUELEKEA KURUDISHA FOMU YA KUGOMBEA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI 27 DISEMBA 2008

Waheshimiwa viongozi wa CHADEMA;
Watanzania wenzangu, wanaMbeya Vijijini-wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana, itifaki zote nimezingatia.

Amani iwe kwenu.

Awali ya yote nimshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha jumuika pamoja leo mkiwa mmekusanyika kunindikiza kwenda kurejesha fomu za kugombea ubunge jimbo la Mbeya vijijini katika uchaguzi mdogo wa marudio jimbo la Mbeya vijijini. Tunajumuika leo, ikiwa ni siku moja toka kusherehekea sikukuu ya Noeli ambayo kwa waamini; ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa ukombozi.

Nawashukuru kwa kujumuika nami kunisindikiza kwa kuwa suala la kurejesha kwangu fomu, na kugombea kwa kwangu; si la kwangu peke yangu, ni suala la umma. Mtafahamu kwamba CHADEMA inaamini katika falsafa ya “Nguvu ya Umma”, kwa umma wa watanzania ndio una mamlaka juu ya viongozi wao. Chini ya falsafa hii, mimi ambaye CHADEMA imeniteua kugombea ubunge katika kura za awali na Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Mbeya Vijijini iliteua katika uteuzi wa awali Disemba 17 na baadaye kuthibitishwa na Kamati Kuu Disemba 20; nawajibika kwa umma wa wanachama. Naamini, ndio maana mmeamua kujitokeza kunisindikiza kutekeleza wajibu wa demokrasia na maendeleo. Na mara baada ya kurejesha fomu kwa tume ya uchaguzi leo Disemba 27 na kuteuliwa kuwa mgombea, nitawajibika kujieleza kwa umma wa wananchi wa Mbeya vijijini katika kampeni. Hivyo leo, sitazungumza nanyi kwa nia ya kupiga kampeni, wakati wake bado. Baadhi yenu hapa, mmenidhamini na kuweka saini zenu katika fomu yangu ya kugombea, kila mmoja kwa wakati wake; kila mmoja akiwa na sababu ya kwanini ameamua kunidhamini. Nichukue fursa hii kuwaeleza, maono yangu kuhusu dhamira yetu ya pamoja, ambayo naamini ndio sababu ya nyinyi kunidhamini na wengine wengi zaidi kunithamini kwa kujitokeza kunisindikiza kwenda kurujesha fomu. Tutaipeleka fomu hii kwa msimamizi wa uchaguzi ambaye ofisi yake ipo Mbeya Mjini kutokana na halmashauri kutokuwa na makao makuu yake ndani ya wilaya yetu; tunahitaji uongozi mbadala utakaotoa msukumo wa kuhakikisha makao makuu ya Mbeya vijijini yanakuwa Mbeya Vijijini.

Taifa letu linapita katika wakati mgumu wenye ombwe la uongozi katika maeneo mbalimbali; ambalo kwa bahati, chini ya mfumo wa vyama vingi kuna tumaini la kupata uongozi mbadala. Ni wajibu huu wa kidemokrasia umenifanya nijitokeze kuchukua fomu ya kugombea; ni wajibu huu huu wa kihistoria ndio unaotufanya leo kujumuika pamoja kunisindikiza kurejesha fomu hii ya kugombea.

Nayakumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere niliyojifunza wakati nikiwa shule ya msingi Uyole kati ya mwaka 1977 na 1982; kwamba ili taifa liendelee linahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Nikiyatafakari maneno hayo wakati huu; naona watu katika nchi yetu wameongezeka hata hapa Mbeya Vijijini, wakiwa na utamaduni ule ule wa ukarimu. Pamoja na kuongezeka kwa umasikini na gharama za maisha, watanzania wana matumaini ya mabadiliko. Na ongezeko hili la watu, limelazimisha kuwepo mifumo ya kidemokrasia ya uwakilishi; hivyo, fomu hii ninayoipeleka leo, si yangu- ni fomu ya umma, wadhamini waliopo ni wanawakilisha dhamira ya wote wanaotaka niwe muwakilishi wa wananchi wa Mbeya vijini katika Bunge la Tanzania. Kitendo cha kukubali dhamana hiyo, ni ishara ya kuukubali wajibu wa kuwa mtumishi na kiongozi wa watu. Hivyo ndivyo, uongozi wangu utakavyokuwa.

Nikiyatakari maneno hayo, naona ardhi bado tunayo. Tena mkoa wetu wa Mbeya umejaliwa ardhi yenye rutuba na rasilimali. Ni mkoa uliojaliwa ardhi yenye kuzalisha mazao mbalimbali, na ardhi yenye madini mbalimbali. Hali iko hivyo pia hapa kwetu Mbeya Vijijini. Lakini pamoja na hali hiyo, sera za umiliki wa ardhi hazikidhi matakwa ya umma; na katika maeneo ambayo wananchi wamenyanganywa ardhi kwa sababu moja au nyingine wamekuwa wakipata fidia kidogo na wengine wakikosa kabisa. Hata wanaondesha kilimo katika ardhi waliyopo bado tija imekuwa si ya kutosha. Na kwa upande mwingine, rasilimali ikiwemo madini zimekuwa hazitumiki ipasavyo katika kuleta maendeleo. Katika hali hii, mimi niliyepata fursa ya kusoma kwa kodi zenu wananchi wenzangu shahada ya sheria pale Chuo Kikuu cha Dar es salaam na baadaye kwenda kusoma shahada ya pili ya Sheria Chuo Cha Keele Nchini Uingereza, naamini nina deni kwenu. Sehemu ya kulipa deni hilo, ni kutumia taaluma yangu ya uanasheria kuwatetea wananchi wanakosa haki zao ikiwemo haki ya ardhi, lakini pia kutumia uwakili wangu kuwawakilisha wananchi katika vyombo vya kutunga sheria ili kutoa wigo mpana zaidi wa kutetea rasilimali za wananchi wa Mbeya vijijini na taifa kwa ujumla. CHADEMA imeonyesha dhahiri kuwa na wabunge wenye kutetea rasilimali za Taifa, kama Zitto Kabwe na wengine.

Nikiyatafakari maneno hayo; tunakosa mahitaji muhimu mawili ya maendeleo, siasa safi na uongozi bora. Hivyo, tunaongozana leo kwenda kurudisha fomu kama ishara ya kuonyesha dhamira yetu ya pamoja katika kuleta siasa safi na uongozi bora katika Jimbo letu la Mbeya Vijijini na taifa kwa ujumla ili kuunganisha watu watumie ardhi yetu katika kuleta maendeleo.

Tunachokiona leo, ni siasa chafu hususani ndani ya CCM; zenye kuchochea mifarakano, ukabila. Hapa mkoa wa Mbeya zimekuwa zikitokeza katika sura ya makundi ambayo hatimaye yamekuwa yakikwaza maendeleo. Siasa hizi chafu, zimekuwa zikichafua fursa ya baadhi ya watu wazuri katika jamii kushindwa kuchaguliwa kuwa viongozi. Wakati umefika, wa wote wasiopenda siasa chafu, kuunga mkono mabadiliko; bila kujali kabila, chama au hali. Siasa hizo chafu, zinajitokeza pia wakati wa uchaguzi, siasa za kuwahonga wapiga kura, siasa za vitisho kwa wananchi, siasa za uongo na pengine siasa za ushirikina. Leo tunakwenda kurudisha fomu, tukiwa na dhamira ya kuleta tumaini jipya la siasa safi katika mkoa wa Mbeya, siasa za hoja na sera; siasa zenye maadili ya kisiasa. Siasa zenye kuamini kwamba sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Na kwa kweli, dhamira hii ya pamoja nilishaanza kuitekeleza miaka mingi nyuma kabla hata ya kuwaza kuwa mbunge. Mathalani, wakati Diwani wa CCM na wananchi wenzake wa kata ya Isuto wa vyama mbalimbali walipobambikiziwa kesi wakati wakiwa katika kuunganisha nguvu kupingana na ufisadi; nilijitolea kuwatetea katika mahakama kama chombo cha usimamizi wa sheria. Dhamira yetu ya pamoja leo ninaporudisha fomu, ni kutaka kuongezewa wajibu wa uongozi, ili niweze kutoa mchango mkubwa zaidi katika kukabiliana na aina zote za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Hatima ya yote, ni siasa hizo safi ndizo zitakazotuletea uongozi bora katika jimbo letu la Mbeya vijijini na taifa kwa ujumla. Uongozi bora unaotambua mahitaji ya watu. Na ili tupate uongozi huo, tuhahitaji kubadili mfumo wa utawala. Ni siasa safi ndizo zitakazoleta uongozi wenye uadilifu utakaotutoa katika utamaduni wa ufisadi. Huu ni uongozi wenye kuelewa kwamba mabadiliko ya Kweli, hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale, wa chama kile kile, chenye uoza ule ule, wakiendeleza yale yale kwa ari, nguvu na kasi mpya. Ni muhimu wananchi wote wakatambua kwamba kwa falsafa ya chukua chako mapema, Tanzania yenye neema haiwezekani. Uchaguzi wa Mbeya vijijini ni fursa ya kuongeza tofali lingine katika msingi huo. Naamini wote ambao mmenidhamini na kunisindikiza leo, mmefanya hivyo mkielewa vyema uadilifu wangu na dhamira yangu ya kupambana na aina zote za ufisadi.

Tufike mahali tukubaliane, kwamba ni matatizo ya mfumo wetu wa uongozi ndiyo yametufikisha hapa tulipo. Ambapo, gharama za maisha zimepanda kwa ari, nguvu na kasi mpya. Huku bei ya mafuta ikiwa imeshuka duniani hali ni tofauti Tanzania kutokana na usimamizi mbovu na mzigo wa kodi wenye athari zaidi kwa masikini. Pembejeo na mbolea ya ruzuku ambayo kimsingi si hisani ya serikali bali ni mchango wa kodi yangu mimi na wewe, imepanda bei, chanzo kikuu kikiwa ni ufisadi katika mfumo wa usambazaji. Hata katika mfumo wa kugawiwa pembejeo kwa vocha, mbolea inafikia watu wachache tena hata hao kwa kiasi kidogo. Na katika kipindi hiki cha uchaguzi, tayari mbolea imeanza kutumiwa kisiasa kuwagawa watu na kuwaghilibu. Ni wakati wa wananchi kuamka kuelewa kwamba ni zao la kodi na jasho lao, serikali ni chombo tu cha kuratibu upatikanaji. Na kiongozi wa kuunganisha nguvu hiyo ya pamoja, hawezi kuwa mbunge wa chama ambacho ndio kimeweka mfumo huo mbovu bali mbunge wa kambi ya upinzani. Hivyo, ni wakati wa wananchi wa Mbeya Vijijini kuunga mkono upinzani na kutimiza wajibu wa kihistoria wa kuongeza upinzani bungeni kupitia CHADEMA, chama mbadala.

Ni uongozi bora wa CHADEMA ndio uliowezesha wananchi wa Karatu kupata maji baada ya kuukataa utawala wa miaka mingi wa CCM ulioshindwa kutimiza wajibu wake. Ndio uongozi bora wa CHADEMA wenye sera mbadala ndio uliowezesha kule Tarime watoto wa watanzania wa kawaida kusomeshwa bure kupitia mapato ya kwenye madini. Ni uongozi bora wa CHADEMA uliosukuma kufuta kwa michango ya manyayaso kule Kigoma Ujiji. Sio uongozi unaoweka nguzo za umeme miaka mingi zioze bila ya kuvuta umeme kwa wananchi waliowengi. Sio uongozi unaokusanya michango ya ujenzi wa sekondari kwa manyanyaso na kushindwa kukwepa kusoma kwa wananchi mapato na matumizi ya michango mbalimbali. Hivyo, uongozi mbadala unahitajika Mbeya Vijijini kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazokabili wilaya yetu na jimbo letu. Uchaguzi wa Januari 25 ni hatua muhimu katika safari yetu ya pamoja na kuelekea katika njia sahihi ya demokrasia na maendeleo.

Tumaini jipya limekuja Mbeya Vijijini, hili ni tumaini la mabadiliko ya kweli. Tumaini la kuwapima viongozi, sio kwa maneno yao tu; bali kwa matendo yao. Ni wakati wa kuwatambua kwa matendo yao. Wale wanaohubiri kupinga dhuluma, huku wakishiriki na kushirikishwa kutoa rushwa ili wachaguliwe kuwa viongozi; tuwatambue kwa matendo yao. Wale wanaojinadi kuwatetea wananchi huku wakiwazunguka na kuwanyanganya ardhi na mali zao bila fidia inayostahili; tuwatambue kwa matendo yao. Wale wanajifu uhuru huku wakirudisha taifa katika ukoloni mamboleo wakutegemea wageni kwa kisingizio cha uwekezaji uchwara wenye kuwanyonya raia; tuwatambue kwa matendo yao. Wale wanaojitangaza kutetea haki za wafanyakazi huku wakiwanyonya wafanyakazi kwa kuwalipa chini ya kima cha chini; tuwatambue kwa matendo yao. Wale wanaohubiri kuwa wacha Mungu mchana na usiku kubariki ushirikina; tuwatambue kwa matendo yao. Mbwa mwitu, hata ajivike ngozi ya kujifunika na kujifanya mchungaji wa kundi la kondoo; tuhakikishe anafichuliwa. Ndio namna pekee ya kurudisha taifa letu katika misingi ya uongozi bora. Tuyasikilize maneno yao, tuyachambue matendo yao; tuuweke bayana uongo wao, na hatimaye ukweli utufanye tuwe huru. Mapambano ya ufisadi yaliyochochewa na harakati za CHADEMA ikiwemo kupitia ile orodha ya mafisadi iliyotolewa na Mbunge Dr Slaa na wenzake, yanapaswa kuungwa mkono na wote wanaochukia ufisadi; halaiki hii inayonisindikiza kurudisha fomu ni ishara ya kuniunga mkono niwe kamanda wa zaida katika mapambano hayo.

Na huu ni wajibu wa pamoja; si wa jibu wangu pekee, wala si wajibu wa nyinyi mlionidhamini na mnaonisindikiza pekee. Nilipokuwa mtoto, baba yangu Mzee Shitambala Mwaifani Mwalyego-mzaliwa Lwanjilo na kuhamia Uyole kwa ajili ya usimamizi wa uchifu; alikuwa akinilea na kunifundisha kuhusu uwajibikaji. Ni malezi haya ndiyo yaliyonifanya hata nilipokuwa Mwalimu pale Sekondari ya Irambo tulikuwa tukiunganisha juhudi na maarifa. Naamini, ni kwa sababu hii niliweza kustaafu jeshi kwa heshima zote nikiwa na cheo cha kapteni ili kunipa fursa ya kuwajibika kwa upana zaidi katika kutumikia umma kama mwanasheria. Ninaposimama mbele yenu leo, mkiwa mmenidhamini na wengine kuamua kunisindikiza kwenda kurejesha fomu; naiona safari ya uwajibikaji wa pamoja tunayoianza katika kuleta demokrasia na maendeleo Mbeya Vijijini. Safari hii inahitaji baraka na kuungwa mkono na machifu wote; bila kujali itikadi, kabila, eneo ama hali hali. Ni mwito wa wajibu wa pamoja wa kutetea haki za wananchi, kukemea maovu na kuhamasisha maendeleo. Ni wajibu wa wazee wanaotaka kuona matunda ya uhuru walioyatazamia yanapatikana kwa kizazi cha sasa na vijavyo. Ni wajibu wa wanawake ambao ni chimbuko la maendeleo na wazazi wa ukombozi. Ni wajibu wa vijana ambao wameona mabadiliko katika mataifa mbalimbali na wamekuwa nguvu ya mabadiliko hayo. Leo nimeeleza hii dhamira ya pamoja ambayo inatuunganisha, leo haikuwa siku ya kampeni; hivyo, nimedokeza tu dhamira yangu, lakini ahadi zangu na za chama changu, kuhusu nini tutawafanyia wananchi wa Mbeya, nitaeleza wakati nazindua kampeni baada ya kupitishwa na Tume ya Uchaguzi kutokana na fomu ninayoipeleka leo nikiwa nanyi. Ni wajibu wa kila mmoja kila mahali, na tuianze sasa safari ya ushindi.

Mungu awabariki kwa kunisikiliza.

Chanzo: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23484-sambwee-shitambala.html
 
we unafikiri hata akiiandikiwa si lazima aweke ukomedi wake, pale hmna kitu
 
Huo ni mtazamo wako.
Si lazima uwe sahihi.
Hotuba za Rais kwa mtazamo wangu ni nzuri sana.
 
Mbona hivi vinavyoandikwa humu Politics, Society & Things: What's your solution? katika Blogu ya January Makamba havilingani na hizo hotuba za Rais zinazosemekana kuwa zimeandikwa na huyu Makamba Junior? Kuna tofauti kubwa kati ya mwandishi wa hotuba na mtoa hotuba. Pamoja na hayo yote, watu hupata kiongozi wanayemstahili hivyo wananchi husikiliza hotuba zinazowastahili pia. Tuliamua stahili yetu mwaka 2005. Tutaaamua tena stahili yetu 2010. Zidumu hotuba na fikra stahili!
 
....huu ni mwaka wa tatu tangu JK aingie madarakani .........watu bado mnajadili Rais asaidiwe kuunda hotuba.......!!!
 
Ukiachia mambo ya uanamtandao, urafiki, upenzi, kujuana, nk. katika kupeana kazi, mambo ambayo Rais wetu amejidhihirisha kuwa "sterling", mimi naona Rais kwa kumchagua January Makamba kuwa mwandika hotuba zake, ambazo sasa tunazilalamikia, amefanya makosa mawili tunayoyaita "fallacy of association". Kwanza, amemu"associate" January na baba yake - mzee makamba. Pili, ame"associate" eloquence ya public speech na kuwa writer. Yaani kwa kiingereza wanasema "a great speaker is also a good writer". Haya ni makosa yanayowakumba sana watu wenye uwezo mdogo kiakili wa kuchambua mambo kiundani, yaani "people with limited minds go with associations". Maana unaweza kuwa great public speaker lakini si kwa hoja bali ni kwa vichekesho na burudani. Hivyo hata utakachoandika kitaendana na mind ya ki"comedy". Pili, si lazima kipaji cha baba ndicho kipaji cha mtoto. Unapompa kazi mtu, hasa katika nafasi nyeti, unapaswa kumjua kwa ndani mteule wako, hapo inabidi uende hatua moja mbele kukiruka kihunzi cha "association". Yaani ufanye analysis za ideas za mteule kabla ya kumpa nafasi.


SHARE,
Naona umeamua tu kuchanganya watu kwa wingi wa maneno ya kiingereza.
Hakuna hoja ya msingi uliyomsaidai mtoa mada.

Onyesha basi mchakato mzuri wa kumpata Rais hapa TZ uweje?
 
we unafikiri hata akiiandikiwa si lazima aweke ukomedi wake, pale hmna kitu

Antony,
Kulaumu bila kuonyesha njia ni kusengenya.
Umeandika PALE HAMNA KITU,..........Sasa KITU NI KIPI NA KIKO WAPI?
Kama una hoja, andika hoja sii masengenyo.
 
Rais wetu anajitahidi sana kuoanisha lile analolisema na hatua anazochukua. Sema tu wengi tulishamhukumu hata kabla ya kumsikiliza.


..katika lipi hasa mkuu?, kuahidi kuwa hakuna mwanafunzi wa chuo kikuu atakayekosa elimu kwa kukosa ada..halafu watoto wa maskini wanakosa udahili mlimani? kuwa ataweka kipau mbele kuutatua mgogoro wa Zanzibar..halafu anaenda Pemba na kutoa kauli zenye utata?..orodha ni ndefu!
 
Huyu Rais jamani na hizi hotuba zake! Ni kama Tz hatuna wataalamu wa hotuba kiasi kwamba Rais hajapata mtu wa kumuandikia hotuba za ki-Rais.

Zile za kila mwisho wa mwezi ni kama summary ya matukio. Yeye akaziita hotuba.

Akatoa ile ya half term ikawa imejaa matusi pale alipojidai kutoa michapo. Eti lazima uliwe ndo ule. Tena kwa kurudia-rudia na kucheka. Rais huyo!

Kuna ile nyingine ya siku ya UKIMWI hiyo ndo alitoa mpya. UKIMWI ni wa kujitakia. Mbele ya wananchi wake, wenye ukimwi na wasio na ukimwi. Wakubwa na watoto. Akaendelea na matusi mengine.

Huko Pemba tena ndo kaja na hayo anayodhani ni ushujaa wa kisiasa kwa kutumia maneno kama ya taarabu.

Rais yabidi ashauliwe apate mwandishi wa maana. Aaambiwe asome hotuba na siyo kutoa yake kichwani maana yaonekana uwezo huo hana. Najua ugumu utakuwa ktk kujibu maswali lakini kwa Rais wa Africa ni rahisi kukwepa mahojiano. Tahadhari yaficha aibu.

Mchunguzi, naona kwanza ungejifunza wewe kuandika kiswahili vizuri ukishaelewa ndio utowe nasaha za namna ya Rais kutowa hotuba zake: Somo la kwanza, ni ushauri si ushauli, kama ulivyoandika hapo juu. Somo la pili, ni Afrika sio Africa kama ulivyoandika wewe hapo juu.
 
Haya majitu yanayoponda kila afanyacho Kikwete ndio yale yale au ni mitoto ya yale yale yaliyokuwa yakimponda Mwinyi, tumeyashtukiaa hayoo, hayana lao jambo bali yana agenda za siri zilizokwisha bainika zamani kwa wenye kujuwa maana.

Mtabaki hivyo hivyo na chuki zenu za kibinafsi, mwenzenu anadunda tena kwa mbwembwe za ki-bwagamoyo.
 
Nadhani kuna baadhi ya watetezi wa rais wamekuja hapa kuvuruga hoja hapa. Kama unaona rais huyu anatoa hotuba nzuri it is your right, lakini usianze kupoteza mada, eti mchangiaji hajui kuandika kiswahili vizuri etc.
FMES, ameshamaliza mjadala kwani amesema hotuba hata ni taswira ya mtu anayeitoa hotuba na mawazo yake.
Mjadala ni kuwa rais huyu apewe msaada gani ili asijiaibishe. But there's not much left to do, ni kumwacha kama alivyo. Msisahau hata W. Bush alikuwa na 20 something percent of Americans who still thought he did a good job! Na rais huyu naye ana mashabiki ambao kila mwezi husubiri kwa hamu hotuba yake . Let him preach to his audience, tusiumize vichwa.
 
Nadhani kuna baadhi ya watetezi wa rais wamekuja hapa kuvuruga hoja hapa. Kama unaona rais huyu anatoa hotuba nzuri it is your right, lakini usianze kupoteza mada, eti mchangiaji hajui kuandika kiswahili vizuri etc.
FMES, ameshamaliza mjadala kwani amesema hotuba hata ni taswira ya mtu anayeitoa hotuba na mawazo yake.
Mjadala ni kuwa rais huyu apewe msaada gani ili asijiaibishe. But there's not much left to do, ni kumwacha kama alivyo. Msisahau hata W. Bush alikuwa na 20 something percent of Americans who still thought he did a good job! Na rais huyu naye ana mashabiki ambao kila mwezi husubiri kwa hamu hotuba yake . Let him preach to his audience, tusiumize vichwa.

Haswa, taswira ya JK ni ukweli na uwazi na anaongea, kwenye hotuba zake ukweli mtupu, chuki binafsi zinawafanya mumchukie, kawakosa nini? Rais aliyewajengea mashule mengi kuliko Rais yeyote aliyepita! Rais aliyewafichua mafisadi wa toka enzi za Nyerere! Rais aliye ahidi na kuanzisha chuo kikuu kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki, katika muda usiofikia miaka miwili toka aahidi, Rais anaemalizia mabarabara yaliyowashinda ma Rais wote waliopita, mpaka sasa unaona raha ukienda Mwanza kutokea Dar, huna haja tena ya kupitia Kenya labda uwe na sababu zako za kupita huko, lakini si kuwa barabara ni mbovu. Rais alieweza kwa mara ya kwanza katika Historia kumuweka na kumfadhili Rais wa Merekani kwa siku nne katika Afrika, Looh, bado tu hajui kutoa hotuba? ooopssss, Rais wa kwanza wa Tanzania kuwa Mkulu wa AU,, Rais wa kwanza katika Tanzania alieweza kushusha bei ya mafuta yanayotumika kwenye magari na viwanda, haijawahi kutokea, bado hajui kutoa hotuba tuu? tafuteni jengine sio hili. Looohhh.
 
kwa kawaida hotuba hutokea moyoni mwa mhutubiaji, zile karatasi huwa zinasaidia kumkumbusha mtililiko mambo anayotaka kuhutubia. Sasa kama yaliyoko moyoni mwake ni upupu, hata ukimwandikia karatasi lenye mtililiko mzuri, bado atatoa upupu.

Siku moja huyu Kikwete alitayarishiwa hotuba nzuri kwa kwa ajili ya kikao cha bunge. Kufika pale yeye akatoa upupuambao haukuwa kwenye karatsi na kusababisha proceedings za bunge zicheleweshwe kusudi ikaandikwe hotuba upya.
 
Haya majitu yanayoponda kila afanyacho Kikwete ndio yale yale au ni mitoto .................[snip]

Mtabaki hivyo hivyo na chuki zenu za kibinafsi, mwenzenu anadunda tena kwa mbwembwe za ki-bwagamoyo.

Dar Es Salaam, Mbona unakwepa kutusaidia kufahamu tatizo la Rais wetu na badala yake unaanza ku-edit messages za watu? hapa kuna koma, pale kuna el hapa pawe hivi na unamaliza kwa mtindo wa jinsia ya aina fulani, kwamba ukizozwa wewe unaishia kuzomea.. Hiloooo! Oooo! yebaaa!

JF tunataka Uandike maoni yako kwa mada iliyoko mbele yetu. Hatujasema haleti maendeleo. Hatujasema hajafanya kitu, nk. Tatizo letu ni hotuba na aina ya maneno anayotumia ktk hotuba. Hata kama atatuletea kocha wa mpira kila mkoa kama kitendo cha maendeleo, bado hiyo siyo sababu ya kufurahia hotuba zilizopinda-pinda kwa uzembe wakati uwezekanao wa kuzionyoosha unaonekana.
 
Back
Top Bottom