Mipango ya maendeleo walioiweka inasemaje? Maji ya bomba kwa kila mtanzania , elimu bora, kilimo, afya n.k haihitaji kuzunguka na kuanza kuhoji watumishi pamoja nawananchi wakati unajua dawa hakuna fedha ya kuendeshea ofisi hakuna. Kiongozi anatakiwa kabla ya kwenda kwa wananchi akutane na viongozi wa idara ajue kasma walizopata na jinsi walivyotumia kuwahudumia wananchi. Mfano dawa kwenye zahanati zinapelekwa za aina nyingi za tb za kupunguza makali ya ukimwi, hapa watu wakiona gari limelete dawa wanajua ni dawa zote wakiandikiwa dawa wakikosa wanafikiria kuwa dawa zilizoshushwa jana zimeuzwa na hawajui kuwa zilikua dawa za aina gani na za kundi gani. Kwa nini wananchi wasimuulize mkuu wa mkoa juu ya dawa zinazotolewa na serikali zinakidhi mahitaji yao na je zipo? Yeye anatakiwa awe na data zote ili atoe maelezo kamili kwa wananchi wake