Hizi kwangu mimi naziona kama ghiliba,kama kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa!
Kutuita watanzania wanyonge watanzania masikini ni kutukejeli! Watanzania sio wanyonge bali ni wavumilivu na watu tunaoheshimiana.
Tunakutaka usituite wanyonge,huku ukitubomolea makazi yetu tena kwa kukiuka agizo la mahakama.
Unatuita wanyonge huku ukikataa kutuletea katiba mpya itakayo wawajibisha wapindisha haki na mafisadi wote wa serikali yako!
Unatuita wanyonge huku ukituingiza kwenye hasara kubwa kwa kukiuka naagizo ya mahakama.
Unatuita wanyonge huku ukitupiga danadana kuwaongeza mshahara wafanyakazi
Unatuita wanyonge huku ukiruhusu makampuni yapoteze ajira kwa watu wako kwa kushindwa kujiendesha
Hili jina la Watanzania wanyonge tunaona linatumika kujinufaisha kwa baadhi ya viongozi kujiona miungu watu. Tunaomba likome
NDIO MIMI NI MBOVU WA MGUU LAKINI SIKO TAYARI KUITWA KILEMA