Prof. Kabudi: Rais wa Ufaransa amwandikia Barua kumpongeza Rais Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kuingia Uchumi wa Kati

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,705
Rais wa Ufaransa Emanuel Macron amuandikia Barua kumpongeza Rais Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kuingia Uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliopangwa

Serikali imesema katika kipindi cha pili cha awamu ya pili ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itajikita zaidi katika kuboresha uwekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika kujenga uchumi wa nchi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ufaransa hapa Nchini na kuongeza kuwa baada ya kipindi cha kwanza cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli kujikita katika uwekezaji mkubwa wa maeneo ya miundombinu na nishati pamoja na huduma za kijamii sasa serikali inalenga kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi katika ujenzi wa uchumi.

Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Mhe. Frederic Clavier amemkabidhi Prof Kabudi barua ya iliyoandikwa na Rais wa Ufaransa Mhe Emmanuel Macron kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kumpongeza kwa kuiwezesha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ikiwa ni miaka mitano kabla ya muda uliopangwa.

FB_IMG_16069763695138433.jpg
 
RAIS wa Ufaransa Emanuel Macron Amuandikia Barua Kumpongeza Rais Magufuli Kwa Kuiwezesha Tanzania Kuingia Uchumi Wa Kati Miaka Mitano Kabla Ya Muda Uliopangwa
Dira ya Maendeleo 2025 inasema by 2025 kufikia Uchumi wa Kati kwa kufikisha USD 3000?! Sasa Tanzania imeingia miaka 2 kabla ya wakati kivipi wakati By July 2020 ndo kwanza tumefikia USD 1080?!
 
Tunawajulisha kwamba zile dual zenu za kutaka Tanzania itengwe zinazidi kupotea kwa kasi ya kutisha.EU wamesema hawana mpango wa kuweka vikwazo Tanzania Wafuasi wa Lissu poleni kwa kuingizwa chaka. Lissu hajui serikali duniani zinavyoshirikiana.
Iweke hapa mkuu hiyo barua na niya lini. Nadhani ni kabla ya Uchaguzi.
 
Mambo haya hayahitaji hasira ni ya kidiplomasia zaidi

Wanamitandao kuweni na utulivu mliyoyatarajia huenda yasitokee kabisa.

HAPA KAZI TU
 
Back
Top Bottom