Rais Samia zuia vibali vya chakula kwa sasa, utalaumiwa lakini Taifa litakukumbuka kama mkombozi wa kiuchumi

Ameshasalimu amri au hujaskia huko? Endeleeni kupigwa na jua kuwaneemesha wa mjini
Wewe ni mmoja wa madalali mnaoficha vyakula Ili vipande Bei.

Rais anajibu HOJA za LISSU Kwa vitendo.

Soon BASHWE atashusha Bei mzigo aloficha kupitia Kampuni zake na rafiki zake.
 
Hiki kilio sio cha wakulima bali madalali na walanguzi,wakulima chakula washamaliza kuuza tokea mwaka jana, sasa hivi wapo mashambani wanalima.
Tatizo la nchi za kiafrika ni kwamba mbumbumbu ndiyo wanakaa mstari wa mbele kushauri.

kilimo kina kitu kinaitwa "chain of production"

hiyo chain inajumuisha wakulima, viwanda vinavyochakata mazao ya wakulima, wachuuzi wa jumla, wachuuzi wa reja reja mpaka kumfikia mkulima.

ukitazama katika chain hiyo mkulima wa Tanzania hana storage, kuna watu wa kati ndo wenye storage. mabadiriko ya bei yanatokea kutoka kwa mlaji wa mwisho.

watu wenye storage ndiyo waathirika wa kwanza kuathirika na bei. kama ni bei kuporomoka sokoni wao wanakuwa washanunua na kuweka kwenye maghala na ndiyo wa kwanza kupata hasara.

kama ni bei kupanda wao wanakuwa washanunua na ndiyo wa kwanza kupata faida.

lakini hawa watu wanapoathirika athari kwao hurudi mpaka kwa mkulima mwanzo. wakipata hasara wakulima wakitaka kuuza lazima bei watakuta mbaya.

na kama wakipata faida basi mkulima naye anapata faida anapokuja kuuza.

hii mifumo inajiregulate labda serikali iweke ukiritimba wa kuwazuia watu na kuwapa exclusive watu.

mfano kama bei ya mahindi dar ikiwa 1,200, na songea ni 500. watu wengi watasafiri kwenda songea kutafuta mahindi.

ila mtu akiona kufuata mahindi bei ni ile ile kama kununua kwa anayeleta kwa jumla hana haja na ataendelea kutumia watu wa kati. dhana ya kwamba watu wa kati ndiyo wanafaidika ni dhana potofu.

tukikuza kilimo, tunaweza kutoa elimu kwa wakulima kujenga vienge, kuwapatia mikopo ili vitu kama shule za watoto zisiwape presha ya kuuza mapema kwa hasara.

tukihakikisha kiasi kizuri cha pesa kinazunguka kwenye sekita ya kilimo. nchi itapiga hatua kubwa.
 
Sio dhana potofu ndio ukweli wenyewe hamna mkulima anayeuza mchele hata kwa sh 3000,bali anaye nufaika ni mlanguzi.

Issues hapa kila mmoja apate ,mkulima apate na mlaji asiumizwe ndio hoja yangu.

Ila uzuri serikai haijafunga mipaka ,maana mwanzoni walidai bei inapanda sababu watu wa nje wanapandia dau basi waendelee kuuza huko nje kwa bei hizo wanazo ziamua wao, huku wengine tusubirie huo wa kutoka nje wa bei nafuu.

Ila waliokuwa wananufaika na bei ya vyakula ni walanguzi na madalali kwani wakulima wenyewe tokea mwaka jana walisha maliza kuuza vyakula vyao, wana vyakula vya kula wao wenyewe. Brother mimi sio mkulima ila mdogo wangu na degree yake ya Information System analima mpunga na najua ninacho kiongea.
 
Mama ingiza chakula watu washibe, madalali watatumaliza ni walafi, hakuna mkulima anayeuza mazao saa ivi, yuko shambani anapambana na jembe la mkono
 
Tatizo chakula kimepanda sana bei.
Mchele Mwezi wa 8 1700, leo 3400

Bora huo uje ushushe bei.

Ikiwezekana waagize maharagwe na mahindi pia ili bei zishuke
 
Mama kwa kifupi hatua unazochukua katika kilimo sina uhakika na zote lakini hili la kufungua masoko ya nje ni mwarobaini wa kilimo.

Kilimo cha Tanzania kilidumaa kwa sababu ya upofu wa viongozi waliopita.

Naomba nirejee katika hadithi iliyoko katika biblia.

Wamisri walikuwa utumwani misri, walikuwa wanakula na kunywa lakini walikuwa watumwa. Wamisri hawa walivyoambiwa kuwa wanatoka misri utumwani na kwenda nchi ya ahadi, wao walidhani ni swala la kutoka kwenye utumwa na kuanza kula bata mara moja.

Wamisri hawa walianza safari, lakini kumbe ili wafike nchi ya ahadi, walitakiwa kupitia jangwani ambako kuna shida.. Jangwani walikabiliana na njaa na kiu. Wamisri hawa hawakuwa tayari kuvumilia shida walipofika jangwani. walianza kupiga kelele na kutamani kurudi utumwani misri kwani huko walikula na kunywa.

Kama wamisri wale wangekuwa na maamuzi, wangerejea misri na kuachana na safari ya kwenda nchi ya ahadi.Mama umasikini ni sawa na utumwa. Watanzania wamekaa katika utumwa wa umasikini kwa mda mrefu.

Kilimio kinayo nafasi kubwa sana ya kuwatoa watanzania katika utumwa wa umasikini. Lakini ili kilimo kikue na kulikomboa taifa lazima kuna jangwa la kukatiza ili kufika nchi ya ahadi. Ili kilimo kikue ni lazima kufungua masoko ya nje yategemee uzalishaji wetu wa ndani. hapa ndipo penye jangwa sasa. unapofungua masoko ya nje ni wazi kwamba demand itakuwa kubwa kuliko supply na hiyo italeta mfumuko wa bei katika chakula.

Lakini mama mfumuko wa bei ni gea ya kwanza itakayosukuma watanzania kuwekeza katika kilimo. mfumuko huo wa bei utawafanya vijana kufanya kilimo kama ajira. vijana kitu chochote ambacho wakifanya wanapata faida wala hawahitaji kuimbiwa nyimbo watafanya tu. hakuna anayewaimbia vijana kufanya kazi za boda boda, wao wakiona wanaendesha na kuendesha maisha yao watafanya tu na tena serikali itagombana nao kwa kutofuata taratibu.

Mama mfumuko huu wa bei ndiyo chachu ya kuendeleza kilimo chetu, mfumuko huu wa bei ni bei nzuri kwa mazao ya kilimo. kijana akipiga mahesabu kulima ekari moja ya mahindi akajua anaweza kupata kima cha chini cha mshahara kwa mwaka mzima ataenda kulima.

Ukitoa vibali vya kuagiza chakula, kwa kusikiliza wamisri wanaoogopa jangwa na kutamani tanzania irudi misri utumwani tuendelee kula lakini tukiwa utumwani.

Serikali zilizopita zilishindwa kukwamua kilimo kwa kuwa watu waliogopa jangwa. wakaanza kuzuia chakula kuuzwa nje ili kuzuia mfumuko wa bei, walizuia chakula kutengenezwa vitu mbadala kama kuchoma mahindi ili eti kulinda taifa lisiwe na njaa.

Wachumi wa leo wanaojua uchumi wanakwambia "confort zone" ni shida sana. ukitaka kubadiri mfumo wa maisha lazima uachane na confort zone. kama watanzania tunataka kukomboa kilimo chetu ni lazima tuachane na conforte zone ya "cheap food prices"

Tujiandae kununua vyakula kwa gharama ya juu kwa miaka kama 5. wakulimaa wataongeza uzalishaji kutosheleza soko letu la ndani na nje.

Serikali inachoweza kufanya ni kuweka ruzuku kwenye chakula kinachokwenda nje ili bei zetu bado ziwavutie wanunuzi kutoka nje. Serikali isamehe ushuru kwenye mazao yote ya chakula yanayolengwa kuongeza uzalishaji. Sasa ni hatma ya kuvumilia shida hizi za mfumuko wa bei ambao unaletwa na kufungua masoko ya chakula ya nje.

Wakulima kwa sababu wanapata faida wataongeza kilimo na juhudi zao, kwa kuwa chakula kitakuwa hakilipi kodi kuongezeka kwa mazao ya chakula kutaongeza kipato kwa wakulima.

Watanzania wengi wataongeza uwezo wa kununua na hilo ndiyo nguzo kuu ya uchumi bora. hawa watanzania watachochea biashara maana wakulima watakuwa wananunua, kodi zinazopatikana kwenye traansactions zitaongezeka. wakulima wakipata vipato sekita zote zitainuka, wakulima watakuwa wanajenga nyumba nzuri mafundi watapata kazi, wauza vifaa vya ujenzi watapata masoko zaidi.

Kwa kifupi ukifungua kilimo kitafungua sekita zote kwa urahisi.

Lakini hiyo fursa unaweza kuifungwa kwa ama kuzuia wateja kutoka nje wasije kununua chakula ili tusiingie jangwani au kufungua bidhaa za chakula kuja kuua presha hii ambayo tunatakiwa kuielekeza kwa wakulima ili tusiende jangwani kuvuka kuelekea nchi ya ahadi.

Wizara ya kilimo inafanya vizuri ila tu kuna jambo hawakufanya ambalo lingepunguza kelele.
Wewe ni MBUMBUMBU na TAPELI.....,
 
Sio dhana potofu ndio ukweli wenyewe hamna mkulima anayeuza mchele hata kwa sh 3000,bali anaye nufaika ni mlanguzi.

Issues hapa kila mmoja apate ,mkulima apate na mlaji asiumizwe ndio hoja yangu.

Ila uzuri serikai haijafunga mipaka ,maana mwanzoni walidai bei inapanda sababu watu wa nje wanapandia dau basi waendelee kuuza huko nje kwa bei hizo wanazo ziamua wao, huku wengine tusubirie huo wa kutoka nje wa bei nafuu.

Ila waliokuwa wananufaika na bei ya vyakula ni walanguzi na madalali kwani wakulima wenyewe tokea mwaka jana walisha maliza kuuza vyakula vyao, wana vyakula vya kula wao wenyewe. Brother mimi sio mkulima ila mdogo wangu na degree yake ya Information System analima mpunga na najua ninacho kiongea.
Haya mambo yanahitaji utaalamu wa uchumi

na upofu wa utaalamu wa uchumi ndiyo umedidimiza kilimo miaka yote.

no pain no gain

maana ya msemo huo ni nini?

huwezi kutaka kukunja 4 mda wote ukapiga hatua, sometimes inabidi upitie shida ili ufike mahali pazuri. kupitia shida ni pale inapokulazimu, kwamba hakuna njia isiyo na shida.

chaina ya kilimo inajumuisha sekita zote zilizoko kwenye kilimo. upofu wetu na ujinga wetu ndiyo unafanya tuone mkulima siye anayenufaika na kupanda kwa bei.

hii ni mifumo ya uzalishaji, kama wewe humpi mkulima pesa mkononi sasa itamfikiaje mkulima bila kupitia kwa mtu wa kati.

hakuna mtu mwenye akili timamu anataka bei zikibadirika zianzie kwa mkulima. mifumo ya uzalishaji katika kilimo ilivyo ina mda mazao yako kwa nani? kipindi hicho mabadiriko yakitokea yataathiri walio na mazao mkononi.

uzuri ni kwamba masoko yako wazi, hakuna mtu anayezuiwa kununua moja kwa moja kwa wakulima au wakulima kuleta wenyewe mjini.

tuache huu umbumbu wa kutaka kukontrol nani apate na nani asipate. mfumo " yaani chain of production" utajiregulate wenyewe.

sisi tunachokitaka ni kila mtu awe tayari kushiriki anapoona kuna gepu.

swala hili lingekuwa na hoja kama vipato vya watanzania vingekuwa haviwezi kumudu mabadiriko haya ya bei.

chakula ndiyo sekita ambayo ikiwa na mzunguko mkubwa wa fedha watu wengi watachomoka kwenye umasikini.
 
Tatizo chakula kimepanda sana bei.
Mchele Mwezi wa 8 1700, leo 3400

Bora huo uje ushushe bei.

Ikiwezekana waagize maharagwe na mahindi pia ili bei zishuke
Taifa haliwezi kupiga hatua kwa ujinga huu wa bei zilikuwa 1700 na sasa zimekuwa3400.

hakuna ujinga mkubwa tumekuwa tukiufanya nchi hii na kutumia dhana ya kushusha bidhaa ili watu wamudu kwenye umasikini wao badala ya kupandisha vipato vya watu.

mtanzania yoyote mwenye akili atajua ya kuwa kwa sasa bei imetoka 1700 mpaka 3400 kama unavyosema, tutumie mwaya huu kuelimisha wakulima na kuwataka kuongeza kilimo kwa kigezo kuwa bei sokoni ni nzuri. Tuendelee kushawishi wageni kuja kununua.

kwa bei hizo zilivyo kama tungetumia vyombo vya habari na mitandao kuwastua wakulima, mwaka ujao tungepata mavuno mengi sana.

lakini haya mavuno yasije kushusha bei bali wageni waje zaidi wazidi kuchukua.

ndani ya miaka michache tutaongeza uzalishaji wa chakula. tunakoelekea huko mbele ni watanzania wengine kukua na kuanza kutumia technolojia ya ulimaji wa kisasa.

hao wataweza kuzalisha kingi kwa gharama nafuu na kuanza kuyasakama masoko ya nchi kama urusi, ukraine, brazil.

lakini tukikaa kwenye huu ujinga wa chakula kimepanda ama tuzuie au tuagize chakula kushusha bei kamwe kilimo hakitakua. kilimo kikkua hata mshahara wa mwalimu utapanda maana makusanyo ya kodi ya serikali yatapanda
 
Wewe ni mmoja wa madalali mnaoficha vyakula Ili vipande Bei.

Rais anajibu HOJA za LISSU Kwa vitendo.

Soon BASHWE atashusha Bei mzigo aloficha kupitia Kampuni zake na rafiki zake.
Sasa akishusha kwani anaumia nani? Mimi au mkulima? Dalali anampa maisha mkulima
 
Taifa haliwezi kupiga hatua kwa ujinga huu wa bei zilikuwa 1700 na sasa zimekuwa3400.

hakuna ujinga mkubwa tumekuwa tukiufanya nchi hii na kutumia dhana ya kushusha bidhaa ili watu wamudu kwenye umasikini wao badala ya kupandisha vipato vya watu.

mtanzania yoyote mwenye akili atajua ya kuwa kwa sasa bei imetoka 1700 mpaka 3400 kama unavyosema, tutumie mwaya huu kuelimisha wakulima na kuwataka kuongeza kilimo kwa kigezo kuwa bei sokoni ni nzuri. Tuendelee kushawishi wageni kuja kununua.

kwa bei hizo zilivyo kama tungetumia vyombo vya habari na mitandao kuwastua wakulima, mwaka ujao tungepata mavuno mengi sana.

lakini haya mavuno yasije kushusha bei bali wageni waje zaidi wazidi kuchukua.

ndani ya miaka michache tutaongeza uzalishaji wa chakula. tunakoelekea huko mbele ni watanzania wengine kukua na kuanza kutumia technolojia ya ulimaji wa kisasa.

hao wataweza kuzalisha kingi kwa gharama nafuu na kuanza kuyasakama masoko ya nchi kama urusi, ukraine, brazil.

lakini tukikaa kwenye huu ujinga wa chakula kimepanda ama tuzuie au tuagize chakula kushusha bei kamwe kilimo hakitakua. kilimo kikkua hata mshahara wa mwalimu utapanda maana makusanyo ya kodi ya serikali yatapanda
Wakulima mtakoma,nimeshawapa njia mbadala undeni shirikisho lenu lenye Nguvu sio Hilo la ccm mviwata
 
Haya mambo yanahitaji utaalamu wa uchumi

na upofu wa utaalamu wa uchumi ndiyo umedidimiza kilimo miaka yote.

no pain no gain

maana ya msemo huo ni nini?

huwezi kutaka kukunja 4 mda wote ukapiga hatua, sometimes inabidi upitie shida ili ufike mahali pazuri. kupitia shida ni pale inapokulazimu, kwamba hakuna njia isiyo na shida.

chaina ya kilimo inajumuisha sekita zote zilizoko kwenye kilimo. upofu wetu na ujinga wetu ndiyo unafanya tuone mkulima siye anayenufaika na kupanda kwa bei.

hii ni mifumo ya uzalishaji, kama wewe humpi mkulima pesa mkononi sasa itamfikiaje mkulima bila kupitia kwa mtu wa kati.

hakuna mtu mwenye akili timamu anataka bei zikibadirika zianzie kwa mkulima. mifumo ya uzalishaji katika kilimo ilivyo ina mda mazao yako kwa nani? kipindi hicho mabadiriko yakitokea yataathiri walio na mazao mkononi.

uzuri ni kwamba masoko yako wazi, hakuna mtu anayezuiwa kununua moja kwa moja kwa wakulima au wakulima kuleta wenyewe mjini.

tuache huu umbumbu wa kutaka kukontrol nani apate na nani asipate. mfumo " yaani chain of production" utajiregulate wenyewe.

sisi tunachokitaka ni kila mtu awe tayari kushiriki anapoona kuna gepu.

swala hili lingekuwa na hoja kama vipato vya watanzania vingekuwa haviwezi kumudu mabadiriko haya ya bei.

chakula ndiyo sekita ambayo ikiwa na mzunguko mkubwa wa fedha watu wengi watachomoka kwenye umasikini.
Brother kwani nani ka control, je wamezuiwa kuuza nje au ndani kwa bei waitakayo.

Hatukatai kila biashara sometimes ina mtu wa kati, ila huyo mtu wa kati hasituumize issues ni kila mtu apate ,halafu hata hizo principles zenu za uchumi hazipo kumuumiza mtu,kila fans ina ethics zake msisingizie principles za uchumi.

Ndio maana serikali inaagiza chakula bei ita jiregulate yenyewe ila hawaja zuiwa kuuza chakula Kenya,Uganda,Rwanda waaweza kuendelea kuuza.

Ila na rudia statement yangu hamn mkulima anaye uza mchele kwa bei ya 3000 hayupo bali na walanguzi na madalali sasa kwa nini wananchi waumie,hata kama unauza uza kwa bei uhalisia sio kwa kujiamulia.

Uamuzii huu wa serikali haumuumuzi mkulima bali unamuumiza mlanguzi na dalali kwa ujinga wao wa kutaka faida kubwa,kwani wakulima sasa hivi hawana chakula cha kuuza wapo shamba.

Hizi kelele ni za madali na walanguzi waache kujificha kwenye migongo ya wakulima.
 
Sasa akishusha kwani anaumia nani? Mimi au mkulima? Dalali anampa maisha mkulima
Atakaeumia ni dalali ambaye ameficha mzigo store na kupandisha Bei.

Bei anayouza MKULIMA Iko pale pale, ni ya chini, iwe pamba, korosho, kahawa nk.

Madalali msitumie kisingizio Cha MKULIMA kubeba agenda zenu za Siri.

Narudia, Rais anajibu HOJA za Lissu Kwa vitendo,

Wanaonufaika ni wananchi wanapata ujira wa chini ya 10,000 Kwa siku, angalau wataweza kumudu mahitaji ya familia zao ikiwa Mchele utarudi 1800 Kwa kilo au below that margin.

Mungu ibariki TANZANIA.

Aaamen
 
Back
Top Bottom