Tanzania na China zasaini mkataba wa uendelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Mwanza - Isaka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
835
1,000

TRC.JPG

TANZANIA NA CHINA YASAINI MKATABA WA KUJENGA RELI YA KISASA (MWANZA-ISAKA)

Serikali ya Tanzania na China vimeingia makubaliano ya kujenga reli ya kisasa ya Kilometa 341 kutoka Mwanza hadi Isaka

Hicho ni kipande cha tano, ambapo kipande cha Kwanza ni kutoka Dar mpaka Morogoro, Cha pili ni kutoka Morogoro hadi Makutupora

Kipande hiko cha tano kitajengwa na kampuni ya ujenzi ya China. Mkataba wake umetiwa saini mbele ya Rais Magufuli.

---
HOTUBA YA RAIS MAGUFULI (KWA UFUPI)
Naipongeza Kampuni ya Kichina kwa kushinda zabuni ya ujenzi wa reli ya kisasa Kilometres 341 kutoka Mwanza hadi Isaka( mradi una gharama ya Tril 3.0677), nina matumaini watafanya kazi kubwa.

Ujumbe kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping, tumeupokea lakini na mimi nimetuma ujumbe mwingine umfikishie Rais wa China na mimi mambo niliyomueleza ni masuala ya kushirikiana kwa hizi nchi mbili katika masuala ya kiuchumi.

Kwa ujumla mazungumzo tuliyoyafanya yalikuwa mazuri na nimemhakikishia Tanzania itaendelea kushirikiana na China kwa sababu ni ndugu zetu, sasa ni wakati wa Tanzania na China kujenga uchumi kwa nguvu zote na kuonesha ushirikiano mkubwa.

Rais Xi Jinping nimemuomba watusaidie katika miradi mikubwa mitatu kule Njombe, nimemuomba watujengee KM 48 kule Zanzibar.

Nimewaeleza hali halisi kwamba China ni Nchi Tajiri Duniani, na sisi Tanzania tuna mazao mengi, ndio maana kwenye zawadi zangu nimetoa korosho, chai na kahawa, nataka wakaanze kula korosho za Tanzania badala ya Nchi nyingine, huu ndio wakati wa kulishika soko la China. Endapo kila raia wa China atakula korosho nusu kilo, maana yake watakuwa wanakula Tani Mil 750, korosho zote zinazolimwa Tanzania zitaisha.

Nimemuomba Waziri wa Mambo ya Nje China Wang Yi, akafikishe salamu zangu kwa Rais Xi Jinping kwamba watusamehe madeni ikiwemo deni lile tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA, deni la nyumba za Askari USD 137 M, na deni la kiwanda cha urafiki USD 15 M, nimeomba watufutie kwasababu China ni Rafiki zetu, pia wao ni Matajiri.

Nampongeza sana Waziri Wang Yi kwasababu hajavaa barakoa maana anajua Tanzania hakuna Corona na kwa kumuhakikishia nakwenda kumshika mkono tukale chakula.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom