Rais Shein: Mafuta na gesi ni mali ya Zanzibar na si Muungano

Jana vyombo vyote vya habari vimemwonyesha rais wa Zanzibar akisaini mkataba wa uchimbaji mafuta na gesi huko Zanzibar na akiturushia dongo wabara kwamba tusiyatolee macho kodo hayo mafuta maana hayatuhusu Tanzania bara....

Kwa wataalam wa sheria na wachambuzi hii imekaaje? Je huku bara tukichimba na sisi mafuta na gesi fedha sita kazi katika na si zinakwenda hazina na zinatumika hadi upande wa Zanzibar ? Mbona kama bara tunapunjwa hapa? Ni nani mtetezi wetu maana nimemwona hadi waziri Muhongo anafurahia it means wamekubaliana jambo hilo.

Nahisi hili swala litaleta mgogoro badae maana naona ule mchezo wa " changu changu cha kwako cha wote"

Tanganyika za Zanzibar ziliungana na kuunda serikali 2. Zanzibar wanatumikiwa na serikali yao na serikali ya muungano. Huku bara tunatumukiwa na serikali ya muungano. Hivyo basi yapo mambo ya muungano ambayo bara na visiwani tunayafanya kwa pamoja na yapo ambayo si ya muungano visiwani wanayafanya kivyao.
 
Tutaufutilia mbali huo mkataba kama tutagundua una ukufi wa ulaghai kama tembe ya ghardali juu ya jabali kwenye kiza cha usiku wa manane.
 
Is that's all you can ask?
Mtu kaja na uzi akitarajia hekima za great thinkers wewe unauliza kifacebook facebook hapa? can't you think a little bit more?

Asante mkuu, maana mi kqa uelewa wangu sijamwelewa Dr Shein ndo nikataka wajuzi watudadavulie tuelewe maana watu wanabishana mtaani na hapa nna uhakika watu wanamajibu
 
Tanganyika za Zanzibar ziliungana na kuunda serikali 2. Zanzibar wanatumikiwa na serikali yao na serikali ya muungano. Huku bara tunatumukiwa na serikali ya muungano. Hivyo basi yapo mambo ya muungano ambayo bara na visiwani tunayafanya kwa pamoja na yapo ambayo si ya muungano visiwani wanayafanya kivyao.

Asante, kwahiyo la mafuta na gesi halipo katika muungano ?
 
Back
Top Bottom