Rais wa awamu ya 5 akitoka CCM nitahamia Somalia

Rais wa awamu ya 5 akitoka CCM nitahamia Somalia

Nakushauri uende huko Somalia mapema na ikiwezekana washawishi na Bavicha wenzio! Mtu anaye jua kufikiri vyema hawezi kuandika maneno haya maana hakuna asiye jua kuwa Rais wa nchi hii lazima atoke CCM!

Haitakuja kutokea nchi hii Rais kutoka nje ya CCM na wewe unalijua hilo.kuandika haya ni sawa na kuwa na fikra za kuanzisha kikundi cha uasi ndani ya nchi yako!

Pole sana maana CCM itatawala milele na milele.
Nakushauri uende Somalia mapema.

Iwapo rais wa awamu ya 5 atatoka CCM,nitaukana uraia wa nchi hii na kuhamia Somali ambapo hakuna serikali.

Ukiishi katika nchi ambayo unajua hakuna serikali ya kueleweka,basi hata yakitokea yasiyotarajiwa waweza jifariji ni kwasababu hatuna serikali.

Ukweli ni kuwa,inauma sana kuishi katika nchi ambayo serikali siku zote iko likizo!A failed state.

Mfano,waliokwapua hele za Escrow kupitia Stanbic bank eti serikali imeshindwa kuwabaini?

Tuna serikali alafu twiga wanapindishwa ndege na kusafirishwa nje ya nchi tena mchana kweupe!!

Mpokea rushwa anashitakiwa;mtoa rushwa uchunguzi unaendelea!

Miaka mingine mitano chini ya CCM ni bora kuhama nchi.
 
Pia usisahau kuwa CCM ni Chama cha maajabu wanauwezo wa kujichagua wenyewe,wakajipitisha wenyewe,wakajitangaza washindi wenyewe.

Hata pale walipotangazwa kushindwa,kesho yake mwanangu ukakuta mambo yamepinduka miguu juu kichwa chini kageuzwa mshindi na aliyeshinda kageuzwa mshindwa,haya ndiyo maajabu ya CCM.

Wakati mwingine unaweza ukaenda kwenye kituo cha kupigia Kura ukajipigia Kura mwenyewe(Kama ni mgombea)muda wa kuhesabu Kura ukakuta Kura zote ulizopigiwa na mke wako,Watoto wako na wale ambao unauhakika nao kuwa walikupigia Kura zikiwa zimeyeyuka ndani ya box la Kura.

Cha ajabu zaidi ni pale ambapo utakapo kuta hata Ile Kura yako uliokuwa na uhakika kabisa kuwa umejipigia mwenyewe nayo haipo ndani ya sanduku la Kura.
Sasa kuna sababu gani ya kuwa na wapinzani dhaifu kiasi hiki ambao hawana uwezo wa kulinda kura? CCM itatawala milele
 
Huyu mleta mada hajielew kasema atahama nchi, akibanwa anasema atapambana Akili nyingine bana
Somalia utapokelewa vizuri sana, jiandae kuondoka maana Ccm kuondoka n miaka dahari ijayo
 
Nikuulize,Tanzania kuna serikali?

Kama tuna serikali,inawezekanaje,kwa mfano,waliopata mgao kutoka stanbic wasijulikane?

Bora niende Somalia nijue moja.

Teh Teh Naomba umshawishi Slaa muende nae maana kamwe hawezi kuwa Rais wa nchi hii.
 
Mtoa mada ni kielelezo cha fikra za bavicha!

Huyu mleta mada hajielew kasema atahama nchi, akibanwa anasema atapambana Akili nyingine bana
Somalia utapokelewa vizuri sana, jiandae kuondoka maana Ccm kuondoka n miaka dahari ijayo
 
Mi mwenyewe nawaza sana sijuwi itakuwaje ccm ikichukuwa nchi au sijuwi nitaenda nchi gani maana hapa kwetu its too much.
Kuna jiran yangu kachoka sana economically juz kapita home anagawa card za ccm akanitoa kwenye mood kabisa.
 
Bavicha umejisahau nchi hii ilishakombolewa toka miaka ya 60 na hakutakuwa na ukombozi tena! hivi ingekuwa haijakombolewa ungepata huu uhuru wa kuandika unacho jisikia?
Salary Slip

...usiondoke mkuu baki hapa hapa kama shahidi ili siku nchi hii itakapo kombolewa uwe mmoja kati ya watu watakao toa ushuhuda...kumbuka na kuwaombea adui zako Mungu awape maisha marefu ili siku nchi hii itakapo kombokewa wajionee kwa macho yao...
 
Last edited by a moderator:
Huyu mleta mada hajielew kasema atahama nchi, akibanwa anasema atapambana Akili nyingine bana
Somalia utapokelewa vizuri sana, jiandae kuondoka maana Ccm kuondoka n miaka dahari ijayo

Acha kukurupuka!Nimesema damu itamwagika nikimanisha kuna watakaopigania nchi yao.


Hatuwezi kuondoka wote!
 
Acha kukurupuka!Nimesema damu itamwagika nikimanisha kuna watakaopigania nchi yao.


Hatuwezi kuondoka wote!
Hakuna damu itakayo mwagika kabisa na Rais kutoka CCM ataapishwa kwa amani na utulivu! hivi una mtoto wewe au mke?
 
Mtoa mada ni kielelezo cha fikra za bavicha!

Hivi kwa nini Wanajukwaa wanapoikosoa Serikali ya Ccm kwa nini akina Ruttashobolwa Msalani Lizaboni Simiyu yao na timu yao yote huwa wanakimbilia kusema ni mtu wa bavicha yani wakuu tuseme hao niliowataja hawaoni madudu ya Serikali yetu jamani au ni kweli hawa huwa wanalipwa buku 7 maana huwa wanapoitwa buku 7 fc huwa nadhani ni utani.maana wao hao buku 7 kazi yao humu ni kuitetea Ccm na Serikali tusiwe hivyo jamani jina la buku 7 sio zuri ikosoeni Serikali pale inapokosea sio kuitetea
 
Mi mwenyewe nawaza sana sijuwi itakuwaje ccm ikichukuwa nchi au sijuwi nitaenda nchi gani maana hapa kwetu its too much.
Kuna jiran yangu kachoka sana economically juz kapita home anagawa card za ccm akanitoa kwenye mood kabisa.

Mi mwenyewe leo asubuhi hapa mtaani kwangu kapita mjumbe wa serikali ya mtaa anaandikisha majina kwa ajili ya mchango wa maabara.Eti tuchangie kila kaya sh 10,000/=

Nimemuangalia nikatamani nimuwashe makofi ila nikajua huyu katumwa tu nikampotezea.

Wakishatuchangisha baadae wanakuja kujisifu kuwa wamejenga maabara nchi nzima wakati hela zimetoka kwetu.

Hii ni kama kujisifu kusambazaa umeme vijijini kupitia REA wakati mradi huo unawezeshwa na watumiaji wa umeme.Sijawahi kuwasikia wakiwashukuru wateja wa TANESCO badala yake wanaishia kujisifu tu utazani hela inatoka CCM!
 
Back
Top Bottom