"Rais wa misiba"

Kazi kweli
 
Duh,umenifanya nikumbuke zile enzi zako Nyani McCain na cupcake wako Kelly1

Oh wow.....hahaaaa umenikumbusha Cuppy....nimemmiss kiaina.

Ngoja nimtafute and see what she's been up to...
 
Oh wow.....hahaaaa umenikumbusha Cuppy....nimemmiss kiaina.

Ngoja nimtafute and see what she's been up to...
Nilikuwa najua ile ID ya Kelly1 ilikuwa ya kwako,ukimpata msalimie sana
 
Ni kweli, jamaa kwenye baadhi ya mambo yupo consistent sana....

Rais Magufuli ana mapungufu yake lakini linapokuja suala la msimamo huwa hayumbi.

Kwa wale tunaomfahamu vizuri hatushangai kwa yale anayafanya hasa kutokusikiliza kelele za wanasiasa wanafiki.

Hata kama angeenda kwenye msiba, hawa hawa baadhi ya wanasiasa/wananchi wangekuja na kelele zingine zinazotoa lawama. Kuna wengine wangesema ameenda kuuza sura!

Kuna baadhi ya wanasiasa/wananchi hata Rais Magufuli afanye nini hawawezi kuaacha kulalamika na kukosoa.
 
Nilichokiandika ni ukweli mtupu.

Kikwete alibezwa sana humu ingawa mimi sikuona tatizo la yeye kwenda misibani.

Leo hii huyu Magu analaaniwa kwa kutokwenda misibani.

Ubinadamu ni kazi sana.
Mwisho wa siku, aende au asiende, habadilishi kilichotokea. Tujifunze kukubaliana na ukweli, tusiongozwe kwa matukio
 
Mnafahamu gharama za msafara wa Rais?
 
Nyani Ngabu, naamini ulishawahi kumsina au kumsikia Aristotle na theory yake ya "the mean" au moderation. You become a virtuos person when you avoid extremes and practice modetation in whatever you do. Ukienda to the extremes katika jambo lolote it becomes a vice. Sasa huyu Mh anashindwa kubalance mambo yake. Kila snalofanya anakwenda to the extremes! Angalia mfano la kutosafiri. Yeye kaamua kabisa kutosafiri! Anachojaribu kufanya Magu ni just ili aonekane anatofautiana na Kikwete! Hata kama in the process anaharibu!
 
Unadhani fikla zako ndo za wengine pia?
Haziwezi kuwa sawa kwasababu hata Mimi na wewe tu tumeshindwa kushabihiana katika kufikiri,ila ukweli ndio huo kuwa hawana hamu na yeye.
 

Hiyo moderation kipimo chake ni kipi?

Na unadhani angeenda wangekosekana wa kumlaumu kuwa kaenda?
 
Nyani Ngabu habari ya huko ulipo?

Kwa heshima kubwa naomba nipishane na wewe katika hilo Mimi nikiwa miongoni mwa walioumuita Kikwete "Rais was Misiba" hiyo ni dhahiri kabisa Kikwete alikuwa muhudhuriaji mkubwa wa matukio mbali mbali ya ndani na nje ya nchi yaliokuwa na umuhimu na yasiyokuwa na umuhimu Pote "alikaba nafasi". Jambo ambalo lilikuwa likiligharimu sana Taifa letu.

Back to the topic ni Kwamba Uelewe kuwa Rais ndiye Raia Namba Moja, Amiri Jeshi Mkuu na Mfariji Mkuu Wa Taifa hili, Hivyo alipaswa na anaowajibu Kuwa Faraja Kwetu RAIA katika Jambo lolote kubwa la kitaifa.

Ni jambo la ajabu na kushangaza sana Rais Kutohudhuria mambo makubwa kama Lile la Kuaga Miili ya Wale Askari waliokufa Wakiwa Katika Kutimiza Wajibu wao wa kizalendo Kule Kibiti,

Pia Kwa Mshangao huo huo Ndio unapelekea kutilia shaka "roho" yake ikoje? Yaani Msiba Mkubwa wa Watoto Waliokuwa katika Safari ya kelekea kutimiza Ndoto zao kwa Taifa lao wanapoteza uhai wao alafu mfariji hatokei Ila kuzindua Majengo na Barabara daima hutokea wala hatumi muwakilishi.

Funzo hapo ni Kuwa yeye hayo ya "uzinduzi" ni muhimu zaidi kuliko "faraja" na kutia Moyo kwa Taifa.
 

Okie dokie....you're entitled to your opinion.

Ila hata sijui umepishana nami wapi maana msimamo wangu kuhusu Magu upo wazi....
 
Okie dokie....you're entitled to your opinion.

Ila hata sijui umepishana nami wapi maana msimamo wangu kuhusu Magu upo wazi....

Watu wakisema hawaoni kwa sababu wamepewa Radio waves badala ya visible light, ukiwapa Gamma Rays unakuwa bado hujatatua tatizo lao.

It is entirely conceivable to replace one extreme with another and totally miss the required sweet spot in between.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…