Rais wa zanzibar aapishwa kuudhuria vikao vya baraza la mawaziri Ikulu DSM leo

Jombi Jombii

Senior Member
Jun 4, 2011
185
10
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi,Dr. Ali Mohamed Shein ameapishwa ikulu DSM leo na Jaji Mkuu Othman Chande,Mbele ya Rais Jakaya Kikwete,Waziri mkuu na mawaziri wengine ili aweze kuhudhuria vikao vya baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano.

Huu ni udhaifu wa wazi wa katiba ya JMT na SMZ kwa Rais kuapa kama waziri huku akiwakilisha nchi ya Zanzibar.
 
Jamani wanasheria: Hebu tujuzeni iwapo shughuli hii iliyofanyika Ikulu haipingani na Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
 
Halafu huyu Shein -- urais wake ni illegitimate kabisa, Ashukuru kwamba kaungana na CUF kuunda serikali ya pamoja hivyo hakuna chama kikuu cha kumpeleka mahakamani.

Aligombea urais wakati hakuwa kabisa na sifa ya kugombea kwani sifa mojawapo ya kugombea urais Zanzibar kufuatana na Katiba ya huko ni kwamba lazima awe amejiandikisha kupiga kura katika daftari la kule, kitu ambacho hakukifanya kwa sababau alijiandikisha huku Bara wakati akiwa VP.

Hili lilizungumzwa katika vikao vya NEC na Nimrod Mkono, lakini akina JK wakalipunch, sijui kwa vigezo gani.
 
Naona ile PhD ya sheria inaanza kufanya kazi - or not! Katiba ya Zanzibar baaday ya kufanyiwa marekebisho ya kuruhusu uwepo wa serikali ya umoja wa kitaifa inaruhusu Rais wa Zanzibar awe kwenye baraza la mawaziri kwenye JMT?
 
Na kwa Katiba ya JMT kuruhusu rais wa Zanzibar chini ya Serikali ya Pamoja kuwa katika Baraza la Mawaziri la Muungano?
 
Inamaana tangu awe rais wa znz hajawahi kuhudhuria vikao hivyo au alikuwa anahudhuria bila ya kuapishwa? Hiyo ndio tz ya kikwete bwana, duuh!
 
This implies that serikali ya mapinduzi ya zanzibar kiutawala ni equivalent na wizara moja tu e.g wizara ya mali asili na utalii na rais wa zanzibar ni kama waziri wa wizara hiyo.
 
kama makosa yalifanyika na sasa yamerekebishwa hakuna tabu,hata obama alikosea kuapa!nilidhani wanasheria wetu ni mbumbumbu kwenye mikataba tu kumbe hata kwenye katiba wanaharibu.lakini naondoa hofu baada ya kumpata Dr mpya wa sheria(jk)
 
Zanzibar ni nchi tukiwa ndani ya mipaka
zanzibar si nchi tukiwa nje ya mipaka ya jmt ni mkoa,so rais wao ni km waziri au mkuu wa mkoa
 
Kuna nini hadi kaamua kuja kuhudhuria kikao na kuapishwa ili aingie huko ?Imekuwaje mtoa hoja hebu tupe maneno
 
Kweli hujuhi Karume mtoto na Salmin hawajawahi kuhudhuri hata siku moja kwa kuwa walikata kuapishwa, kwani ni kujidhalilisha.

Sasa kama huo si unafiki ni nini hasa? kama walikuwa na jeuri mbona hawakuvunja muungano ili wasijidhalilishe kuwa maraisi chini ya Rais. Heri ya huyu aliyepata hekima ya kukubali kuapishwa ingwa ni baada ya mwaka kupita.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi,Dr. Ali Mohamed Shein ameapishwa ikulu DSM leo na Jaji Mkuu Othman Chande,Mbele ya Rais Jakaya Kikwete,Waziri mkuu na mawaziri wengine ili aweze kuhudhuria vikao vya baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano.

Huu ni udhaifu wa wazi wa katiba ya JMT na SMZ kwa Rais kuapa kama waziri huku akiwakilisha nchi ya Zanzibar.
Kwa hiyo SMZ ni kama wizara mojawapo tu ndani ya JMT?
 
CCM ni janga la kitaifa na inavyoelekea CCM Bara na CCM znz ni vyama viwili tofauti kwani wanaogopana na kila kimoja kinajifanyia kinavyopenda.Dr Shein Aliapa kinyonge san mpaka nikamhurumia.

Sasa kama huo si unafiki ni nini hasa? kama walikuwa na jeuri mbona hawakuvunja muungano ili wasijidhalilishe kuwa maraisi chini ya Rais. Heri ya huyu aliyepata hekima ya kukubali kuapishwa ingwa ni baada ya mwaka kupita.
 
Mzee wa Katavi aliposema kwa mujibu wa Katiba ya JMT, Z'Bar si Nchi, wenye "nchi" yao wakapanda munkari wakidai wamedhalilishwa. Saasa, mkuu wa kaya yao anaapishwa na Jaji Mkuu (tena wa Bara) ili ahudhurie vikao vya baraza la mawaziri; Je bado Zenji ni NCHI?????
 
Back
Top Bottom