Rais Samia: Wenye akili za kawaida ndiyo wananikosoa kusafiri nje

Hi
 

Attachments

  • 514E2AB2-4B20-4B2D-8298-2C7F6C3ADC1B.jpeg
    514E2AB2-4B20-4B2D-8298-2C7F6C3ADC1B.jpeg
    28.5 KB · Views: 6
We ambae hata samsung s9 inakushinda utamuweza nani?
Dada hata nikinunua nokia kitochi ni cha hela yangu siyo wewe unajivunia simu za bei mbaya huku unahongwa tu.

Na tutakuhonga sana tu, si mbutuaji wako Magu hayupo?
 
Nimeshuhudia matusi, dhihaka na ghadhabu za Watanzania leo baada ya mh Rais baada ya kutetea kusafiri nje kuwa wananikosoa wana akili za kawaida

''Wale wenye akili za kawaida ni rahisi kulaumu, wanasema ‘Rais anasafiri tu, hakai, hatembelei mikoa’, nikienda mkoani tajenga siasa ya ndani hakuna maendeleo, nikienda nje nakwenda kutafuta fedha za maendeleo.''

Swali akili za kawaida ndio zipi?

USSR
WAPIGA KURA WETU
 
Nafikiri sahihi ni kuwa wenye akili za chini ya kawaida ndiyo hawamuelewi.
Wenye za kawaida kwenda juu huelewa.
 
"Wenye uwezo wa Kawaida wa Kufikiri ( Nadhani akina GENTAMYCINE ) wanasema kuwa ninasafiri sana Nje ya nchi. Ukweli ni kwamba nikisafiri Mikoani nakuza tu Siasa za Ndani ila nikienda huko Ulaya naenda Kuwaletea Pesa kama hizi"

Rais Samia Mwanao GENTAMYCINE nilikuwa sijui kuwa kumbe Kufanya Ziara za Mikoani kwa Rais wa Tanzania ni kuitia tu Njaa nchi na kuendeleza Umasikini ila kumbe ukienda Ulaya unaenda Kuchota Fedha za Watanzania Masikini walizozihifadhi kwa Wazungu.

Halafu Rais Samia Mwanao GENTAMYCINE nilikuwa sijui kuwa kumbe Kura nyingi tunazowapeni pale mkigombea Urais ni za kuwatumeni tu Kuzurula Ulaya kuomba Pesa na kwamba Shida za Watanzania Masikini wengi tutakuwa tunazimaliza Wenyewe na 'Miungu' yetu tunayoiomba na Maombi ya akina Mitume Mwamposa na Kuhani Richard Mwacha.

Sawa Mama Safiri ukatuletee Fedha.
 
Rais lazima atengeneze deals zitakazoiingizia nchi mapato, iwe ni deal za biashara na uwekezaji, au mikopo ama misaada

Sio jambo la kuficha kuwa nchi yetu ni maskini, wananchi wazawa hatuna mitaji ya kuwekeza kwenye miradi mikubwa, uwezo wetu wa kulipa kodi pia ni mdogo

Kufanya zuara za mikoani tu utaishia kuambiwa tuna shida ya maji, barabara, hospitali n.k lakini fedha hakuna, utatatua vipi hizo shida?

Magufuli yeye alikuwa akikopa mikopo kutoka benki za kibiashara, ambayo riba ni kubwa na muda wa kulipa ni mfupi, so unataka Samia afabya hivyo?

Wewe unaenlaumu Samia wewe mchango wako ni upi kuhakikisha nchi inajitegemea kwenye mapato hasa ya kufanya miradi mikubwa? Kulalamikia kodi na tozo?
 
Back
Top Bottom