Rais wa Msumbiji na ujumbe wake kuwasili nchini wakiwa wamevaa barakoa

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,510
4,224
Naangalia mapokezi ya rais wa Msumbiji Felipe Nyusi pamoja na viongozi na wanahabari alioandamana nao wote wamevaa barakoa pamoja na hayo pia salamu zao si za kushikana mikono.

Siku chache zilizopita waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi aliwasili akiwa hajavaa barakoa na alisalimia kwa kushikana mikono kama kawaida.

Je, hii ndio kusema Msumbiji kuna Corona zaidi kuliko China?
 
Ndivyo wanavyosema, lakini hatujawahi kuona mgonjwa wala kusikia, ila tunalazimishwa kuvaa barakola. Shule toka zilifunga mwaka jana mwezi wa Tatu.

Wanafunzi wengi wamejiingiza kwenye bangi, pombe Mabinti wengi wajawazito, hii yote sababu ya kukaa nyumbani mda mrefu, Maofisini wafanyakazi wanaingia kwa zamzam yaani ni hatari.
 
Ndivyo wanavyosema, lakini hatujawahi kuona mgonjwa wala kusikia, ila tunalazimishwa kuvaa barakola.Shule toka zilifunga mwaka jana mwezi wa Tatu.
Wanafunzi wengi wamejiingiza kwenye bangi, pombe Mabinti wengi wajawazito, hii yote sababu ya kukaa nyumbani mda mrefu, Maofisini wafanyakazi wanaingia kwa zamzam yaani ni hatari
muongo mkubwa
 
barakoa ya mgeni wetu rais wa Msumbiji imeishavuliwa tayari......makofi kwa mgeni wetu tafadhali!
 
Naangalia mapokezi ya rais wa Msumbiji Felipe Nyusi pamoja na viongozi na wanahabari alioandamana nao wote wamevaa barakoa pamoja na hayo pia salamu zao si za kushikana mikono.

Siku chache zilizopita waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi aliwasili akiwa hajavaa barakoa na alisalimia kwa kushikana mikono kama kawaida.Je, hii ndio kusema Msumbiji kuna Corona zaidi kuliko China?
Ukiishi kwa hofu siku zote lazima hiyo hofu ikutese,wavae wasivae sisi tumeshikilia pale pale,kuanza na Mungu na kumalizia na Mungu...
 
Mtoa hoja mbona hujiulizi kama nchini hakuna covid 19 why serikali imepanga 100usd kwa covid 19 certificate kwa wasafiri?kwa nini zisitolewe bure maana nchi haina corona?
 
Naangalia mapokezi ya rais wa Msumbiji Felipe Nyusi pamoja na viongozi na wanahabari alioandamana nao wote wamevaa barakoa pamoja na hayo pia salamu zao si za kushikana mikono.

Siku chache zilizopita waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi aliwasili akiwa hajavaa barakoa na alisalimia kwa kushikana mikono kama kawaida.

Je, hii ndio kusema Msumbiji kuna Corona zaidi kuliko China?

..wewe unapovaa barakoa unamlinda jirani yako.

..na jirani anapovaa barakoa anakulinda wewe.

..hivyo ndivyo barakoa inavyofanya kazi ktk suala zima la maambukizi ya covid-19.

..Ni kweli Waziri wa Mambo ya nje wa China hakuwa amevaa barakoa, lakini wale alioambatana nao walikuwa wamevaa barakoa wakati wote. Hata mlinzi wa Kitanzania aliyekuwa akimlinda Waziri wa Mambo ya Nje wa China alikuwa amevaa barakoa.

..Nadhani tunatakiwa tutumie BUSARA ktk suala zima la kuvaa au kutokuvaa barakoa tunapopokea wageni toka nje ya nchi.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Huyu Rais alivua face mask, asichojua ni kuwa Tanzania hatuna COVID lakini tuna matatizo ya kupumua yanayotokanawna pneumonia.
 
Barakoa inafaida kwa pande za mvaaji na asiyevaa.

Mvaaji anajilinda asiambukizwe na pia asiambukize wengine.
 
Naangalia mapokezi ya rais wa Msumbiji Felipe Nyusi pamoja na viongozi na wanahabari alioandamana nao wote wamevaa barakoa pamoja na hayo pia salamu zao si za kushikana mikono.

Siku chache zilizopita waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi aliwasili akiwa hajavaa barakoa na alisalimia kwa kushikana mikono kama kawaida.

Je, hii ndio kusema Msumbiji kuna Corona zaidi kuliko China?
Siyo kila jambo la kujadiri,tumia muda mwingi kujikwamua kwenye umasikini kuliko inafiki wa maisha ya watu..vitu vyankawaida unapoteza muda kuandika jf
 
Naangalia mapokezi ya rais wa Msumbiji Felipe Nyusi pamoja na viongozi na wanahabari alioandamana nao wote wamevaa barakoa pamoja na hayo pia salamu zao si za kushikana mikono.

Siku chache zilizopita waziri wa mambo ya nje ya China Wang Yi aliwasili akiwa hajavaa barakoa na alisalimia kwa kushikana mikono kama kawaida.

Je, hii ndio kusema Msumbiji kuna Corona zaidi kuliko China?
Waziri wa mambo nje alipokuwa anashuka kwenye ndege alikuwa na barakoa ila alikuja kuvua badae kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili Mkichwa Best. Anadanganya hakuna COVID-19 halafu huyoooooo kaikimbia Dodoma.
Huyu Rais alivua face mask, asichojua ni kuwa Tanzania hatuna COVID lakini tuna matatizo ya kupumua yanayotokanawna pneumonia.
 
Akili Mkichwa Best. Anadanganya hakuna COVID-19 halafu huyoooooo kaikimbia Dodoma.
Muda mwingine akili zenu zinaendeshwa kwa mihemko. COVID-19 sio issue ya kudanganywa, halafu mara ya mwisho yeye kuzungumzia COVID ni muda mrefu kweli.
 
Back
Top Bottom