Rais Serikali inaangalia tija, wachukue watu kama Maxence Melo waingize Serikalini tulijenge Taifa

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Mh Rais siku zote serikali inaangalia tija kwamba an individual anaifanyia Nini nchi kwa manufaa ya taifa. Cha muhimu kwenye serikali ni deliverence na uadilifu.

Naishauri serikali

Iwachukue vijana wenye mafanikio Katika sekta binafsi iwaingize Serikalini ili watumie vipaji vyao na uwezo wao kuleta tija kwa taifa.

Wazee Wana urasimu (bureaucracy)

Kujaza wazee serikali ni kuongeza urasimu usio na lazima. Mtu kama Maxence Melo hata kama hataki kuajiriwa serikalini unamuita Ikulu unamlisha kiapo cha kijeshi unampa ofisi hapo hawezi kukataa kwani anajua what consequences may be fall him in case akikataa.

Mh. Rais Magufuli, wachukue vijana wabunifu waliofanikiwa kama kina Melo walishe kiapo cha moto kama cha jeshi waingize Serikalini walete tija tujenge Taifa.

Superbug.
 
Kwani unafikiri vijana wenye akili hawapo au hawajawahi kuwepo serikalini?

Mr slow slow wa bunge la katiba na huyu wa sasa wapo sawa?

Yule Katibu Mkuu wa CCM kwa nondo alizokuwa anashusha before kabla hajapewa ukatibu na huyu wa sasa ni mbingu na ardhi.

Unamkumbuka Katibu Mkuu wa CUF Taifa aliyeunga juhudi sasa sijui ana cheo gani huko alikua kichwa sana leo unamsikia?

Hussein Bashe kabla hajawa Naibu Waziri alikuwa na madini kichwani leo ana tonge mdomoni ataongea nini?

Tatizo sio kujaza vijana ila tatizo ni mfumo wanaokutana nao huko.
 
Kwann usichukuliwe wewe Mkuu humu nyote s mnajiita MA great thinker hata wewe nenda kajitolee usimtafutie balaaa mtoto wa WATU unazunguuuka lengo Jf iwe mikononi mwenu

Mifumo ya serikali ikiwekwasawa hapo ndipo watu watatumia bongo zao na SS sasa mtu mmoja Akiamua basi Hakuna cha weledi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humpendi baba wa watu.

Yaani unataka mwenzio akanyofolewe ubongo wamuwekee kimba?

Melo usikubali mwaayego.
 
Back
Top Bottom