Rais wa wanyonge, wanyonge wapi?

Rais wa wanyonge, wanyonge wapi?

Halafu watu wengine bhana sijui mkoje,
Ina maana mkuu wanyonge huwajui wewe au unachezea akili zetu,
Mnyonge Gambo humjui au?
Mnyonge bashite humjui pia? Hebu acha hizo
Yule mnyonge Dotto James humjui pia?
Ina maana hujawahi kabisa kujua wale ndo wanyonge aliowasema rais?
Hizo habari zenu za pembejeo nyie kalimieni meno pumbafu zenu
Sisi kipaumbele chetu sio ninyi ni chato kwanza
Tunataka chato iwe kama dubai watu watoke los angels na Miam kuja kushangaa chato ilivyojengeka

uje sentro mwenyew
 
Hao waliokosa mkopo waendelee kukaa tu nyumbani hivyohivyo wasijiongeze kwa lolote
Kuna watu lukuki wana vyeti wamerudi mtaani wanatoka kwa fursa nyingine kumbe wao wamekaa tu
Baada ya kuona Joverest kang'aa basi ukaona uchukue picha yake kbsa. Umaarufu hauji kwa picha ya ID ya mtu.
Hongera naona unajitahidi km mhusika mwenyewe. mhusika ana verified user na feki hana. Hapo ndiyo ujue kutofautisha ktk ya original na feki.
Ila nachukia sana kuona watu wanaiga watu wengine. Try to be unique.
 
Unajua taifa linapata laana kwa sababu kila siku tunatamka madhaifu tu na kijitabilia udhaifu na tunaona kama ni sifa kumbe twajitabilia laana au kushindwa.

Katika maandiko Mungu alichukia sadaka ya Kaini kwa sababu alitoa vitu vinyonge kama sadaka mbele ya Mungu na akaadhibiwa na kuwa mtumwa wa ndugu yakr mpka leo.

Sasa ccm kuwafanya watanzania wanyonge na kijinasibu kuwa kiongozi wa wanyonge wenye akili washajua tutakuwa watumwa wa ccm mpka mwisho wa dahari.

Mungu hakutuumba Watanzania tuwe wanyonge tena ndani ya ardhi yetu ila tunafanywa wanyonge na serikali iliyo madarakani. Ivi kuwa mnyonge ni sifa? Na kwanini tuwe dhaifu na wanyonge kama hatusababishiwi kuwa ivyo?

Kuanzia leo tukatae kuitwa wanyonge/dhaifu hii laana ya kufanywa watumwa wa watu fulani ikome na tumwambie hatutaki kuitwa dhaifu
 
Hizi kwangu mimi naziona kama ghiliba,kama kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa!

Kutuita watanzania wanyonge watanzania masikini ni kutukejeli! Watanzania sio wanyonge bali ni wavumilivu na watu tunaoheshimiana.

Tunakutaka usituite wanyonge,huku ukitubomolea makazi yetu tena kwa kukiuka agizo la mahakama.

Unatuita wanyonge huku ukikataa kutuletea katiba mpya itakayo wawajibisha wapindisha haki na mafisadi wote wa serikali yako!

Unatuita wanyonge huku ukituingiza kwenye hasara kubwa kwa kukiuka naagizo ya mahakama.

Unatuita wanyonge huku ukitupiga danadana kuwaongeza mshahara wafanyakazi

Unatuita wanyonge huku ukiruhusu makampuni yapoteze ajira kwa watu wako kwa kushindwa kujiendesha

Hili jina la Watanzania wanyonge tunaona linatumika kujinufaisha kwa baadhi ya viongozi kujiona miungu watu. Tunaomba likome

NDIO MIMI NI MBOVU WA MGUU LAKINI SIKO TAYARI KUITWA KILEMA
 
Kanyinya

Kwani uwongo?

- Katiba mpya katia kwapani

-Nunge live kaliweka kufiri

-Siasa na vyama vya siasa kazipiga makufuli

- Vyombo vya habari kaviziba midomo

- Polisi anawatumia kufungafunga watu bila makosa

Kweli Tanzania yetu nitaifa la wanyonge kunyongwa hovyo hovyo.
 
Hizi kwangu mimi naziona kama ghiliba,kama kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa!

Kutuita watanzania wanyonge watanzania masikini ni kutukejeli! Watanzania sio wanyonge bali ni wavumilivu na watu tunaoheshimiana.

Tunakutaka usituite wanyonge,huku ukitubomolea makazi yetu tena kwa kukiuka agizo la mahakama.

Unatuita wanyonge huku ukikataa kutuletea katiba mpya itakayo wawajibisha wapindisha haki na mafisadi wote wa serikali yako!

Unatuita wanyonge huku ukituingiza kwenye hasara kubwa kwa kukiuka naagizo ya mahakama.

Unatuita wanyonge huku ukitupiga danadana kuwaongeza mshahara wafanyakazi

Unatuita wanyonge huku ukiruhusu makampuni yapoteze ajira kwa watu wako kwa kushindwa kujiendesha

Hili jina la Watanzania wanyonge tunaona linatumika kujinufaisha kwa baadhi ya viongozi kujiona miungu watu. Tunaomba likome
Nani kakutuma labda kama una jiwakilisha wewe na familia yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama we una mitonyo ucfikir wote, wengne bila kushika jembe hawajala tena kwa mvua za mcmu
 
Naona mahakama ya Kenya imewapandisha mori. Basi changieni kwa hekima maana.....!
 
Hizi kwangu mimi naziona kama ghiliba,kama kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa!

Kutuita watanzania wanyonge watanzania masikini ni kutukejeli! Watanzania sio wanyonge bali ni wavumilivu na watu tunaoheshimiana.

Tunakutaka usituite wanyonge,huku ukitubomolea makazi yetu tena kwa kukiuka agizo la mahakama.

Unatuita wanyonge huku ukikataa kutuletea katiba mpya itakayo wawajibisha wapindisha haki na mafisadi wote wa serikali yako!

Unatuita wanyonge huku ukituingiza kwenye hasara kubwa kwa kukiuka naagizo ya mahakama.

Unatuita wanyonge huku ukitupiga danadana kuwaongeza mshahara wafanyakazi

Unatuita wanyonge huku ukiruhusu makampuni yapoteze ajira kwa watu wako kwa kushindwa kujiendesha

Hili jina la Watanzania wanyonge tunaona linatumika kujinufaisha kwa baadhi ya viongozi kujiona miungu watu. Tunaomba likome
Kweli nyinyi sio wanyonge maana mafisadi wote wamekimbilia kwenu
 
Unyonge wa watanzania anausababisha yeye

Utawala wa sheria ndio dawa ya unyonge,kwa maana kila mtu anakuwa sawa mbele ya sheria,mkiwa sawa mbele ya sheria,masikini na tajiri wote wanasikilizwa bila kujali hali zao,serikali na mwananchi wote wanasikilizwa kwa usawa bila kujali hali zao(serikali ina mapesa,mabomu,bunduki)mfanyakazi na mwajiri wakiwa mbele ya sheria wote ni sawa muajiri huwezi,kwa ubabe tu,kukataa ongezeko la mishahara

Serikali na wamiliki wa majengo,wanapokuwa mbele ya sheria,wanakuwa sawa, hakuna mmoja mnyonge na mwingine mbabe,serikali ikipokea amri za mahakama inatakiwa izitekeleze,ikizuiwa kufanya jambo na mahakama,basi,iache,na tena iwe mfano kwa wananchi kwa jinsi inavyotekeleza maagizo ya mahakama,badala yake,serikali ndiyo inkataa kutekeleza amri za mahakama kuzuia bomoa bomoa na inatumia nguvu za jeshi,katika hali hii mwananchi ataacha kuwa mnyonge mbele ya mbabe serikali?

Nani asiyejua kwamba mahakama haina jinsi ya kutekeleza amri zake na badala yake wanaitegemea serikali? Hakimu/Jaji huandika karatasi kuitaka serikali isifanye,basi,inaishia hapo, je serikali ikienda kufanya jambo,mfano bomoa bomoa ikiwa na FFU mamia kwenye magari,je JAJI/HAKIMU au mahakama,wao watolee wapi jeshi la kwenda kupambana na hao Tanroad(serikali) pamoja na FFU?

Unyonge utaishaje wakati anayeuhubiri ndiye chanzo cha tatizo?

Unyonge utaishaje wakati unazuia Uhuru wa majadiliano na watu wanaishi kwa hofu,badala yake umeruhusu ubabe wa ccm na Polisi ,sasa ccm wako juu ya sheria pamoja na polisi,wanakamata watu hovyo,utarajie watu hawa wasiwe wanyonge?

Uendeshaji wa bunge unatarajia usiwafanye wapinzani wasiwe wanyonge?

Uonevu wa mahakama,na Taasisi za Tanganyika dhidi ya CUF unatarajia utawafanya wazanzibari wasiwe wanyonge?

Unyanyasaji wa wafanyabiashara unatarajia uwafanye wasiwe wanyonge?
 
Back
Top Bottom