Rais sio Mungu naye huwa anakosea

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
Ninampenda sana Rais wetu Mama Samia ila ninaomba kumsahihisha kuwa rais ni binadamu huwa anakosea.

Tukianzia kwa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Marehemu na yeye mama mwenyewe tukisema tuorodheshe mazuri na mabaya yao jamiiforums server haitatosha.

Ushauri kwa mama: Achape kazi tunampenda ila awe makini sana na kauli zitakazomshushia heshima mbele ya jamii. Tunakumbuka hata kauli zake wakati wa kampeni kuwa askari wa CCM huwa hawakosi risasi. Pia tangu aingie ameshafanya makosa kibao hasa kwenye teuzi zake mfano Mwesiga wa TPDC na yule RAS wa Simiyu.

Rais anakosea!
 
Rais anakosea. Mfano unamstafisha mama Mghwila mwenye miaka 62 unamchagua mlevi Makongoro mwenye miaka zaidi ya 62 ili tu kumuenzi baba yake.
 
Rais huwa anakosea. Mfano unachukua jitu mtaani ambalo halijawahi kufanya kazi serikalini tangu lizaliwe halafu unalipa kazi ya uRAS.
RAS lazima atoke kwenye watumishi wa umma. Huyo sio mwanasiasa!
 
Kikatiba HAKOSEI....

Mh.Rais ameongelea "presidential decree" ya uteuzi....Sasa anapoitumia kuteua maDC na maRC anakose kitu gani ?!!!
 
Rais anakosea. Mfano unamchukua mke wa Ndugai aliyekuwa mkurugenzi Bahi kapata ripoti chafu ya C.A.G ila unampandisha cheo kuwa RAS makao makuu ya nchi.
Huu ukweli mchungu, naona kama element za mwendazake zinaendelea.
Ukiharibu ndo kwanza unaenda kula shavu la juu kuliko kule ulikowepo awali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom