mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,502
- 257
Mnyonge nyongeni lakini haki yake mpeni....
Kuna kipindi watu wamekua wakilaumu serikali kwa mambo mbalimbali. Na lawama zinapotoka muhusika wa kwanza anakuwa Mh raisi. Lakini pamoja na lawama zote yapo mambo mema sana ambayo Mh Raisi anafanya ambayo ni mazuri na yanayoonyesha upendo wake kwa Watanzania na Uzalendo wake.
Mathalani katika siasa za vyama vingi kumekuwa na tabia ya watendaji mbalimbali wa chama tawala kuwasusia au kuwatenga viongozi wa upinzani katika mambo mabalimbali. mfano bungeni wapinzani wanaweza kuja na hoja nzuri lakini wabunge wa chama tawala wakaikataa kwa sababu tu ni kutoka upinzani. Wakati mwingi wamekua wakiwazomea wapinzani hata katika mambo ya msingi.
Si hilo tu mfano baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wamekua wakiwatenga watendaji au viongozi wa upinzani katika mambo ya kitaifa. Raisi wetu amekuwa tofauti na wote hao ameonyesha ukomavu kisiasa, ameonyesha uzalendo halisi, ameonyesha ni mtu anawapenda watanzania wote. Na hili limezibitishwa katika mambo mbalimbali. Mfano CDM walipoleta mawazo ya kuwa na katiba mpya bungeni walipingwa sana kuanzia bungeni, Waziri wa sheria na hata mwanasheria mkuu.
Lakini kwa busara zake na uzalendo wake raisi wetu aliwaita CDM ikulu na kuongea nao na kuwasikiliza...Matunda yake tunayaona sasa. Pia raisi amekua akiwatambulisha viongozi wa chadema hasa wabunge katika ziarambalimbali za kitaifa bila kinyongo kitu ambacho wenzake wamekuwa hawakifurahii kama alivyofanya Jijini Mwanza hivi karibuni kuwatambulisha wabunge wa chadema wakati mtendaji wake aliacha kuwatambulisha.
HONGERA RAISI WANGU>>>KEEP IT UP....Mungu aendelee kukupa moyo huo ili Tanzania izidi kuwa na amani.