Rais wa zanzibar aapishwa kuudhuria vikao vya baraza la mawaziri Ikulu DSM leo

Zanzibar ni nchi "ndani" ya Jamhuri ya Muungano so kwa kweli siyo nchi. Na yeye siyo Rais wa Zanzibar (hakuna cheo hicho) ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Is it Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Rais wa Serikali ya umoja wa kitaifa? May be wanasheria wafafanue zaidi. Utata kweli.
 
Tundu lissu akionge kuhusu mambo ya zanzibar wanadai mchochezi,leo wazanzibar wanajionea wenyewe raisi kuapishwa kuudhuria baraza la mawaziri ndo nimesikia tanzania ila kuna siku wataelewa tu jinsi katiba ilivyo mbovu.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi,Dr. Ali Mohamed Shein ameapishwa ikulu DSM leo na Jaji Mkuu Othman Chande,Mbele ya Rais Jakaya Kikwete,Waziri mkuu na mawaziri wengine ili aweze kuhudhuria vikao vya baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano.

Huu ni udhaifu wa wazi wa katiba ya JMT na SMZ kwa Rais kuapa kama waziri huku akiwakilisha nchi ya Zanzibar.

Hapa kuna utata mkubwa sana. Kwa nini Seif Sharrif hakuapishwa?. Maana ya Makamu wa kwanza wa rais ni kwamba likitokea jambo la kumfanya rais ashindwe kuendelea na majukumu yake kama kifo au ugonjwa nafasi hiyo inachukuliwa na makamu wake. Ili makamu wake awe na tayari kwa kazi hiyo anatakiwa kuwa na access zote za taarifa anazokuwa nazo rais. Kwa Shein kuingia katika baraza la mawaziri wa JMT bila makamu wake wa kwanza ni dhahiri kuna mushkeli katika katiba na inavyoonekana nchi inaongozwa kama club isiyokuwa na katiba, siku wanachama wakiamua wanafanya watakavyo provided miongoni mwao wamekubaliana ( I mean hapa ni CCM).

Halafu tuliambiwa mchakato wa katiba unaanza October mbona kimya?, wapinzani nao kama wamelala vile. Hakuna cha maana kitakachofanyika katika demokrasia ya Tanzania bila kuwa na unified voice kutoka kwa wapinzani kudai katiba mpya. Nchi nyingi zimepata katiba mpya baada ya misukosuko ya kiuongozi kama vurugu baada ya uchaguzi au mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. CCM isitake Tanzania ipitie hatua hizo ambazo kila mtu anaomba isitokee, wakubali kurudisha uhuru waliopora kwa wananchi wenyewe. Delay tactic huwa hai-solve tatizo bali ni kulifanya liwe complex zaidi inapokuwa hakuna jinsi zaidi ya kuli-solve. Kuapishwa kwa shein tena na jaji mkuu badala ya Rais wa JMT kama member wa baraza la mawaziri inaonesha kuwa there is lacuna in our constitution.
 
mkuu katiba ya zanzibar ilivotungwa maalim seif yupo kama pambo tu kwasababu raisi kama hayupo au hakifariki nchi anakabiziwa makamu wa pili wa raisi na sio wa kwanza.
 
Huyo "Rais" wa ZNZ anapohudhulia vikao vya baraza la mawaziri wa JMT anakuwa sawa
na Waziri asiyekuwa na wizara maalumu. Huu ni mkanganyiko wa KATIBA. Tundu Lissu
alijaribu kulisema hili bungeni surprisingly hata wabunge kutoka ZNZ wakampinga. Sasa
ngoja tuwadhalilishe, huyo Rais wenu huku Bara ni sawa na waziri asiyekuwa na
wizara maaulum what a shame to Zanzibaris! Hata Nahodha (waziri wa mambo ya ndani)
yuko juu zaidi ya Shein kwenye baraza la mawaziri.
 
mkuu katiba ya zanzibar ilivotungwa maalim seif yupo kama pambo tu kwasababu raisi kama hayupo au hakifariki nchi anakabiziwa makamu wa pili wa raisi na sio wa kwanza.

Kwa nini wanamruka?
 
Inamaana tangu awe rais wa znz hajawahi kuhudhuria vikao hivyo au alikuwa anahudhuria bila ya kuapishwa? Hiyo ndio tz ya kikwete bwana, duuh!

Alikuwa anasubiri wakuu wa mikoa wenziye wateuliwe na kuapishwa ili yeye nae aapishwe(Zanzibar kiukweli ni mkoa tu)
 
wazanzibar kwa hili wanakaa kimya as if hakuna kilichotea,nao wote ni hamnazo tu
 
..wa-Zenj walilazimisha aapishwe na Jaji Mkuu.

..nadhani kuna thread nilianzisha humu kuuliza kulikoni Dr.Shein haonekani kwenye vikao vya baraza la mawaziri wa muungano?

..inawezekana sasa hivi Zanzibar wana shida ndiyo maana Dr.Shein kaamua "kujisalimisha" ili waweze kukomba misaada toka Tanzania Bara.
 
Kuna nini hadi kaamua kuja kuhudhuria kikao na kuapishwa ili aingie huko ?Imekuwaje mtoa hoja hebu tupe maneno
Kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa Zanzibar is no body ndani ya serikali ya muungano, hata akija huku hivyo vingora na escort ni heshima tuu lakini sio kwa mujibu wa protokali.

Ili kuilinda hadhi ya rais wa Zanzibar nae aonekana mtu katika serikali ya muungano, ameteuliwa kuwa Waziri, asiye na wizara maalum. Uteuzi huo umefanywa kimya kimya kuilinda hadhi ya rais huyo. Hivyo huko kuapishwa alikoapishwa leo, ni ili auchukue huo uwaziri usio na wizara maalum ili angalau aingie kwenye vikao vya cabinet vinavyojadili mustakali wa taifa letu.

Kiukweli this is wrong, kama ni kweli Tanzania ni muungano wa nchi mbili zenye haki sawa, lakini serikali ya JMT ndio hiyo hiyo serikali ya bara, ilitakiwa representation ya Zanzibar kwenye JMT iwe 50% 50%.

Hata rais wetu anapokwenda Zanzibar, anakuwa chini ya rais wa Zanzibar pia nimakosa, JMT ndio iko juu ya kila kitu, SMZ iko chini ya JMT iweje rais wa JMT awe chini ya rais wa SMZ huko Zanzibar?.

Muungano una matatizo ya msingi kwenye structure, kila siku tunatibu cosmetics tuu yale ya msingi tunayaacha, siku ya siku, msingi utapata ufa na nyumba inaweza kuanguka.
 
Ili kuilinda hadhi ya rais wa Zanzibar nae aonekana mtu katika serikali ya muungano, ameteuliwa kuwa Waziri, asiye na wizara maalum. Uteuzi huo umefanywa kimya kimya kuilinda hadhi ya rais huyo. Hivyo huko kuapishwa alikoapishwa leo, ni ili auchukue huo uwaziri usio na wizara maalum ili angalau aingie kwenye vikao vya cabinet vinavyojadili mustakali wa taifa letu.

Kwa hiyo pia analipwa mshahara kuwa waziri asiye na wizara maalumu?
 
Mapungufu haya ya Kikatiba ni kwsababu CCM imekua inachukulia mambo muhimu na nyeti ya nchi kama mambo binafsi ya chama badala ya wananchi wote. Kuna matatizo mengi lakini mtu unashangaa mwanasheria mkuu ambaye pia ni jaji anasema hakuna tatizo.
 
Back
Top Bottom