Rais wetu Asaidiwe kuandaa Hotuba

Rais wetu Asaidiwe kuandaa Hotuba

MchunguZI

Platinum Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,047
Reaction score
2,239
Huyu Rais jamani na hizi hotuba zake! Ni kama Tz hatuna wataalamu wa hotuba kiasi kwamba Rais hajapata mtu wa kumuandikia hotuba za ki-Rais.

Zile za kila mwisho wa mwezi ni kama summary ya matukio. Yeye akaziita hotuba.

Akatoa ile ya half term ikawa imejaa matusi pale alipojidai kutoa michapo. Eti lazima uliwe ndo ule. Tena kwa kurudia-rudia na kucheka. Rais huyo!

Kuna ile nyingine ya siku ya UKIMWI hiyo ndo alitoa mpya. UKIMWI ni wa kujitakia. Mbele ya wananchi wake, wenye ukimwi na wasio na ukimwi. Wakubwa na watoto. Akaendelea na matusi mengine.

Huko Pemba tena ndo kaja na hayo anayodhani ni ushujaa wa kisiasa kwa kutumia maneno kama ya taarabu.

Rais yabidi ashauliwe apate mwandishi wa maana. Aaambiwe asome hotuba na siyo kutoa yake kichwani maana yaonekana uwezo huo hana. Najua ugumu utakuwa ktk kujibu maswali lakini kwa Rais wa Africa ni rahisi kukwepa mahojiano. Tahadhari yaficha aibu.
 
- Mchunguzi, huwezi andika hotuba ambayo ni tofauti na matendo yako na mawazo yako, hivi huoni ya Obama huko US maneno na matendo yalivyo sambamba!
 
- Mchunguzi, huwezi andika hotuba ambayo ni tofauti na mtendo yako na mawazo yako, hivi huoni ya Obama huko US maneno na matendo yalivyo sambamba!

😀 Mkuu FMES, hili jibu ni 100% correct, SAFI SANA!!!!!! hata msomaji wa hiyo hotuba hayo maandishi yatakuja msuta!...
 
Kuna jamaa yangu hapa amekaa sana hapa nchini anasema hivi nyie watanzania mnapata vipi viongozi?

Je, Rais wenu ndo the best among CCM members? sikuweza kumjibu mana mimi sijui CCM inaendeshwa kivipi.
 
- Mchunguzi, huwezi andika hotuba ambayo ni tofauti na matendo yako na mawazo yako, hivi huoni ya Obama huko US maneno na matendo yalivyo sambamba!

haha good point...si mliona hotuba za Bush...they were a reflection ya mtu mwenyewe
 
Nilishaacha kusikiliza hotuba za mwezi za Kikwete muda mrefu. Sikutarajia Rais wangu awe mtangazaji wa kipindi cha matukio "Tanzania mwezi huu" !.
 
Nilishaacha kusikiliza hotuba za mwezi za Kikwete muda mrefu. Sikutarajia Rais wangu awe mtangazaji wa kipindi cha matukio "Tanzania mwezi huu" !.

Whar are we trying to imply? kwamba Rais wa Tanzania amepatikana by default na si merits yani si presidential material? hana uwezo wa kuchanganua mambo au mvivu wa kuchambua hotuba anazoletewa mezani? amezungukwa na waandishi wa hotuba wasio na 'upeo' wa kuandika hotuba? Kwani hili mtu awe muandishi wa habari wa rais anatakiwa awe na elimu ya aina gani au awe na CV ya namna gani? my take ni kwamba rais anatakiwa asilimia 50 achangie katika kutengeneza hotuba
 
Kuna jamaa yangu hapa amekaa sana hapa nchini anasema hivi nyie watanzania mnapata vipi viongozi?

Je, Rais wenu ndo the best among CCM members? sikuweza kumjibu mana mimi sijui CCM inaendeshwa kivipi.

Best kwa maana gani?

Yawezekana sii mla rushwa..na then ktk CCM is the best!

Mkapa alikuwa na hotuba safi sana..ila he was not clean!
 
hivi mnataka aeleze nini.msaidieni au mundikieni kwenye web site yake kumueleza mnayopenda kusikiliza.pengine mumezoea porojo
 
hivi mnataka aeleze nini.msaidieni au mundikieni kwenye web site yake kumueleza mnayopenda kusikiliza.pengine mumezoea porojo

Hatukuzoea porojo ndiyo maana tunaona kuna kasoro kubwa kwenye hotuba zake. Hivi tangu aingie madarakani amefanya nini kuhusiana na sera zake alizozipigia debe wakati wa kampeni?
 
hivi mnataka aeleze nini.msaidieni au mundikieni kwenye web site yake kumueleza mnayopenda kusikiliza.pengine mumezoea porojo

Eeee! nawe kazi unayo. Kuna porojo zaidi ya matusi anayozungumza mbele ya kamera za TV akisema analihutubia taifa? Katika kipindi cha hii takriban miaka 3, waweza kunyofoa chochote tukiite 'words of wisdom' toka ktk hizo zinazoitwa hotuba?

Naona ukweli kwamba Hizi hotuba zilingane na matendo yake. 🙂
Ila tu nilidhani hata kama tuna serikali kama ya Hitler, lazima wimbo wa Taifa letu uwe wa kuwatakia watu pamoja na Taifa mambo mema.

Sasa ukiwa hivyo hivyo na hotuba zako zikawa za hivyo hivyo. Kweli inabidi hata ukiitoa Bungeni, bora ipotee ktk kumbukumbu.
 
Whar are we trying to imply? kwamba Rais wa Tanzania amepatikana by default na si merits yani si presidential material? hana uwezo wa kuchanganua mambo au mvivu wa kuchambua hotuba anazoletewa mezani? amezungukwa na waandishi wa hotuba wasio na 'upeo' wa kuandika hotuba? Kwani hili mtu awe muandishi wa habari wa rais anatakiwa awe na elimu ya aina gani au awe na CV ya namna gani? my take ni kwamba rais anatakiwa asilimia 50 achangie katika kutengeneza hotuba

Yote uliyoyasema yawezakuwa sababu. Tathmini ya hotuba zake ni hiyo matukio "Tanzania mwezi huu".!
 
Kuna jamaa yangu hapa amekaa sana hapa nchini anasema hivi nyie watanzania mnapata vipi viongozi?

Je, Rais wenu ndo the best among CCM members? sikuweza kumjibu mana mimi sijui CCM inaendeshwa kivipi.

We kweli kichwangumu sasa kwanini hukuwambia sisi huwa hatufanyi uchaguzi yaani National Election ila tunafanya Selection. Hivyo ndivyo tunavyo wapata viongozi wetu. Kazi kweli kweli
 
I don't care about whether speech reflect who you are or not!

Mimi nahitaji mkuu wa nchi anayewafanya watanzania wafanye kazi; anayeweza kuwaondoa watanzania kwenye ugonjwa wa siasa kila mahali hata pale ambapo si muhimu siasa iwepo...

Sipendi kiongozi yeyote yule anayejinadi kwamba atawaletea wananchi maendeleo... Nahitaji kiongozi anayewaambia wananchi tangu kwenye uchaguzi kwamba nitawaongoza mujiletee maendeleo...

Kwa sababu tukiongoze kufanya kazi kwa 20% tu... effect kwenye uchumi inaweza kuwa 50%

Kitendo cha kujadili hotuba za Rais badala ya kujadili kipi kimefanyika na kipi hakijafanyika.... ni muendelezo wa ugonjwa wetu wa muda mrefu wa kuweka siasa mbele.

Leo nilibahatika kuona gazeti moja la kiingereza linalotoka kila jumapili amini usiamini zaidi ya 40% ya contents ilikuwa EPA, na Oboma... sasa hapo nchi itaendelea vipi... Hakuna habari za Kilimo, Miundombinu, Ufugaji, Uvuvi etc.

Sifa ya Rais gani anaingia madarakani inatokana na rai wanahitaji nini wakati gani? Mfano... Mkapa aliingia kwa wakati muafaka...

Na kulingana na ya utawala wa Mkapa, alihitaji Kikwete... hayo mambo yenu ya EPA baada ya muda mutaona hayana maana, mutatafuta Rais wa Kukuza uchumi...ndio evolution ya Taifa... Hakuna Rais hata awe vipi ataweza kujibu hoja za miaka 15 mfululizo... Kawaida ukiingia madarakani kuna unayoleta mazuri alafu kutakuwa na ambayo umeyarudisha nyuma....
 
Juzi nilisoma mahali fulani kwamba mwandishi wa hotuba wa Rais ni January Makamba. Kama kuna mtu ana taariafa kamili basi naomba atupe ili tujue. Hapa Bongo wakati mwingine tunateua watu kujaza nafasi tu na si kuangalia uwezo wao.
 
Hotuba nzuri yenye maneno mazuri inasaidia nini kama matendo yenyewe ovyo? Naona rais yuko honest, hotuba zake n vitendo vyake vinaendana.
 
mwandishi wa hotuba wa Rais ni January Makamba. Kama kuna mtu ana taariafa kamili basi naomba atupe.

"Taarifa kamili" iambatane na CV ya mtajwa itakayojumuisha kiwango chake cha elimu.
 
Best kwa maana gani?

Yawezekana sii mla rushwa..na then ktk CCM is the best!

Mkapa alikuwa na hotuba safi sana..ila he was not clean!

hivi bora yupi, mla rushwa mambo nchi yaende,aonekane muelewa wa kuchambua mambo,aweze kumiliki nchi, au ambaye si mla rushwa mambo hayaendi, siri za nchi zinavuja ovyo, na kichwani mtupu kama mtoto wa darasa la pili?
 
Hiyo ni mada nyingine. Anzisha thread ukitaka. Sasa hivi tayari tunaye Rais mmoja, na hotuba zake ndiyo hizo "hazikidhi haja". Tunachambua tatizo liko wapi, kuanzia yeye mwenyewe mpaka waandaaji wake.
 
Back
Top Bottom