Rais Shein: Mafuta na gesi ni mali ya Zanzibar na si Muungano

gwa myetu

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
4,413
4,589
Jana vyombo vyote vya habari vimemwonyesha rais wa Zanzibar akisaini mkataba wa uchimbaji mafuta na gesi huko Zanzibar na akiturushia dongo wabara kwamba tusiyatolee macho kodo hayo mafuta maana hayatuhusu Tanzania bara....

Kwa wataalam wa sheria na wachambuzi hii imekaaje? Je huku bara tukichimba na sisi mafuta na gesi fedha sita kazi katika na si zinakwenda hazina na zinatumika hadi upande wa Zanzibar ? Mbona kama bara tunapunjwa hapa? Ni nani mtetezi wetu maana nimemwona hadi waziri Muhongo anafurahia it means wamekubaliana jambo hilo.

Nahisi hili swala litaleta mgogoro badae maana naona ule mchezo wa " changu changu cha kwako cha wote"

Halafu akasema kisiwa gani sijui ni mali ya Zanzibar na sio Tanzania , hapo ndo akanichanganya kabisa
 


Kuna cha wote na cha wageni
 
Mpaka muda ninaoandika, hakuna mafuga Zanzibar. Labda ni makubaliano ya kufanya utafiti.
 
Gesi ni suala mtambuka liko nje ya hadhi ya shein

Anawadanganya watu tuuuu
 
Ni lazima aseme hivyo hata kama si kweli maana hakuna namna. Angekuwa na ubavu asingemng'oa mwanasheria mkuu wa Zenji baada ya kutoa maoni yake kuhusu katiba.
Zanzibar inatawalika kwa siasa za kilaghai, kibabe, fitna na uzandiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…