Rais Samia ndiye nayecheza ngoma isiyokuwa yake

Son of Nuni

Member
Joined
May 30, 2025
Posts
10
Reaction score
49
RAIS SAMIA ANACHEZA NGOMA ISIYOKUWA YAKE

Katika historia ya Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan ni Rais wa kipekee aliyeingia madarakani si kwa matakwa yake binafsi, bali kwa matokeo ya kikatiba kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa kinywa chake mwenyewe, Samia aliwahi kukiri kuwa hata alipoteuliwa kuwa mgombea mwenza hakutaka nafasi hiyo, akisema “hawezi kuwa Makamu wa Rais.” Samia hakukosea ni kweli Hawezi.
Nitakuonesha kwanini nasema hawezi.

➡️ Ukosoaji Mkali wa Kitaifa na Kimataifa

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Rais anapokea upinzani mkali kutoka ndani ya taifa lake na hata kutoka jamii za kimataifa. Enzi za Magufuli, viongozi wa Afrika waliona Tanzania kama dira ya ujasiri na utawala wa kizalendo. Kenya walitamani “Magufulification” ya taifa lao. Lakini leo hii, vijana wa Kenya (Gen Z) wameinuka kumkataa Samia waziwazi — si kwa chuki, bali kwa mshikamano wa haki.

Zaidi ya hapo, Marekani imetoa onyo la vikwazo dhidi ya Tanzania kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu. Umoja wa Mataifa umetaka maelezo ya kina kuhusu watu waliotekwa, kupotea, na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanaharakati. Bunge la Ulaya nalo limejadili hali ya kisiasa nchini Tanzania — jambo ambalo halijawahi kutokea chini ya uongozi wa rais mwingine yeyote wa Tanzania.

Utakumbuka Rais kikwete na mkapa ndio marais waliofanya vizuri sana kidiplomasia na kujijengea heshima kubwa wao wenyewe na Taifa katika nyanja za kimataifa na wakawa watu muhimu wenye kuhitajika katika kutatua migogoro mikubwa ya mataifa mengine.

➡️ Kutokubalika Hata Ndani ya Chama Chake

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kila muhula wa urais kumalizika, chama huandaa mchakato wa kidemokrasia wa kumpata mgombea mpya wa urais atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu. Mchakato huu kwa kawaida huwa huru, shirikishi na wenye ushindani wa hoja na maono.

Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, Rais Samia Suluhu Hassan aliamua kuvunja utaratibu huu kwa kutumia mamlaka ya kiutendaji kujipitisha kama mgombea pekee wa nafasi hiyo, bila ya kushindanishwa. Hili linaashiria hofu ya wazi ya kushindwa iwapo angeingia kwenye mchakato wa wazi na halali. Akitambua kuwa hana uungwaji mkono wa kutosha ndani ya chama chake mwenyewe, aliamua kufunga milango ya ushindani ili kujihifadhi kisiasa.

Zaidi ya hapo, yeyote aliyethubutu kuhoji uhalali au kupendekeza njia mbadala ya mchakato huo aliondolewa kwenye chama kwa mbinu za ukandamizaji. Hii ni dalili tosha kwamba uhalali wa Samia haujajengwa juu ya ridhaa ya chama chake, bali juu ya mabavu na hila za kisiasa.

Hii ni dhahiri kua Samia hakubaliki analazimisha kucheza ngoma isiyokuwa yake na mwishowe anaishia kuharibu na akishaharibu mbinu pekee ambayo anabakiwa nayo ni kuua wanaompinga, kuteka watu na kuwafukuza uanachama kwa ubabe.

Tujiulize mbona marais wengine waliotangulia walikua hawaogopi kuingia kwenye uchaguzi?? Ni kwa sababu walikua hawana hofu ngoma waliyokua wanaicheza ilikua ngoma yao kwa hiyo walikua wanaijua vizuri.

➡️ Siasa za Hewa na Umati wa Kusombwa

Samia hawezi kufanya mkutano wowote wa hadhara bila kusomba kwenye malori watoto wa shule na wananchi kutoka maeneo ya mbali sana na pale anapofanyia mkutano ili kudanganya jamii kuwa anakubalika kwa kuonesha umati wa watu.

Ukweli mchungu ni kwamba mikutano ya Samia haiwezi kufanyika kwa ufanisi bila kusomba wananchi kutoka mbali, hususan wanafunzi, ili kuunda taswira ya uungwaji mkono.

Katika hali isiyo ya kawaida wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, tulishuhudia kupitia vyombo vya habari picha za Rais Samia akiwatembelea na kuwasalimia watoto wadogo waliolazwa hospitalini, wakiwa kwenye vitanda vyenye mashuka mapya na mazingira yaliyopambwa. Hata hivyo, hakukuwa na taarifa rasmi juu ya sababu ya ziara hiyo ya ghafla, wala maelezo kuhusu kilichowasibu watoto hao hadi kuwalaza hospitalini.

Lakini, kama methali inavyosema, mficha maradhi kifo humuumbua—ukweli uliofichwa ulijidhihirisha. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa moja ya malori yaliyokuwamo kwenye msafara wa kusomba wanafunzi na baadhi ya wananchi kutoka maeneo ya mbali kuja kujaza mkutano wa Rais lilipata ajali mbaya. Ajali hiyo ilisababisha vifo na majeruhi kadhaa, na ndiyo hao watoto waliokuwa hospitalini ambao Rais aliwaendea kimya kimya.

Tukio hilo linaacha maswali magumu juu ya uhalali wa kutumia wanafunzi na wananchi kama “umati wa kusafirishwa” kwa maonyesho ya kisiasa, bila kuzingatia usalama wao. Badala ya kuwajibika au kuomba radhi kwa hasara hiyo, tukashuhudia sarakasi za kisiasa zilizofunikwa kwa kamera na mashuka mapya.

➡️ Ukandamizaji wa Uhuru wa Imani na Mawazo

Tanzania haijawahi kushuhudia wimbi la mashambulizi dhidi ya taasisi za kidini kama inavyoshuhudiwa katika utawala wa sasa. Tumeona kufungwa kwa makanisa kwa misingi isiyoeleweka kisheria—ikiwemo Kanisa la Nabii Suguye na Kanisa la Askofu Josephat Gwajima—bila mchakato wa haki wala maelezo ya wazi kwa umma. Mbali na hayo, tumeona pia juhudi za wazi za kuwatisha na kuwadhibiti viongozi wa dini walioko mstari wa mbele katika kulinda misingi ya maadili ya taifa. Tukio la kushambuliwa kwa Padri Charles Kitima katika mazingira ya kutatanisha, na ukimya wa serikali hadi leo, linaacha maswali mengi yasiyo na majibu.

Hali imefika hadi hatua ya Kanisa Katoliki, taasisi kubwa na yenye heshima duniani, kulazimika kusimama hadharani na kutoa waraka uliosomwa kwenye makanisa yote nchini, kupinga kwa nguvu zote hatua ya serikali kuuza Bandari ya Tanganyika. Hii si ishara ya uongozi imara, bali ni alama ya kuzorota kwa maadili ya kiutawala na udhaifu wa maamuzi yanayokinzana na masilahi ya taifa.

Katika haya yote, kuna jambo moja linalojitokeza wazi: Rais Samia Suluhu Hassan analazimisha kushika usukani wa uongozi ambao kwa kauli yake mwenyewe aliwahi kukiri kuwa hawezi kuubeba. Na kwa sababu hiyo, Samia anacheza ngoma isiyokuwa yake—na matokeo yake ni kuchanganya midundo, kupoteza hatua, na hatimaye kuharibu kabisa muziki wa taifa letu.

Ngoma ya uongozi si jambo la kulazimisha. Ni mwito wa ndani, unaohitaji maandalizi ya kiakili, maono ya kitaifa, na ridhaa ya waliokupa mamlaka. Samia analazimisha kucheza ngoma isiyokuwa yake — ngoma aliyoikataa mwenyewe mwanzoni. Matokeo yake ni migongano, vurugu, ukandamizaji, na upinzani usioisha.

Tunaposema Samia anacheza ngoma isiyokuwa yake, hatumaanishi hachukui hatua. Tunamaanisha hatua zake hazina mdundo wa uhalali, wala hamasa ya kusadikika. Na mtu anayecheza ngoma asiyoijua, huishia kukanyaga miguu ya wengine — na kuharibu ngoma nzima.

Mungu ibariki Tanzania.
 
🙋✍️👌👏👍👊🤝🙏
 
Samia alazimishwe kustaafu siasa.Kama atalazimisha kuwa rais wa taifa letu, basi tujiandae kula nyasi. Kaingia madarakani kwa mserereko lakini kawa dikteta kumshinda Magufuli kwa muda mfupi. Kijana aliyechoma picha yake kapotezwa, Mdude aliyesema Samia anahotuba za hovyohovyo naye kapotezwa, Lissu aliyedai tumehuru ya uchaguzi Samia kakusudia kumnyonga. Watanzani tusiende kupiga kura kumchagua shetani Samia amesha tuvurugia amani yetu.No Reform No Election
 
Jambo moja dhahiri, sa100 analazimisha kusalia madarakani kwa NAMNA yoyote ile, zingatia neno namna!!.
 
Nina hakika gazeti hili linamilikiwa na John Heche😎
 
Back
Top Bottom