Rais Shein: Mafuta na gesi ni mali ya Zanzibar na si Muungano

Wazanzibari acheni ubaguzi huu. Je, pesa inayopatikana katika madini ya dhahabu, almasi, tanzanite nk huku Bara haiwanufaishi Wazanzibari? ubaguzi wa ovyo kabisa. Na baya zaidi mafuta na gesi yenyewe havijapatikana, vitakapopatikana naona mtarudisha passport!
 
ndio maana tunaoona mbali tuliwaomba wanaojua mipaka ya Tanganyika na Zanzibar kabla ya muungano watueleze ilikuwa baharini,au ilikuwa nchi kavu na kama ilikuwa nchi kavu ni kwa upande wa Zanzibar au upande wa Tanganyika na kama ilikuwa baharini ni kilometa ngapi kutoka nchi kavu?
 
Muungano wa "Change changu. Chako chetu.."
Lakini ni ujinga tu.
Eti walio wengi (Tanganyika) wanawaogopa na wapo tayari kudhulumiwa na waliowachache (Unguja na Pemba).
 
Sasa hapa Mkuu anajaribiwa .................!!

Awamu iliyopita walifanikiwa wakaja na Katiba yao!!
 
Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibar yasiyo Mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba itakuwa batili.
 
Katiba ya jamhuri
Sura ya tatu
64:5
Bila ya kuathiri kutumika kwa Katiba ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba hii kuhusu mambo yote ya Tanzania Zanzibar yasiyo Mambo ya Muungano, Katiba hii itakuwa na nguvu ya sheria katika Jamhuri nzima ya Muungano na endapo sheria nyingine yoyote itakiuka masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ndiyo itakuwa na nguvu, na sheria hiyo nyingine, kwa kiasi inachokiuka Katiba itakuwa batili.
 
Sheria ya mafuta ya Zanzibar inaweza kutenguliwa na ibara hii. Kwa kiasi ilivyoingilia mamlaka ya muungano

"4.-(1) Mamlaka yote ya kutunga sheria juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuw mikononi mwa Bunge. (2) Mamlaka yoyote ya kutunga sheria katika Tanzania Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano yatakuwa mikononi mwa Baraza la Wawakilishi. (3) Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka. (4) Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kuhusu jambo lo lote haitatumika Tanzania Zanzibar ila kwa mujibu wa masharti yafuatayo- (a) sheria hiyo iwe imetamka wazi kwamba itatumika Tanzania Bara na vile vile Tanzania Zanzibar au iwe inabadilisha, kurekebisha au kufuta sheria inayotuka Tanzania Zanzibar; au 49 (b) sheria hiyo iwe inabadilisha au kurekebisha au kufuta "

NA
NYONGEZA YA KWANZA _________ (Imetajwa katika ibara ya 4) Mambo ya Muungano 1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 2. Mambo ya Nchi za Nje. 3. Ulinzi na Usalama. 4. Polisi. 5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari. 6. Uraia. 7. Uhamiaji. 8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje. 9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 10. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha. 11. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu. 12. Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni. 13. Leseni ya viwanda na takwimu. 14. Elimu ya juu. 15. Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa, na gesi asilia. 16. Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo. 17. Usafiri na usafirishaji wa anga. 18. Utafiti. 19. Utafiti wa hali ya hewa. 20. Takwimu. 21. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano. 22. Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine yanayohusiana navyo.
 
Jana vyombo vyote vya habari vimemwonyesha rais wa Zanzibar akisaini mkataba wa uchimbaji mafuta na gesi huko Zanzibar na akiturushia dongo wabara kwamba tusiyatolee macho kodo hayo mafuta maana hayatuhusu Tanzania bara....

Kwa wataalam wa sheria na wachambuzi hii imekaaje? Je huku bara tukichimba na sisi mafuta na gesi fedha sita kazi katika na si zinakwenda hazina na zinatumika hadi upande wa Zanzibar ? Mbona kama bara tunapunjwa hapa? Ni nani mtetezi wetu maana nimemwona hadi waziri Muhongo anafurahia it means wamekubaliana jambo hilo.

Nahisi hili swala litaleta mgogoro badae maana naona ule mchezo wa " changu changu cha kwako cha wote"

Halafu akasema kisiwa gani sijui ni mali ya Zanzibar na sio Tanzania , hapo ndo akanichanganya kabisa
Zanzibar yao, Tanganyika yetu
 
Ukisoma comment ndio utagundua watanzania wengi hawelewi huu muungano jamani muungano huu ni wa serikali mbili zanzibar na Tanzania...tanganyika imemezwa na Tanzania lakini Zanzibar ipo kama zanzibar lakini ipo ndani ya Tanzania ndio maana tunataka muungano wa serikali tatu ili kila upande upate haki sawa ya kimaslahi na uwakilishi na usimamizi wa mambo yake.
 
Back
Top Bottom