Rais wa Zambia, Hichilema aalikwa Ikulu ya Marekani

My friend, wenyeji wanatafuta mbinu ya kutimua mshindani wao kiuchumi (China) kutoka kwenye himaya ya mgeni wao. Uangalie mwaliko huu kwa jina la Tatu utagundua hili na mengine. Najua, tukio la Kashoggi wa Arabia bado unalikumbuka. Kwa ufupi tu Arabia haikufungiwa/wekewa vikwazo. Jibu unalo la kwa nini hawakuwekewa vikwazo mbali na ushahidi usiotiliwa shaka kuwa Arabia ilihusika moja kwa moja.
Endeleeni kupanua magoli
 
Ukipata uongozi kwa njia ya Haki kila mtu atakuheshimu , utaalikwa na kila mwenye akili timamu na hasa kama Utawasamehe wote waliokufanyia unyama , huku ukisisitiza Demokrasia ya kweli kwenye Nchi yako hata Mungu atakulinda .

Wakati wengine wakipambana kwa njia za Panya ikiwemo kuloga ili kuingia Ikulu ya Marekani , Haikainde Hichilema yeye ametafutwa na Ikulu yenyewe ya Marekani . Hili ni fundisho kubwa sana kwa waafrika

Hii itasaidia chadema kushinda uchaguzi

USSR
 
Waafrika huwa tunakuwa na haraka sana kuwasifia wanasiasa. Huyu jamaa wapinzani wake wakianza kumpa pressure tu, atabadilika mtasahau kama ni yeye.

Tuna matatizo mengi, tuna hamu sana atokee masiha wa matatizo yetu yote. Bahati mbaya ni kwamba siasa zetu, utu wetu, imani zetu, ufahamu wetu, historia yetu vyote hivyo vimevurugika kiasi kwamba siasa zetu haziwezi kutusaidia sana.
 
Tatizo ilikuwa kiingereza si unajua kujiamini lazima ngeli ipande. Lakini utawasikia mataga wanadai alikuwa anabana matumizi. Kama alikuwa anabana matumizi angeiba rambirambi, angeiba matrillion hazina na angejenga international Airport porini?

Ni kingereza tu kilimfanya aogope 'to rub shoulders with elite'.

Magonjwa Mtambuka
Kaa kimya wewe, acha kupiga kelele zako hapa.
 
Naongelea heshima ya Nchi

Mwinyi ndiye Rais aliyepewa pesa nyingi sana za misaada na mikopo ya Bei nafuu na WB na IMF
Mwinyi ndie rais aliyedharauliwa na wazungu kuliko Marais wote labda nikupangie kuanzia wa kwanza mpaka wa mwisho na namna wazungu walivyomuona.

Nyerere aliheshimiwa Sana.
Mwinyi alidharauliwa.
Mkapa alipendwa na aliheshimiwa.
Magufuli alichukiwa Sana.
Samia hawamuelewi bado.

Unaswali niulize.
 
Huu ni Ndio ukweli wenyewe na huyu Rais yupo very negative na investment za wachina nchini kwake na hii ni kutokana na conditions zake....
Ila mabeberu ni walewale...
Bora Wazungu kuliko Wachina
 
Ukipata uongozi kwa njia ya Haki kila mtu atakuheshimu, utaalikwa na kila mwenye akili timamu na hasa kama Utawasamehe wote waliokufanyia unyama, huku ukisisitiza Demokrasia ya kweli kwenye Nchi yako hata Mungu atakulinda.

Wakati wengine wakipambana kwa njia za Panya ikiwemo kuloga ili kuingia Ikulu ya Marekani, Haikainde Hichilema yeye ametafutwa na Ikulu yenyewe ya Marekani. Hili ni fundisho kubwa sana kwa waafrika

Mungu wabariki wazambia
 
Dah!
Huu ss sijui tuuite ni ushamba au ulimbukeni!
Hivi kuitwa na ikulu ya Marekani mafanikio ya nchi ?
Hiz ni akili za kitumwa kabisa!!!
Lakini mkipewa kondom za msaada mnawaita wafadhili..
 
Back
Top Bottom