Rais wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi alazwa kwa maradhi ya kifua

"Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua. Anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari" - Nukuu. Uangalizi huu ni ule wa "Intensive Care Unit, ICU" ama wa ni wa "High Dependency Unit, HDU"?

Ukifikifikisha umri wa miaka 70 wewe tayari ni "pensioner of God", na kwa kufikisha miaka >95 hapo basi "formular" zote za uhai wa mwanadamu zinabakia kwa Muumba mwenyewe.

Nahisi Taifa letu linakwenda kushuhudia tena bendera zikipepea kwa nusu mlingoti. Asante sana kwa familia kwa kuwaandaa watu kisaikolojia.
 
Safari imewadia, kodi zetu tangu 1995 zitapumua
Wewe utakua ni mtu ambae umepigika kinoma,ndio ukaamua hasira zako uzielekeze kwa wengine,

Unaamini kua kushindwa kwako kumesababishwa na wengine,chuki haziwezi kukutoa kwenye umasikini,kulaumu wengine kwa kushindwa kwako hakuwezi kubadili kitu,pambana ufanikiwe ili usiwe na chuki za kijinga.
 
Huyo naona ana matatizo ya akili yanayomsumbua ambayo yanahitaji matibabu ya haraka sana.maana mtu mwenye akili Timamu hawezi kuandika ujinga aliouandika.
 
Akufe tu zee gani limedinya hadi mama mzazi
 
Mungu ampe wepesi mzee wetu.

Lakini Lucas Mwashambwa, mbali na kuwa chawa, wewe ni msemaji wa Serikali? Mbona una kimbelembele sana?
 
Pamoja na mapungufu yao. Lakini ubinadamu wao unapaswa kutunzwa kama namna ambavyo sisi tunavyotaka kuheshimiwa kama watu.

Tusivuke mipaka sana ya utu. Tukatae matendo yao lakini tuhwshimu na kuenzi utu
Watoto wa Mwinyi wengine tumewakaribisha kutoka Zanzibar, tumesoma nao vizuri, tumekuwa marafiki wakiwa watu wa kawaida sana mpaka tukawa tunatilia shaka kama hawa ni watoto wa rais kweli au tunadanganywa tu, kwa jinsi walivyoishi maisha ya kawaida.

Ni wazi walilelewa kwa maadili ya kuthamini utu wa watu kuliko kujiona wao watoto wa rais.

Kwa hivyo huyu Mzee unaweza kumuangalia kama "Mzee Ruksa" Mwinyi ex president, lakini watu wengine huyu ni mzazi wa rafiki tuliyeishi naye vizuri kwa heshima kubwa.

Hivyo tuangalie hilo pia.

Sio kila kitu siasa.
 
Wakutanikapo tai ndipo mzoga ungalipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…