Donald Trump: Vitu 8 ambavyo hakuvijua kuhusu rais huyo wa zamani wa Marekani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Donald Trump
5 Oktoba 2022
Kuna vitu vya ajabu ambavyo vimejitokeza kuhusu rais huyo wa zamani kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Confidence Man cha Maggie Haberman kilichozinduliwa siku ya Jumanne.
Kitabu hicho kinaangazia muda wa Donald Trump kutoka kuwa mfanyabiashara mjini New York hadi kuwa rais na zaidi.
Mwandishi wa kitabu hicho alizungumza na takriban watu 200, ikiwemo washauri wa rais huyo wa zamani wa Marekani.
Mbali na mahojiano hayo pia yeye mwenyewe amefanikiwa kumhoji rais Trumpo mara tatu.
Kwa upande wake rais Donald Trump amemshutumu Haberman , katika mitandao ya kijamii akidai kwamba kitabu hicho kinamiliki habari feki ambazo hazijathibitishwa.
Kuna mambo manane katika kitabu hicho ambayo yameangaziwa na mwandishi.

1. Trump alitaka kuwafuta kazi mwanawe Ivanka na mumewe Jared Kushner​

Haberman ansema kwamba rais Donald Trump alitaka kutuma ujumbe katika mtandao wa twitter kwamba mwanawe wa kike na mume wake jared Kushner walikuwa wanajiuzulu kutoka katika nyadhfa zao katika Ikulu ya Whitehouse.
Inadaiwa kwamba Mkuu wa wafanyakazi wa umma John Kelly aliyemzuia na kumshauri kwamba alipaswa kuwaambia kuhusu hatua hiyo kabla ya kutuma ujumbe huo.
Donald Trump hakuzungumza na mwanawe wala na mumewe mwanawe kuhusu hilo na wote walisalia kuwa washauri wa rais Trump kipindi chote alichohudumu kama rais.
KItabu hicho kinasema kwamba baada ya kusikiliza hotuba iliotolewa na jared Kushner, Donald Trump alisema kwamba anazungumza kama mtoto.
Hatahivyo rais Trump amekana kwamba alitaka kuwafuta kazi wanawe hao na kuonezea kwa wazo kama hilo halikumjia katika fikra zake.
.

CHANZO CHA PICHA,REUTERS
Maelezo ya picha,
Jared Kushner na mkewe Ivanka

2- Alitaka kulipua kambi za dawa za kulevya nchini Mexico​

Haberman anaendelea katika kkitabu chake kwamba rais Donald Trump pia alitaka kulipua maeneo ambayo dawa za kulevya hutengenezwa nchini Mexico.
Alilalamika kuhusu suala hilo mara kadhaa. Pendekezo hilo hahativyo lilimshangaza aliytekuwa Waziri wa Ulinzi wakati huo Mark Esper.
Wazo hilo lilitokana na mazungumzo yaliofanyika kati ya Trump na afisa wa afya ya umma Brett Giroir.

3- Trump aliogopa kufariki kutokana na maambukizi ya corona​

Trump aliambukizwa maradhi ya Corona mnamo mwezi October 2020. Hali yake ya kiafya ilikuwa imedorora katika Ikulu ya Whitehouse na alikuwa anaogopa kwamba angefariki kutokana na maradhi hayo.
Ni wakati huo ambapo naibu afisa mkuu wa wafanyakazi wa umma Tony Ornato alimuonya rais Trump kwamba angelazimika kuweka mikakati ya serikali kuemdelea kufanya kazi iwapo hali yake ingedhoofika zaidi.
Trump mara kwa mara alipuuzilia mbali ugonjwa huo , licha ya kwamba alikuwa akiuogopa na kwamba alikuwa ana wasiwasi kwamba ungemuharibia sifa zake.
Kulingana na mwandishi Haberman, Donald Trump alikuwa amewataka washirika wake kutovaa barakoa. Mbali na hilo , alimtaka gavana wa jimbo la New York Andrew Cuomo kutozungumza kuhusu corona katika runinga.

4- Alizungumza kuhusu utajiri wake na Waziri mkuu wa Uingereza​

.

CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Trump na aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
Iliandikwa katika kitabu hicho kwamba katika mkutano wa kwanza na aliyekuwa Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May , Donald Trump alizunguza kuhusu masuala mengi.
AKizungumza kuhusu uavyaji mimba , Trump alisema, watu wengi wanapendelea maisha na wengine wanaunga mkono chaguo la mtu.
Fikiria kuhusu mwanamume mwenye tatoo akimbaka mtoto wako ahalfu apate ujauzito.
Baada ya hilo, Trump alibadili mazungumzo na kuanza kuangazia Irelanda kaskazini ambapo alizungumzia kuhusu mradi wa upepo ambao unaweza kuzuiwa kujengwa karibu na mali yake.

5- Kujaribu kubadilisha matokeo ya Uchaguzi mkuu wa 2020​

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Maandamano katika bunge la Marekani
Wakati ilipobainika kwamba rais Trump alikuwa anapoteza kura ya urais, alimpigia simu Rudy Giuliani , meya wa zamani wa New York ambaye pia ni wakili wake wa kibinafsi.
Kulingana na kitabu hicho , Trum alisema kupitia njia ya simu kwamba , Sawa Rudy….wewe ndio unayesimamia…fanya unachoweza kufanya, sijali.
Trump alisema haya wakati mawakili wake walikuwa hawako tayari kushirikiana naye kuhusu kile ambacho Trump alitaka kufanya.
Trump aliwataja mawakili wake kuwa wabaya. Wakati huo huo, mara nyingi alimkemea wakili wa Ikulu Pat Cipollone.

6- Kukataa kutoa ufafanuzi kuhusu rekodi zake za ulipaji kodi​

.

CHANZO CHA PICHA,US DEPT OF JUSTICE
Maelezo ya picha,
Trump alikataa kutoa ufafanuzi kuhusu ulipaji wake wa kodi
Akiwa katika kampeni mwaka wa 2016, Donald Trump aliombwa na meneja wake wa kampeni Corey Lewandowski na katibu wa waandishi wa habari Hope Hicks kufafanua juu ya ripoti zao za ushuru kwa sababu walidhani suala hilo linaweza kuwapatia kazi ngumu wakat iwa uchaguzi
Haberman anaandika katika kitabu chake kwamba alipokuwa kwenye ndege, Trump aligundua ghafla kwamba malipo yake ya kodi yalikuwa yanakaguliwa.
"Inaweza kusemwa kwamba nitatoa hati zangu za ushuru iwapo sitakaguliwa, na hiyo haitatokea kamwe," alisema.
Hata hivyo, kila rais wa Marekani tangu kutoka uongozi wa Rais Richard Nixon ametoa kodi yake mwenyewe.
Mnamo 2020, uchunguzi wa New York Times ulionyesha kuwa Trump alilipa $ 750 tu katika ushuru wa mapato ya kati mwaka ambao alikua rais.

7.Alitupa nyaraka kwenye choo cha Ikulu ya White House​

Donald Trump alipokuwa katika Ikulu ya White House, wafanyikazi waligundua kuwa choo hicho kilikuwa kimejaa karatasi zilizochapishwa. Inaaminika kwamba alizitupa nyaraka hio chooni.
Pia inadaiwa alirarua nyaraka zinazokiuka Sheria ya Rekodi za Rais. Hati zilizotengenezwa au kupokewa na Rais chini ya sheria hii ni mali ya serikali ya Marekani
Hifadhi ya Taifa ya Marekani pia ilisema hati hizo hazikuwepo, wakati Trump anakabiliwa na uchunguzi wa kuhifadhi nyaraka za serikali katika nyumba yake ya Florida baada ya kuacha urais.

8- Aliwachukulia wafanyakazi wa umma kama wahudumu wa mikawa​

Wakati wa mkutano baada ya kuwa rais, Donald Trump alikutana na wafanyakazi wa viongozi wa chama cha Democratic, ambapo kulikuwa na watu kutoka makundi tofauti ya rangi. Trump aliwakosea kuwa wahudumu wa mikahawa.
Kulingana na kitabu hicho, alitoa matamshi haya kwa wafanyikazi wa Seneta Chuck Schumer na Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi. chanzo.BBC
 
Back
Top Bottom