Rais Shein: Mafuta na gesi ni mali ya Zanzibar na si Muungano

Shein ameweka bayana mafuta na gesi ndani ya mipaka ya Tanganyika mali ya Tanganyika. Hivo hivo mafuta ndani ya mipaka iliyokuwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar ni mali ya Zanzibar.
 
Serikali ya Zanzibar imekabidhiwa rasmi takwimu (data) za utafutaji wa mafuta na gesi kutoka Serikali ya Tanzania. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo Jumatano Agosti 10, 2022 Ikulu ya Zanzibar kwa kutiliana saini kati ya Waziri wa Nishati wa Tanzania, January Makamba na Waziri wa uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Zanzibar, Suleiman Masoud Makame.

Awali takwimu hizo zilikuwa zikihifadhiwa na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu (Pura), ambapo sasa imekabidhi takwimu hizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA). Hatua hiyo inatoa fursa kwa sasa Zanzibar kuanza kujisimamia katika suala hilo na kuliondoa kwenye Muungano .

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema kuna kila dalili inayoonyesha Zanzibar ina rasilimali ya kutosha ya mafuta na gesi. “Mungu atatuwezesha Zanzibar sasa ianze kuchimba mafuta na gesi, kila dalili zipo za kuwa na rasirimali ya kutosha kilichobaki ni kukamilisha kutoka hapa kwenda hatua nyingine. Hizi data nyingi zipo katika hatua ya 2D tunatakiwa twende hatua ya pili ya 3D na ya tatu ni kuanza kuchimba.”

Dk Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji katika sekta hiyo ili kuendelee kufanya utafiti na kuchimba rasilimali hiyo itakayoleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa Zanzibar. Amesema iwapo Zanzibar ikifanikiwa kupata mafuta na gesi asilia, uchumi utabadilika kwa kiasi kikubwa na tayari kitalu cha Zanzibar-Pemba wameshapata takwimu za awali zinazoonyesha kuwa na kiasi cha trilioni 3.8 za gesi asilia.

Naye, Waziri Makamba amesema takwimu hizo ni muhimu katika mnyororo wa utafiti na utafutaji mafuta na gesi. Amesema vitalu vilivyokabidhiwa ni vitano; kitalu namba tisa, 10, 11, 12 na kitalu cha Zanzibar-Pemba. Amesema tangu miaka ya 1950 zilipoanza shughuli za utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi, data zimekusanywa katika maeneo ya baharini na nchi kavu zinazohusisha mitetemo ya 2D kiasi cha kilometa za mraba 139,000 na data za mitetemo za 3D kilometa za mraba 32,094 na data za miamba kutoka kwenye visima 96 vilivyochimbwa na kuchorongwa.
Kwa upande wake, Makame amesema licha ya utafutaji wa mafuta na gesi kuanza kipindi kirefu, kwa Zanzibar ilikuwa ni nadharia ila kwa kukabidhiwa takwimu hizo sasa wanaanza kazi hiyo kwa vitendo. “Wawekezaji walikuwa wakija na kuondoka kwasababu ya kukosa data hizi, sasa zitakuwa kichocheo cha utafutaji wa kukuza uchumi wa Zanzibar,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Zanzibar kamwe haitofaidika na rasilimali za mafuta na gesi Je nchi gani ya Afrika inayofaidika na mafuta na gesi waliyonayo?

Gadaffi aliuawa Tripoli, Libya. Kenny Sarowiwa aliuawa kikatili kwa kunyongwa hadharani, kisa mafuta na gesi.
Kwa nchi za Africa mafuta na gesi imegeuka kuwa laana na sio baraka tena.

Rasilimali zetu zinanufaisha wawekezaji wa kigeni na Waafrika tunaishia tu kujengewa kashule ka kata kasiko na walimu, vifaa, maktaba, wala maabara. Zanzibar isahau kabisa kujitoa kwenye Muungano.
 
Jana vyombo vyote vya habari vimemwonyesha rais wa Zanzibar akisaini mkataba wa uchimbaji mafuta na gesi huko Zanzibar na akiturushia dongo wabara kwamba tusiyatolee macho kodo hayo mafuta maana hayatuhusu Tanzania bara....

Kwa wataalam wa sheria na wachambuzi hii imekaaje? Je huku bara tukichimba na sisi mafuta na gesi fedha sita kazi katika na si zinakwenda hazina na zinatumika hadi upande wa Zanzibar ? Mbona kama bara tunapunjwa hapa? Ni nani mtetezi wetu maana nimemwona hadi waziri Muhongo anafurahia it means wamekubaliana jambo hilo.

Nahisi hili swala litaleta mgogoro badae maana naona ule mchezo wa " changu changu cha kwako cha wote"

Halafu akasema kisiwa gani sijui ni mali ya Zanzibar na sio Tanzania , hapo ndo akanichanganya kabisa
Kwani nyie dhahabu na madini mengine mnayochimba huku Wazanzibari wananufaika nini?
 
Jana vyombo vyote vya habari vimemwonyesha rais wa Zanzibar akisaini mkataba wa uchimbaji mafuta na gesi huko Zanzibar na akiturushia dongo wabara kwamba tusiyatolee macho kodo hayo mafuta maana hayatuhusu Tanzania bara....

Kwa wataalam wa sheria na wachambuzi hii imekaaje? Je huku bara tukichimba na sisi mafuta na gesi fedha sita kazi katika na si zinakwenda hazina na zinatumika hadi upande wa Zanzibar ? Mbona kama bara tunapunjwa hapa? Ni nani mtetezi wetu maana nimemwona hadi waziri Muhongo anafurahia it means wamekubaliana jambo hilo.

Nahisi hili swala litaleta mgogoro badae maana naona ule mchezo wa " changu changu cha kwako cha wote"

Halafu akasema kisiwa gani sijui ni mali ya Zanzibar na sio Tanzania , hapo ndo akanichanganya kabisa
Hiyo ni sawa kwa sababu katika muungano wetu kuna mambo yanayohusu muungano na mengine siyo ya muungano
 
Back
Top Bottom